Waziri Bashe aache sifa apige marufuku Uuzaji wa Chakula nje

Waziri Bashe aache sifa apige marufuku Uuzaji wa Chakula nje

Wewe mleta mada aliyekuleta mjini nani wakati unajijua huna hela? Wenzako wanaishi bila shida kabisa.

Yaani unataka mkulima aingie hasara kwasabb yako wewe unashinda ukibeti?

Nenda kalime mahindi yako ndiyo usiyauze nje. Sisi tuliojiajiri kwenye kilimo tunalima kilimo biashara na tunauza popote ikiwemo nje ya nchi.
 
Unataka kilo ya mchele au mahindi iwe Tsh ngapi? Ni lini wakulima wa Tanzania watapata bei nzuri ya mazao Yao? Bei hupangwa na market forces za supply and demand, period

Wacha bei zipande, wakulima wanufaike ili watu watamani kuhamia kwenye kilimo badala ya umachinga kila mahali. Vyakula vikiisha na sisi tutanunua nje, na pia itakuwa ni wakati mwafaka kufungua kilimo cha mazao mengine ambayo yanakomaa kwa muda mfupi. Hafi mtu Tanzania kwa sababu ya njaa
 
Mtoa uzi kasema

"km vp serikali inunue ihifadhi baadae wauze kwa bei ya serikali,,

Au nmemquote vibaya
 
Duniani kote kuuza nafaka nje ni kawaida sana Ndio maana Ukraine na Russia wanatamba na ngano yao

Jambo la msingi ni kuongeza sana kilimo na haswa cha umwagiliaji
Ni jambo la kushangaza sana karne ya 21 bado hatujui faida za umwagiliaji na bado kuna watu wanaangalia juu kusubiri mvua zinyeshe wakati Neema zote zipo chini na nyie ni kuzitumia tu

Bado ni primitivism
60m bado viongozi walewale tu na akili zile zile miaka nenda rudi na ndio wanaturudisha nyuma

Angalieni duniani kwingine
Nilienda Thailand Damnoen Saduak floating market
Huo ni mto na wanautumia vizuri sana kwa wakulima wote wa mbogamboga na matunda wanakuja na mitumbwi iliyojaa kila siku

Hao wanajua kuzitumia Neema walizozikuta duniani na sio leo wameanza bali miaka maelfu yaliyopita

Nimeenda pia kutalii Egypt mto upande wapo wafugaji na upande mwingine Wakulima asubuhi wanasalimiana

Sisi wakulima na wafugaji kutwa kuuwana kama wanyama pori

Hawa viongozi wakikaa bungeni sijui huwa wanashindwa nini kuongelea masuala na sheria za kuruhusu Mito yote itumike kwa masharti kwa ajili ya ulimaji?

Nchi nyingi nilizotembelea huwa naenda kujionea maendeleo yao na jinsi wanavyoishi na kuzunguka mikoa yao

Oman nimeenda Dakhiliya wana mkondo wa maji unaitwa Aflaj irrigation systems Yaani una miaka zaidi ya 5000 mpaka leo unategemewa na wakazi kibao

Je sisi viongozi wetu wanapoenda nchi hizo kwanini wanaishia Ikulu na kuombaomba na kurudi ?

Hizo delegation wanaoenda huwa wanaenda kununua zawadi za watoto wao tu na Suits zao tu
 
Msitake kuturudisha nyuma tulikotoka!

Sasa hivi kilimo ni deal.

Ile kusema Jembe halimtupi mtu ndio itakuwa dhahiri shahiri.

Sema tu wakulima wadogo hawanaga means of storage kwaajili ya kuwaweza kufanya speculation and hedging otherwise uchumi wao ungekuwa unapaa sana na kuvutia wengi kujihusisha na kilimo.
 
Halafu kilimo ukiamua ukawa na mtaji na usimamizi mzuri unafanikiwa sio mpaka ushike jembe kwa mikono yako mwenyewe.
 
