KERO Waziri Biteko, kwanini nguzo moja ya umeme ilipiwe Tsh 515,000/ wakati ni mali ya shirika? Huu unyanyasaji mpaka lini?

KERO Waziri Biteko, kwanini nguzo moja ya umeme ilipiwe Tsh 515,000/ wakati ni mali ya shirika? Huu unyanyasaji mpaka lini?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Ninachojua kijijini ni REA, hununui nguzo, ukilipia umepigwa, muone mkurugenzi.
Mkuu, Heshima kwako; leo huko vijijini watakwambia aidha awamu ya REA imepita ama nguzo za REA hazipo, zilizopo ni za TANESCO. Si unafahamu wale ni wataalamu?
 
Wewe unaishi Tz kweli?

Mimi niliwaambia wabadirishe nguzo na waweke pembeni na uwanj yaani mpakani maana ipo katikati ya kiwanja wakaniambia 430k Hadi Leo ipo naitafuta hiyo 430k ! Kwahiyo kubadirishiwa nguzo ni Hela vilevile
Hao sasa wezi kabisa, nguzo si wanatumia hiyohiyo?
 
Shirika linapewa bure hizo nguzo?? Na kama ungependa iwe mali yako kwakuwa unalipia je uko tayari kulipia nguzo mpya kila mara inapotakiwa kubadilishwa?? Vipi kuhusu mita ya umeme nayo si unalipia, uko tayari kulipia kila inapopata hitilafu??
Umesoma cost accounting?
 
Mkuu TANESCO ni zaidi ya TRA. Unamuuzia mteja nguzo, na wakija wateja mwengine zaidi ya 5 wanatumia /wana wasambazia umeme nguzo hiyohiyo uliyo nunua wewe bure, hii imekaa kaa je? Mtu amenunua nguzo yake ni mali yake mwachieni atumie atakavyo na sio kuifanyia biashara kwa wateja wengine.
Yaani hicho wanachofanya ni wizi mtupu!
 
Shirika linapewa bure hizo nguzo?? Na kama ungependa iwe mali yako kwakuwa unalipia je uko tayari kulipia nguzo mpya kila mara inapotakiwa kubadilishwa?? Vipi kuhusu mita ya umeme nayo si unalipia, uko tayari kulipia kila inapopata hitilafu??
Kwenye mkataba wa pango hela ya mteja ikitumika kuharakisha mchakato wa ujenzi au ukarabati utaratibu ni kupigiana mahesabu ya fidia kwanza.

Jifunze kutofautisha vitu! Mita ni package kwenye line ya kuvuta umeme. Kila mteja analipishwa!
Lakini malipo ya nguzo yamekaa kitapeli kwani si wateja wote wanalipishwa nguzo!
Pioneers au wale wanaokaa mbali wanalanguliwa sana!
 
Shirika linapewa bure hizo nguzo?? Na kama ungependa iwe mali yako kwakuwa unalipia je uko tayari kulipia nguzo mpya kila mara inapotakiwa kubadilishwa?? Vipi kuhusu mita ya umeme nayo si unalipia, uko tayari kulipia kila inapopata hitilafu??
Nguzo inabadirishwa Mara ngapi kwa mwaka?
 
Ni kweli, hata vodacom wanakuuzia huduma ya mawasiliano na bado simu unanunua mwenyewe. Vilevile gesi ya kupikia mtungi unaulipia au siyo?
Mtungi unakua mali yangu, simu inakua mali yangu. Point yako haina logic
 
Huu wizi upo Tanzania TU mali iwe ya tanesco halafu mteja analipia! Wizi mtupu
 
Ni Picha ya Nchi iliyokosa viongozi wenye kujua Namna ya kukusanya Kodi vzr wao wanafikiri kuweka bei kubwa ya nguzo ndio watapata Kodi kumbe wanajinyima wenyewe kwasababu watu wanatumia njia za Panya ili kupata izo nguzo lkn pia wahitaji wanawapunguza automatically.
Sasa iyo ya Tanesco Ni mfano mmoja tu angalia gharama za kuunganishiwa maji utakimbia,Huwa nawaza siku ningepata nafasi ya kuwa kiongozi haya mambo ya hovyo Ni kiyaondoa mara moja
 
Nililipishwa nguzo na hawa jamaa cha ajabu nimelipia tu na jirani nae akalipia yaan mimi nimepigwa laki 5 na usheee jirani akaungwa kwa laki tatu na ushee huna naumia sana sema hili swala waliangalie bwana haiwezekani mm nipambane nilete umeme wengine waje wapate kwa bei ya chini basi kama ni hivyo mm nilie pambana kuuleta mnipe ofa ya kutumia bure umeme hata miezi 6
 
Kuna site yangu flan waliweka nguzo mbele ya nyumba wakaisimamisha kabisa baada ya wiki kama mbili naskia wakaenda wakataka kuitoa majiran wakaleta noma ndo wakaacha
 
Back
Top Bottom