Wazee, watoto na wagonjwa Mkoani Geita na mikoa jirani washauriwa kufuatilia kuagwa kwa Rais Magufuli kupitia Vyombo vya Habari

Wazee, watoto na wagonjwa Mkoani Geita na mikoa jirani washauriwa kufuatilia kuagwa kwa Rais Magufuli kupitia Vyombo vya Habari

Inakuaje sasa wenyeji kimsingi ndo waliga kura wake tangu 1995 wakose fursa huyo ilihali watu wa dar waage?
Dar ndio kila kitu mkuu. Kifupi ndio Tanzania yenyewe.
 
Imetajwa sababu ni kuwa uwanja husika ni mdogo hautoshi kuhudumia watu wengi, ni kipi huelewi mkuu.
Mkuu, ambacho kielewi ni kitendo cha kumzungusha kila mahali kwa siku sita badala ya kumzika ili apumzike na familia ipumzike.
 
Hilo ndilo suluhisho, wanawake wakienda waende pekee yao, watakaoenda na watoto warudishwe majumbani kwa viboko.

Watu wa ulinzi na usalama poleni lakini mnamaliziamalizia.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Sioni kabisa mantinki ya kuwaruhusu Zanzibar kumuaga hayati Magufuli na kuwazuia Geita kufanya kitu hicho hicho.

Ni kweli maandiko matakatifu yanasema Nabii hakubaliki nyumbani kwao lakini siyo kwa kulazimisha.

Kamati ya mazishi ya hayati Magufuli ijitafakari kwa upya!
 
Sasa kama ni hivyo kuna haja gani ya kuzungusha mwili kwa siku 5 wakimtesa Mama JPM na familia yake kwa uchungu walionao wakati watu wanaweza kufuatilia kwenye TV .... Kwa nini wasiende moja kwa noja Chattle!
Hili nalo neno. Mimi naamini kwamba njia bora ya kuomboleza kifo cha Magu siyo kuona mabaki ya mwili wake, waingereza wanaita 'body remains' Yaani maiti, bali ni kuyaishi yale mema yake. Kama taifa tusijishushe mno, hata kufikia hatua ya kuuzururisha huo mwili mabarabarani, tena kwa siku kadhaa.

Tungeepusha pia misiba ya waliokufa na kujeruhiwa eti wanaaga mwili.

Watanzania waaswe kujikita zaidi katika kumuenzi, siyo misongamano isiyokuwa na maana wala toka.

Shida hapa naona viongozi hawajiamini, wanahofia jamaa anaweza zinduka akawatumbua kwa kutojipendekeza vya kutosha!

Viongozi kwetu, pamoja na Rais, songeni mbele, Magu ndiyo basi tena mwisho wake umetimia
 
Ule wa kimataifa wa soka haujaishaaa? Kwakwakwakwa!
Sio uwanja wa mikutano ni wa ndege au kiswahili hujui tofauti ya uwanja wa mpira au wa hadhara na uwanja wa ndege? Chadema you are so stupid. Kilimanjaro international airport huwa mnaitumia kwa mikutano ya kisiasa au kuaga Ndesamburo?
 
Sio uwanja wa mikutano ni wa ndege au kiswahili hujui tofauti ya uwanja wa mpira au wa hadhara na uwanja wa ndege ? Chadema you are so stupid.Kilimanjaro international airport huwa mnaitumia kwa mikutano ya kisiasa au kuaga Ndesamburo?
Si kuna Uwanja wa Mpira ambao tuliambiwa na Kalemani unajengwa hapo Chatto, inakuwaje tena uwanja mkubwa hautoshi?

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Sio uwanja wa mikutano ni wa ndege au kiswahili hujui tofauti ya uwanja wa mpira au wa hadhara na uwanja wa ndege ? Chadema you are so stupid. Kilimanjaro international airport huwa mnaitumia kwa mikutano ya kisiasa au kuaga Ndesamburo?
Tundu Lissu aliwashauri acheni kuuzurulisha mwili wa marehemu mkajifanya vichwa ngumu! Ona sasa maji yamezidi unga.
 
Back
Top Bottom