Waziri gani alimdhulumu Rais mstaafu Mwinyi vifaa vyake vya ujenzi?

Waziri gani alimdhulumu Rais mstaafu Mwinyi vifaa vyake vya ujenzi?

Ina wezekana mwinyi ndo rais aliye maliza madarakani bila kubwa na mikopo ya kutoka ulaya
 
Kutoka katika historia ya Hayati Mwinyi moja ya jambo kubwa la kiungwana ni kumteua Waziri ambaye alimfukuza katika nyumba ya serikali.

Je atakuwa ni nani huyo? Maana mzee mpaka anafariki hajapenda kumtaja Ila ni vizuri atajwe tu ili watu wajifunze.
Hii inaonesha kama Taifa tusivyo na kawaida ya kusoma vitabu. Hili suala limeelezwa kwenye kitabu chake Mzee Mwinyi.

Na ni uongo kusema kuwa, mzee hadi anakufa hakumtaja. So, ni vizuri tukawa na ratiba za kujisomea vitabu maana hutuongezea maarifa.

Huyo Waziri alikuwa Makweta, na alilazimika kumwachia hata vifaa vyake vya ujenzi alivyokuwa ameandaa kwa ajili ya ujenzi wa ile nyumba yake ya Mikocheni.

Ova
 
Glenn na withdraw comments zangu kuhusu nani hasa alimfukuza Mwinyi kwenye nyumba. Inaonekana ni kitu ambacho hamna mwenye uhakika nacho
Huu ni uungwana mkubwa mkuu.

Nami nimeona watu wanajaribu kuunganisha matukio na hakuna anayejua kwa hakika.

Asante sana Kinyungu
 
Hivi baba yake kaonekana Zanzibar.
Alafu amepotea sana , waziri na mwanae atoe majibu ,maana uyu mzee ana maneno ukikutana ne kwenye halmashauri ya ccm kama vile anatumia computer,

Wapi mzee makamba
 
Huu ni uungwana mkubwa mkuu.

Nami nimeona watu wanajaribu kuunganisha matukio na hakuna anayejua kwa hakika.

Asante sana inyungu
Nilimfukuza Bubu mimi mwenyewe ,hakuna kuondoa huu uzi ,vinginevyo Mh Mdeleka, Pita kibatala , Mwabukusi, mnataka kukutana nao tujue Panapo nyesha mvua
 
Piga picha Tusome. Mimi sijawah msikia Mwinyi akimtaja
Nimekwisha kutajia jina la kitabu, bado unabisha mpaka uone picha ya ukurasa. Siwezi kufanya hivyo kwa kuwa mwishowe utataka nikuwekee .pdf nzima ya kitabu hapa.

Naungana na usemi wa Anonymous aliyesema "“If you want to hide something from a Black person, put it in a book.”
 
Same body makweta
Kauli ile aliomwambia rudi kwenu Zanzibar huko sio kauli ya kiungwana. Inaonekana moyoni mwa viongozi wengi kutoka Upande wa pili muungano ndio zilivyo. Ukichanganya imani tena hapo mambo yanazidi kuwa mambo.
Mwinyi kaonyesha wazanzibsr walivyo. Mioyo yao ipo safi.
 
Kwa hisani kubwa kabisa ya Jamiiforums tarehe 23 Julai 2019
Bofya chanzo : Jinsi Natepe alivyomhenyesha Rais Ali Hassan Mwinyi

Alipojiuzulu uwaziri wa mambo ya ndani ya nchi mwaka 83? kama sijakosea nafasi yake aliteuliwa mzee mmoja kutoka Zanzibar anaitwa mzee Abdallah Said Natepe kushika uwaziri wa mambo ya ndani ya nchi.

Meja Jenerali Abdallah Said Natepe alipoingia tu ofisini alimtaka waziri aliemtangulia kutoka katika nyumba ya waziri ili yeye aweze kukaa hapo kama waziri.

Ilikuwa shida kidogo maana waziri aliyeondoka bado alikuwa anatafuta makazi lakini alitakiwa haraka kutoka na Meja Jenerali Natepe.

Ikampasa mzee Ali Hassan Mwinyi kutoka kwa haraka na siku anatoka pale nyumbani alikuwa amenunua mabati 150 na mifuko ya saruji 100 ya kwake wala sio mali ya serikali.

Mzee Abdallah Said Natepe alimkatalia kuvichukua akidai ni mali ya serekali kweli mzee Ali Hassan Mwinyi akaviacha akaondoka.

Baada ya miezi kadhaa tu mzee Ali Hassan Mwinyi akateuliwa kuwa Rais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar . Mzee Abdallah Natepe wakati anajifikiria jinsi ya kwenda kumpongeza na kumuomba radhi kwa aliyomfanyia kabla ya kufikiria njia mzee Ali Hassan Mwinyi akaletwa bara mwaka 1985 kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hapa sasa Mzee Meja jenerali Abdallah Natepe akajua kazi hana na atatimuliwa haraka iwezekanavyo tena na kutengwa na nyadhifa za serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwakuwa kuna mabaya ya wazi na ya sirini aliyomtendea mzee Ali Hassan Mwinyi.

Mzee Mwinyi baada tu ya kuapishwa kuwa Rais wa JMT wakati anateua baraza la mawaziri akamteua tena Abdallah Said Natepe kuwa waziri pale pale mambo ya ndani.

Siku ya kumuapisha akamwambia mzee Abdallah Natepe sio kwamba nakupenda sana hapana ila napenda kazi yako unavyofanya endelea kufanya kazi.

