Waziri Bashe aache sifa apige marufuku Uuzaji wa Chakula nje

Una hoja kamanda! Serikali yetu inapaswa kuchukua hatua za tahadhari kubwa katika swala la chakula; dunia inakabiliwa na mgogoro mkubwa wa chakula kutokana na vita baina ya Ukraine na Urusi! Umoja wa kitaifa imeshatoa ANGALIZO, nasi ni wakati wa kukaa chonjo kabla hayajatukuta! Na mtu anayebeba dhamana hiyo anaitwa HUSSEIN MOHAMED BASHE kama Waziri wa Kilimo na Chakula!
 
Kalime, wacha porojo.

Bado hapa kwetu kuna mwanya (gap) mkubwa wa uzalishaji, huwezi kufananisha na India ambao wapo exhausted.

Wacha wakulima wapate pesa za kuongeza mitaji yao.

Bei zitashuka kwa mbinu mpya za kilimo, huwezi kutegemea miaka nenda miaka rudi kutatua tatizo kwa njia ileile ya kuzuwia kuuza nje, lazima zitumike njia mbadala.
 
Unatetea usichokijua.
Anayefaidi bei za chakula kupanda ni mlanguzi na mfanyabiashara.
 
  • Kufunga mipaka ni njia za kizamani kuendesha nchi na mashauriabo ya kigeni - primitive.
  • Haya ni mawazo mgando yalioanza zama za Ujamaa; na kufanya kilimo kudumaa.
  • Kwa Afrika, ikiwemo Tz, kilimo ndio sekta duni kuliko zote kutokana na uvivu wa kufikiri uliopelekea kukosekana kwa ushindani wa bei za bidhaa zake.
  • Vijana wanakimbia kilimo kwa kutokuwepo bei halisi. Watu wazoee uhalisia, si kuishi kwenye kinga ya kufungiwa mipaka - kudekezwa.
  • Gharama za kilimo ni kubwa, je nani yupo tayari kufilisika?
  • Wageni wananunua na serikali inunue kwa ajili ya watu wake. Je yale maghala ya serikali ni kwa ajili ya kuhifadhia nini? Kwa ajili ya nani?
  • Hao wanaokuja kununua ni jirani zetu, ndg zetu. Msidhani Tz haiwezi kupata janga litakalolazimisha kuomba msaada kwa jirani. ACHENI ROHO MBAYA ENYI MASKINI!!
 
Unatetea usichokijua.
Anayefaidi bei za chakula kupanda ni mlanguzi na mfanyabiashara.
Huyo bibi hawezi kulijua hili, anayenufaika na bei hizi ni mlanguzi anayejiita mfanyabiashara na madalali wa mazao na labda wakulima wakubwa ambao ni wachache.

Wakulima wadogo ambao ndo wanalisha nchi hii wanaishia kuuza mazao shambani kwa bei chee, wakibahatika kuvuna watapewa bei ndogo na walanguzi ambao pia wanabana mizani au kujaza lumbesa.​
 
Yes
Nina wasiwasi Bashe ni mnufaika wa biashara ya mazao.
Atakuwa mkulima mkubwa au mnunuzi mkubwa so anafaidi kwa kufunguliwa mipaka.
Sasa hivi wakenya wananunua mazao Shambani vijijini yakiwa bado mabichi...huku ndio mkulima kufaidika?
 
Unatetea usichokijua.
Anayefaidi bei za chakula kupanda ni mlanguzi na mfanyabiashara.
Lini na wapi iliacha kuwa hivyo?


Ni pale tu mkulima atapojijuwankuwa yeye pia ni nfanya biashara, na hivho ndicho kinachofabyikabkwenye kituo cha mafunzo cha Bashe. Licha ya ukulima pia vijana haohao wanafundishwa ujasiriamali.

Naona hilo ulikuwa hulifahamu. Bashe kajikita katikankuhakikisha nganyabiadhara anapata haki yake na mkulina anapata halubyake bila kudhulumiana, lakini usifikiri kunafanyika uchawi, jugumba na kufumbua mambo yabadilike, hapana. Hayo ni mambo ya planning na implementation, circle zake ni miezi minne minne kwa uchache, kwa niaka miwili mpaka mitatu ndipo tutayaoba matokeo chanya
 
Yes
Nina wasiwasi Bashe ni mnufaika wa biashara ya mazao.
Atakuwa mkulima mkubwa au mnunuzi mkubwa so anafaidi kwa kufunguliwa mipaka.
Sasa hivi wakenya wananunua mazao Shambani vijijini yakiwa bado mabichi...huku ndio mkulima kufaidika?
Na mimi nina wasiwasi huo huenda jamaa ni mnufaika wa biashara ya ulanguzi wa mazao na labda anamiliki ma godown makubwa, na hii inaweza ikawa ni move ya kuhakikisha chakula kinawafikia ndugu zake huko somalia. Kwanza inakuwaje wafanyabiashara kutoka nje wanaruhusiwa kwenda kununua mazao mashambani? wao wanatakiwa kununua kwenye minada mikubwa, mfano pale soko la mahindi Kibaigwa Kongwa.