Nilishaandika mara kadhaa hamchukulii serious,,sasa tusubiri tuone km serikali yetu haitaingia kwenye dhahama ya kutafuta chakula cha misaada, fanyeni upembuzi, uone faida ya kuuza na faida ya kununua baadae,km vp serikali inunue ihifadhi baadae wauze kwa bei ya serikali,,leo ruhusu watu wavute sigara, baadae dawa za kansa unanunua bei ya ajabu, faida iko wapi?? Mimi kunguru muoga
Ungekua umewahi lima hata tuta moja la nyanya usingekuja kuandika huu upuuzi. Yaani mkulima akutunzie wewe chakula? Kiishe ili msimu ujao kilimwe zaidi kisipo uzwa na kisipoisha mkulima msimu ujao hatolima by the way msimu wa mavuno ni huu kiishe ili maghala yawekwe chakula kingine.
 
Sasa hivi China na India wanahitaji mihogo na parachichi kwa wingi.

Hizo ni fursa.

Serikali itengeneze mazingira wezens hi ya hayo masoko,

Mkulima akishavuna ajue kama yatakuja kununuliwa shambani au mkulima afanye arrangement ya kufikisha Kurasini kwaajili ya export baada ya kuweka gharama zake zote mpaka mzigo kufika Kurasini.

Je contact za mawasiliano na wateja hao wa China na India mkulima atazipata wapi?

Hata pilipili kichaa nasikia ni bonge la deal zinahitajika nje.

Handeni ardhi inakubali hivyo vyote.

Uzuri wa mihogo na pili-pili zinastahamili ukame.
 
Mtoa uzi kasema

"km vp serikali inunue ihifadhi baadae wauze kwa bei ya serikali,,

Au nmemquote vibaya
Amesema ipige marufuku. Na kichwa cha habari ndivyo kinavyosema. Mbona unakuwa na ubishi kwa kitu ambacho kinaonekana wazi?
 
Ungekua umewahi lima hata tuta moja la nyanya usingekuja kuandika huu upuuzi. Yaani mkulima akutunzie wewe chakula? Kiishe ili msimu ujao kilimwe zaidi kisipo uzwa na kisipoisha mkulima msimu ujao hatolima by the way msimu wa mavuno ni huu kiishe ili maghala yawekwe chakula kingine.
Huu ujinga wa kupangia wakulima wauze wapi mazao yao ni wa kijinga na unakuta watu wanakaza mishapa kusema ujinga kama huu. Wakulima siyo vibarua wa watanzania. Anayeona maisha magumu apeleke tumbo mashambani akalime. Kama mshahara hautoshi waliye na CCM inayofuja fedha kama mchwa.
 
Sasa hivi China na India wanahitaji mihogo na parachichi kwa wingi.

Hizo ni fursa.

Serikali itengeneze mazingira wezens hi ya hayo masoko,

Mkulima akishavuna ajue kama yatakuja kununuliwa shambani au mkulima afanye arrangement ya kufikisha Kurasini kwaajili ya export baada ya kuweka gharama zake zote mpaka mzigo kufika Kurasini.

Je contact za mawasiliano na wateja hao wa China na India mkulima atazipata wapi?

Hata pilipili kichaa nasikia ni bonge la deal zinahitajika nje.

Handeni ardhi inakubali hivyo vyote.

Uzuri wa mihogo na pili-pili zinastahamili ukame.
Wewe unasema kitu ambacho serikali ya CCM haitakaa ifanye kwani wananchi wamejilalia kama nyumbu. Ni hivi: hakuna serikali duniani kote itakayowajibika kwa wananchi wake bila wananchi kuwa wakali kama nyuki kupinga ujinga ujinga wa serikali. Hata nchi zilizoendelea hazijaendelea hivi hivi. Ni wananchi wake ndiyo wamepeleka hinya hinya viongozi wao.
 