Siku moja mzee Mwinyi yupo ikulu kapumzika akaona malori yanaingia na akaambiwa mzigo wako huu Mh. Ali Hassan Mwinyi rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania akashtuka mbona sijaagiza kitu mie??

Ndipo akaambiwa umetoka kwa Natepe, mzee Ali Hassan Mwinyi akacheka sana akawaambia wasaidizi wake shusheni mabati 150 na saruji 100 hizo ndio haki yangu zingine mrudishieni tu.

N.B
Habari za ziada kwa hisani ya intaneti

Sunday, September 26, 2010​

MUASISI WA MAPINDUZI ZANZIBAR ABDALLA SAID NATEPE AMEFARIKI DUNIA​


Mmoja wa viongozi 14 wa Mapinduzi matukufu ya Zanzibar,Meja Jenerali Abdallah Said Natepe amefariki dunia jana mchana katika hospitali yajeshi Lugalo mjini Dar es Salaam.

Marehemu Natepe ni miongoni mwa viongozi wa mapinduzi kumbi na mbili waliofariki dunia ambao walifanikisha kufanikiwa kwa mapinduzi ya Januari 12, 1964 yaliyoindoa serikali ya kisultani visiwa vya Zanzibar,

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, kifo hicho kimetokea jana mchana kwenye hospitali hiyo kuu ya Jeshi la Wananchi.
Taarifa hiyo inamnukuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akieleza kushtushwa na kuhuzunishwa na kifo cha mwanamapinduzi huyo na kumtumia salamu za rambirambi katibu mkuu wa CCM akielezea jinsi alivyoguswa na kifo hicho cha Mzee Natepe.

“Kifo kimemchukua mwanamapinduzi, mzalendo na mwanachama wetu mwaminifu katika kipindi ambacho taifa na chama bado kinamhitaji sana. Kifo kimetunyang’anya tunu wakati huu tunaoelekea uchaguzi mkuu; ni huzuni kubwa kwetu; ni majonzi makubwa na hatuna neno kubwa linaloweza kuelezea huzuni hii,” Rais Kikwete anakaririwa kwenye taarifa hiyo.

Rais alipokea taarifa za kifo cha Mzee Natepe jana mchana akiwa Njombe mkoani Iringa ambako yuko kwa ajili ya shughuli za kampeni.

Rais Kikwete pia ametuma salaamu za rambirambi kwa familia, ndugu na jamaa wa Marehemu Natepe.

“Mzee Natepe amekuwa sehemu ya maisha yangu ya kisiasa, kijamii na amenipa malezi na maelekezo mengi nikiwa kama kijana wake na amekuwa moja ya nguzo yangu kubwa katika shughuli zangu za kisiasa na kikazi katika maeneo yote niliyotumikia nchi yangu,” alisema rais na kuelezea kwa masikitiko huzuni aliyonayo na kuwahakikishia kuwa yuko nao katika kipindi hiki kigumu.

“Tunamshukuru mwenyezi Mungu kwa kutupa nafasi ya kuishi na Mzee Natepe na kufanya naye kazi. Tunamuomba Mungu amlaze mzee wetu mahali pema peponi na kumpa pumziko la milele, amina”

Aisee
 
Katika Kitabu cha kuelezea maisha yake Mstaafu Mwinyi anasema alipojiuzulu Uwaziri wa Mambo ya Ndani Waziri aliyechukua nafasi yake alimtaka ahamishe haraka mizigo yake ili yeye ahamie kwenye nyumba ya Serikali aliyokuwa anakaa Mzee Mwinyi.

Mzee Mwinyi alishindwa kuhamisha vifaa vyake vya ujenzi wa nyumba yake ya Mikocheni kwa Mwalimu, yule Waziri akamdhulumu.

Pamoja na ubazazi na udhulmati wa Waziri huyo lakini Mzee Mwinyi alipochaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alimchukua Waziri huyo kwenye Baraza lake la Mawaziri.

Waziri huyo ni nani?

Pia, soma=> Jinsi Natepe alivyomhenyesha Rais Ali Hassan Mwinyi
Kumbe yule Mzee alikuwa na roho kama ya Mandela.
 
Yaani ana roho safi sana. Wajanja ndio walimleta mizengwe kwa kupenyeza ajenda zao wakati wa utawala wake. Mama Samia ajifunze kitu. Sio kila mtu anaaminika 100%
JK alisema akili za kuambiwa changanya na za kwako
Times change. May 21, 2021..and how it is today?
 
Huyo waziri alimkera sana mzee ruksa, mpaka akasimulia kwenye kitabu chake. Binadamu usimdharau mwenzako, hujui unaemdharau atakuwa nani baadae.
 
Maneno sio ya uungwana kabisa, husein mwinyi na mama samia ni wakati wao wa kuvunja huu muungano, otherwise watajutia pale watakapokua hawapo tena madarakani.

Nikifikiriaa ndugu zetu waislamu wameuawa Zanzibar wakati wa revolution naumia sana ndugu yangu Malaria, wamepata tabu sana, wameuawa kinyama si wazee si wamama, wengine inasemeka walikua wajawazito, na wengine walikua baharini wakijaribu kukimbia lakini wakawa wanatupwa baharini.

Mpaka sasa huwa najiuliza hawa viongozi kwanzia amani karume, mohamed shein, na sasa mwinyi wana moyo gani na kuendelea na huu muungano!

Allah awarehemu wote waliouawa dhidi ya makafiri hao, akiwemo na okello ambae walimtumia wakati huo.
Mkuu.
Maraisi wote ukimuondoa Abdull Wakil na Salmin wameishi Bara. Hatukuwabagua. Tena Salmin akapata Mke Bara
 
Back
Top Bottom