Inavyoonekana jamaa wamepandikiza machawa kupinga kila hoja inayoletwa kuongelea kuhusu bei ya chakula kupanda. Maana kila uzi ukipandishwa wanajaa kupinga na kukashfu kila anayekuwa anaunga mkono. Wote wana maneno yanayofanana, utasikia nenda kalime, mara hakuna chakula cha bure, sasa unajiuliza ni nchi gani ambayo kila mtu yuko analima mashambani.​
 
Kuna nguchiro haya hawayaelewi wanashupaza shingo kutetea hata wasichokijua kwenye biashara ya nafaka nchini.
 
Siyo kweli, acheni uwongo. Wakulima siyo wajinga kama nyinyi mnavyotaka waonekane wajinga. Hakuna mkulima ambaye hajui kuwa kuna Demand kubwa ya mazao!!

Ukiyafuata mahindi tu shambani anajuwa demand imepanda, anakuuzia juu
 
Hizo nadharia tu zitapigiwa kelele mwaka mmoja, mwishowe watapewa mitaji badala ya kuanzisha kilimo watafungulia maduka ya nguo mjini.
Ule mkakati wa kijani wa JK unakumbuka uliishaje?
Nchi hii kila kitu siasa
 
Wakazi wa town tunatozwa tozo mbalimbali kibao ili wakulima wapewe mbolea za ruzuku halafu msosi wanawauzia wakenya na wazambia. Sijui tunatobolea wapi
 
Hapa hakuna chawa wote wanachangia humu ambao unaona hoja zao zinafanana kwa sababu wao ni wahusika wakuu na matatizo yao ya kwenye kilimo yanafanana ndio maana hata hoja zao lazima zitafanana !

Bashe anachotakiwa ni kuona hali halisi ya chakula ilivyo Nchini kisha yeye na wataalamu wake waishauri Serikali inunue hayo mazao kwa bei ya soko lilivyo kisha Serikali iwauzie wananchi wake kwa bei nafuu !

Hivyo ndivyo Serikali zote duniani zinavyofanya ! Sio kuwalazimisha wakulima wauze kwa bei wasioitaka! Wakulima Nchi hii wamedharauliwa miaka mingi sana Sasa BaSI inatosha. !
 
Siyo kweli, acheni uwongo. Wakulima siyo wajinga kama nyinyi mnavyotaka waonekane wajinga. Hakuna mkulima ambaye hajui kuwa kuna Demand kubwa ya mazao!!

Ukiyafuata mahindi tu shambani anajuwa demand imepanda, anakuuzia juu
Wakulima wa leo si wale wa 1990.
Acha wabaki na ngonjera zao wakidhani wakulima ni maduwanzi.
 
Lima ya kwako ndo yapigwe marufuku mpuuzi wewe! Jitu hata mmea wa muhindi haliujui linaandika FYOKOFYOKO SHWAINI! Unadhani mkulima akihitaji Hela ataitoa wapi? Au uliposikia ada imefutwa kuanzia std one hadi 4m six ndo unaamini wazazi hawatoi chochote? Mdomo mrefuu kama chuchungi ooh wakulima wafungiwe kuuza mazao! Hebu iambie serikali isiwalipe posho na mshahara wabunge na watumishi mtawalia halafu uone majibu
 
Wakazi wa town tunatozwa tozo mbalimbali kibao ili wakulima wapewe mbolea za ruzuku halafu msosi wanawauzia wakenya na wazambia. Sijui tunatobolea wapi
  • Ungejua kuwa pembejeo za kilimo zinatozwa kodi, mazao yanaposafirishwa yanatozwa ushuru usingeandika hivyo.
  • Mapato Kwa mikoa inayotegemea kilimo yanatokana na kilimo, je biashara ya mazao ikidorora hayo mapato yatapatikanaje?
  • Acha kasumba mbaya ya kuona kuwa wakulima hawana mchango kwenye maendeleo ya nchi hii.
 
Siyo kweli, acheni uwongo. Wakulima siyo wajinga kama nyinyi mnavyotaka waonekane wajinga. Hakuna mkulima ambaye hajui kuwa kuna Demand kubwa ya mazao!!

Ukiyafuata mahindi tu shambani anajuwa demand imepanda, anakuuzia juu
Acha kutetea ujinga Mzee, ni makosa wakenya kuja kununu chakula mashamban kwetu, inaonekana nchi yetu imekosa mwelekeo, chakula kina nunuliwa kwenye minada Ili kuleta ushindani kwenye bei na sio kumfuta mkulima shamban, hapo lazima bei ishuke
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…