Nimesoma unavyojitetea, inasikitisha! tatizo hujui maana ya agriculture ktk nchi. unataka nchi iendeshe agriculture kama familia? Kama kweli uko Canada, basi bado uko bize na show-up za mjini na waya masikioni. Ongeza ufahamu wa dunia badala ya kusema unaishi canada.
Hapo Canada ulipo uliza kama zao la chakula linalimwa na kuuzwa kibiashara. Mkulima hupewa bei ya ruzuku ili aendelee kulima. Kwenye soko (market) zao lolote kuu la chakula kwa nchi yoyote duniani haliwezi kuuzwa kwa mwananchi kibiashara. Usipoyajua hayo utaishia kutaja magunia ya mahindi na mpunga na bei na kutaka uuze nje, sijui wapi. Usichokijua pamoja na Bashe wako ni mambo ya food security na maana yake ktk nchi zote duniani.
Kisiasa ataweza kutumia pesa za serikali kuonesha kwamba kulima mahindi ni biashara, lakini atakwama tu hiyo huwa haikubaliki kokote. Ndo maana nchi haikupi nafasi ya kujiamulia wapi uuze. Bei ya ndani ikiwa kubwa, serikali itaagiza nje kuzuia ongezeko hilo.
Food security ensures that all people have access to safe, nutritious, and sufficient food to meet their dietary needs and preferences for an active and healthy life.
Kama haya hayajakuingia kichwani, endelea kulima mikoa yote na hutaisha kulalama.