Waziri Abdallah Ulega: Madai ya Samaki kuhifadhiwa kwa maji ya maiti ni hisia tu

Huyu naye hakupashwa kusema kauli ile mbele za watu bila ushahidi wa kisayansi. Huyu ndiye alikuwa Waziri wa fedha. kweli mtu kama huyto anafaa nafasi aliyo nayo? hivi mama alimchagua kwa vigezo vipi? nadhani wanajuana toka utotoni...
Wewe sangara wabichi wanasafirishwa kwa basi Kutoka Mwanza hadi Dar ndani ya visalfeti halafu unambishia VP?
 
Ataambiwa ajiuzulu coz amehujumu uchumi wa kanda ya ziwa!

Ndipo kati ya Hawa ;-ulega,uwesu na jabali awe makamu halafu afanikishe next stage!!
 
Huyu naye hakupashwa kusema kauli ile mbele za watu bila ushahidi wa kisayansi. Huyu ndiye alikuwa Waziri wa fedha. kweli mtu kama huyto anafaa nafasi aliyo nayo? hivi mama alimchagua kwa vigezo vipi? nadhani wanajuana toka utotoni...
Ukweli ni kwamba matukio kama hayo yamekuwepo tena kwa muda mrefu sana.

Na hii ndio ilipelekea hata Biashara ya mabucha ya Samaki mikoani ikaporomoka miaka kadhaa iliyopita.

Tatizo kubwa hapa ni Nafasi ya mtoa kauli "VP".
Ambaye ameitoa mbele ya hadhara tena mbele ya wataalamu wa Afya.

Yeye kwa mamlaka yake anayo nafasi ya kutoa amri kwa mamlaka husika za uhifadhi wa madawa hayoili, kuchukuliwa hatua za uzembe wa kuruhusu madawa hayo kuingia mikono isiyostahili.

Pia angehakikisha vyombo vya dola vinalikomesha jambo hilo mara moja.
Tena hiyo ingekuwa amri ya kimyakimya kwa vyombo vya usalama kufanya utekelezaji wake.

Sasa badala yake ametoka hadharani tena mbele ya vyombo vya habari na pia baadhi ya wataalamu wa kutoka nje.
Na kutoa kauli ile. . ....jambo ambalo linaweza kusababisha Madhara makubwa kwenye sekta ya viwanda vya Samaki vinavyosafirusha samaki toka ziwa Victoria nje ya nchi.

Wazungu hawakawiagi kutoa tamko la kuzuia vitu au chakula chochote wanachokihofia kwa usalama wa afya zao.
 

Kwani Dkt. Mpango anasema je?
 
Sipati picha kauli ile ya awali ingetolewa na mtu wa upinzani... in short hivi sasa ama angekuwa Polisi Oysterbay au anatafutwa na polisi!!

Magenge ya vijana wa CCM nao yangekesha mitandaoni kusema Wapinzani wanahujumu sekta ya uvuvi!! Lakini kwavile kasema Mpango, wana-justify!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…