Nilishaandika mara kadhaa hamchukulii serious,,sasa tusubiri tuone km serikali yetu haitaingia kwenye dhahama ya kutafuta chakula cha misaada, fanyeni upembuzi, uone faida ya kuuza na faida ya kununua baadae,km vp serikali inunue ihifadhi baadae wauze kwa bei ya serikali,,leo ruhusu watu wavute sigara, baadae dawa za kansa unanunua bei ya ajabu, faida iko wapi?? Mimi kunguru muoga
Bashe usisikiloze huu upuuzi
 
Bashe usisikiloze huu upuuzi
Katika moja ya mambo machache niliyowahi kukubaliana na JPM kimsingi ni swala la biashara ya mazao. Kuna mwaka JPM alifanya makosa makubwa sana ya kuzuia mazao yasiuzwe nje kwa kisingizio cha kuwasaidia wananchi wa kawaida na ughali wa bidhaa masokoni, jambo hili lilipelekea hasara kubwa sana kwa wakulima. JPM baada ya tathmini pana aliona hili jambo ni upuuzi na kuja na kauli kwamba- MKULIMA ANARUHUSIWA KUUZA MAZAO YAKE POPOTE PALE, MWANANCHI ANAYEONA UNGA UMEKUWA GHALI ABEBE JEMBE AKALIME AMA SIVYO AFE NJAA NA SERIKALI WALA HAITAINGILIA HILO 😁 😁 .
 
Ndio inavyotakiwa yaani mkulima aumie Kisa wa mjini anataka anunie Kwa bei ndogo? Haipo hiyo.
 
Wewe unasema kitu ambacho serikali ya CCM haitakaa ifanye kwani wananchi wamejilalia kama nyumbu. Ni hivi: hakuna serikali duniani kote itakayowajibika kwa wananchi wake bila wananchi kuwa wakali kama nyuki kupinga ujinga ujinga wa serikali. Hata nchi zilizoendelea hazijaendelea hivi hivi. Ni wananchi wake ndiyo wamepeleka hinya hinya viongozi wao.

Ni sahihi kabisa ulichoandika.

Ni werevu wachache sana ambao sanaweza kufikiri ulichoandika.

Ngoja tuendelee kulala usingizi wa pono mpaka karne hizo zijazo sijui vizazi vyetu vya ngapi maana sijui ni mfumo wa elimu uliopo au ni kwa sababu gani?!

Hata wanapokuwepo wapinzani wa kikatiba wanasakamwa wanapigwa vita ili wasiamshe walolala?!

Yaani!
 
Sasa hivi China na India wanahitaji mihogo na parachichi kwa wingi.

Hizo ni fursa.

Serikali itengeneze mazingira wezens hi ya hayo masoko,

Mkulima akishavuna ajue kama yatakuja kununuliwa shambani au mkulima afanye arrangement ya kufikisha Kurasini kwaajili ya export baada ya kuweka gharama zake zote mpaka mzigo kufika Kurasini.

Je contact za mawasiliano na wateja hao wa China na India mkulima atazipata wapi?

Hata pilipili kichaa nasikia ni bonge la deal zinahitajika nje.

Handeni ardhi inakubali hivyo vyote.

Uzuri wa mihogo na pili-pili zinastahamili ukame.

Mkuu mimi kila kukicha na supply vyakula na hapa fursa zilizopo ni vyakula vyenye mda mrefu kuharibika ambavyo tunaweza kufanya kwa sababu vyakula na matunda na mbogamboga zetu tunategemea zaidi msimu

Kwa hiyo kwa kukausha kwa mpigo kama vile pilipili zilizokaushwa au karanga na Korosho na hata spices kama karafuu na hiliki

Soko hili lipo sana Ulaya na hata Uarabuni
Ila ukitaka vibali ndio utajua tuna viumbe wa ajabu kabisa kwenye Taifa letu
 
wasizuie lakini kuwe na udhibiti

ila watanzania bhana; wakiruhusiwa nongwa wakizuiwa nongwa.
 
Back
Top Bottom