Albadiri sio Dua , bali ni uchawi wa kiarabu. Ndio maana siku zote inasomwa kuleta madhara tu na sio manufaa. Huwezi sikia mgonjwa akasomewa albadiri ili spine au mwanafunzi akasomewa albadiri ili afaulu mitihani. Albadiri ni uchawi.
Nitangulize kwanza kuwa, Sipendi na Siungi Mkono Ushirikina, na pia sikijuibsana hiki kitu 'Albadir' pamoja na kukisikia Kwa miaka mingi!
Hata hivyo Kwa Uelewa wangu Kuna tofauti Kubwa kati ya DUA na ALBADIR!
DUA Njema ni Sala ya Heri, Baraka, Mafanikio - Mambo yote Mazuri!.....
Lakini Albadiri (kama kweli Iko na inafanya kazi) ni LAANA au Dilaha ya MAANGAMIZI... kama Nuklia vile...!
Huwezi kutegemea Nyuklia ilete Baraka ila Ni ADHABU; KISASI na MAANGAMIZI tu Kwa Waliotenda MAOVU na UONEVU MKUBWA Kwa Watu Wema na Wasio na Hatia...!
Kinachotofautisha tu Albadir isiwe Ushirikina, ni pale Sala hizo zinapofanywa na Watu WEMA, WANAOMJUA MUNGU; WASIO NA MAKANDO-KANDO ya Maisha (Hata kama ni Wakristo)!
Na Lazima Wawe Wameguswa Sana na Wanachokiombea hiyo ALBADIR!
Kinachofanya Ifanye Kazi Mara Moja Si Kafara na Manjonjo mengineyo ya Wasomaji,
Bali ni JIBU LA MWENYEZI MUNGU Maana ndiye Anayesikia Kilio cha Aliyeonewa/ Walioonewa, basi!
Sasa kama Mtu Muovu Akiadhibiwa na MUNGU Hapa hapa Duniani, ukiita Matokeo hayo ni Ushirikina, basi Shauri yako...!
Mimi ni Muumini wa Imani kwamba Adhabu zingine za MANANI Zinatolewa Hapa hapa Ardhini!
Ahsanteni Sana!