mwelemimmongo
Member
- Feb 16, 2021
- 95
- 75
Mwandishi umeniwahi nilitaka niandike na mie pia, jamani tuache siasa kwa Mambo ya maana nafaka ina paa baraa mfano mchele simiyu-bariadi ni 2000 kwa kilo,mpunga debe 12000-15000, mahindi ndo hayakamatiki debe kwa Sasa vijjini 15000 hii Bei ya wiki hii tu,mjini 15000-17000,mtama 15000 pia,viazi vitamu 5000kwa debe,ushauri fungeni mipaka nafaka isitoke nje chakula ni kichache Sana watu wanatafuta Ila Bei upo juu kwa sababu nafaka inakusanywa baraa vijiji wanapeleka Kenya baraa, Sasa ni hatari kweliIndia mwezi jana ilipiga marufuku kuuza ngano nje ili kulinda soko la ndani make bei ya ngano kule India ilikuwa imeanza kupanda kwa kasi sana. Kumbuka wale Ngano ndo chakula kikuu na Wali pia.
India ni mzalishaji mkubwa wa Ngano Duniani lakini iliona hatari kwa raia wake kuuziwa ngano bei ya juu akaamua kupiga pini.
Indonesia alipiga ban kuuza mafuta ya kula nje kulinda soko la ndani. Kwa kifupi nchi nyingi kwa sasa zinajihami kwa kuzuia uuzaji wa vyakula vikuu hasa nafaka.
Tanzania tunaishi Dunia ya kutafuta sifa sana, Bashe ukimsikia ni mtu wa kutafuta sifa kwamba nchi ina chakula cha kutosha kwa asilimia zaidi ya 100.Bei ya mahindi kwa sasa inazidi kupaa juu sana na haijulikani itaishia wapi.
Ukweli ni kwamba chakula hasa nafaka kuu Mahindi itapanda sana iliopo chache inauzwa nje kwa kasi ya kutisha.
Hapa kinachofuata ni baadae Serikali iagize mahindi Mexco au Brazili na hao hao wakina Bashe wapige cha juu au wakina Bashe waanze kupiga pesa kwa kutoa vibari vya kuagiza mahindi huko Mexco na Brazili.