Waziri Bashe tambua wewe ndiye Yusufu wa Biblia, tafadhali usimpotoshe mfalme

Waziri Bashe tambua wewe ndiye Yusufu wa Biblia, tafadhali usimpotoshe mfalme

gimmy's

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2011
Posts
3,312
Reaction score
3,345
Nakumbuka kisa cha yusuf.u wa bibilia kule misri ambapo mfalme aliota ndoto ile ambayo ilimshinda tafsiri,baada ya ndoto ile kujirudiarudia ndipo kukaonekana haja ya kumpata mtu atakae weza kuitafsiri.

Tafsiri ya yusuf.u ilibaini kwamba kutakuwa na miaka mitatu ya neema sana ambapo yusufu akatahadharisha kwamba wanapaswa kuhifadhi Chakula chakutosha.

Kadhalika yusuf.u akawatahadhirisha kwamba baada ya miaka mitatu ya neema yenye mavuno mengi,miaka mitatu inayofuatia itakua ni ukame na hakutakuwa na mavuno kabisa.

Hivyo yusuf.u akamwambia mfalme ya kwamba ahakikishe anahifadhi Chakula kitakachotosheleza mahitaji ya nchi kwa miaka sita jumla,yaani miaka mitatu ya neema+miaka mitatu ya ukame.Ndipo kwa hekima mfalme akamuachia Yusufu kazi yakuhifadhi Chakula kitakachoweza kuivusha nchi kipindi cha njaa.

Bashe wewe ndiye yusuf.u wa leo ambae mh raisi amekuamini lakini kwa bahati mbaya ni yusufu ulienyimwa maono.

Waziri TMA wanaendelea kutoa tahadhari juu ya mwenendo mbaya wa hali ya hewa lakini chaajabu bado umeendelea kushupaza shingo kwamba hatufungi mipaka nchi inaziada ya Chakula.

Kama mamlaka ya hali ya hewa wanatahadharisha msimu ujao kutakua na shida ya mvua,mwakani utakusanya wapi hio hifadhi ya taifa ya chakula?

Hii hifadhi ya Chakula hizi tani 150,000 unazojigamba nazo kwamba zinauwezo wakutosheleza nchi kwa miezi mitatu,hivi zinaweza fua dafu kwa nchi yenye watu 60 ml?

Waziri, tofautisha Mafuta ya kula na mahindi,mahindi ni Chakula watu wanateseka Sana kwa huu mfumuko wa bei kwa sasa.

Mafuta ya kula unaweza fanya hizi control zako ili ulinde wakulima na viwanda vya ndani kwani hili ni zao la biashara lakini kufanya haya kwenye mahindi ilihali TMA wanatahadharisha ukame kwenye msimu ujao,tambua unahatarisha usalama wa nchi.

Raisi muangalie huyu waziri usifuate kila anachoshauri ataligarimu taifa,kumbuka njaa haina mbadala.

Asante.
 
Eti yeye ndio Nabii Yussuf
Nyie ndio mlimuita aliepita Mungu
Njaa inakuja mjiandae tu
 
Hata yusufu alikuwa wa nchi nyingine lakini alifanya maajabu.
Laiti angefuatilia au kuwa na upana kiasi wa mambo ya ndani na nje angeelewa kuwa nchi inajengwa na kila asili.

Huko Latin America marais wengi walikuwa na asili ya Waarabu.

Leo Sunak ni PM ila ubaguzi mbaya lakini utakuta hata yeye babu yake aliingia kutoka Malawi au Zambia ila hatuna tabia ya kujisifia hivyo kama wenzetu wazungu ambao watakuambia mimi baba yangu ni Myahudi.
 
Ndio shida ya kupachika Raia wa nchi nyingine
Waingereza taifa kubwa kabisa wamemuweka muhindi ndio Waziri Mkuu wa Nchi kubwa kabisa Duniani iliyotawala karibu nusu ya Dunia.
 
Bashe Kesha sema hatazuia chakula kuuzwa nje ya nchi
Juzi rais wa Congo amewekeana mkataba kufungua soko la chakula cha Tz jijini Lubumbashi hii ni mbali na la Goma na Kivu . Sasa changanya na yanayo kwenda Kenya, Rwanda, Sudan
Yusufu wako ni feki
 
Back
Top Bottom