Mganguzi
JF-Expert Member
- Aug 3, 2022
- 1,604
- 3,715
Kijiji cha Ilembo kata ya Mpui wilayani Sumbawanga, nimekutana na kioja kama si kihoja! Ati ukijiandikisha inatakiwa wakapime mashamba yako, wakishayapima ndio upatiwe hiyo mbolea.
Nauliza kijiji kimoja kinawakulima mpaka 10,000' na Kila mkulima ana heka kumi, mtapima mashamba yote ndio mgawe mbolea?
Afisa mtendaji wa kijiji cha Ilembo kasema hawatapewa mbolea mpaka wakayapime hayo mashamba ya kila aliyejiandikisha. Jamani mko siriasi kweli na kilimo cha nchi hii?
Bashe unajua kuongea kwa mbwembwe ila usipokuwa makini hili la mbolea litakuangusha sana!
Msitucheleshe, kama hamna uhakika mseme!