Waziri Gwajima tengua uamuzi wako wa kuunga mkono sheria ya maadili Arusha, hili ni bomu unatengeneza

Anataka iwe kama Zanzibar.

Lengo amfurahishe mteuzi wake
Simfurahishi mtu yoyote pasipo tija Bali natimiza wajibu wangu kuiongoza jamii kwenda mbele na maendeleo na ustawi pasipo kuathiri taratibu za kawaida za binadamu. Hii video hapa chini ndiyo msimamo wangu thabiti kwenye hii hoja, hayo mengine msimamo wako. Kila mmoja na msimamo wake, tusubiri matokeo ndugu. Jioni njema na Baraka.
Your browser is not able to display this video.


Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Ahsante Sana kwa mchango mzuri wenye tija ya hoja. Na mm hapa kama waziri mwenye dhamana ya jamii, siwezi kuwakatisha tamaa jamii hasa ambayo imeona kuwa imiliki ajenda ya mabadiliko. Hatua ngumu kuliko zote kwenye uongozi ni kuwafanya Wanadamu wawe sehemu ya ufumbuzi wa changamoto zao. Sasa Hawa wamefika wenyewe kwenye hatua hiyo, letu sisi kuwa guide, regulate, train... Ili wapanue mawazo wafike salama safari yao na kwa tija. Video ya mwelekeo wangu hii hapa[emoji116]
Your browser is not able to display this video.


Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Acheni kuwa mashabiki wa ujinga watu wa aina hii ndio mmekuwa vichocheo vya ushoga na mmonyoko wa maadili Kwa nyanja mbalimbali.
 
Hongera sana, lakini hata hivyo wapenda mabadiriko tupo na wewe binafsi napenda viongozi wanaosaidia jamii kukua kimaadili.
Nchi yetu inapitia kipindi kigumu vijana wengi wame iga tabia za hovyo mitandaoni, na kuzileta mtaani wanaishi maisha ya hovyo kiukweli inasikitisha simama katika ukweli na daima ukweli utashinda.
 
Kuja hapa na kushiriki huu mjadala tayar umeonyesha ww ni Kiongozi wa namna gani bila kujali utakachokiongea maana ulikuwa na uwezo wa kuipotezea hii mada na Kukaa zako kimya kama wafanyavyo viongozi wengine wa nchi, nakupongeza sana muheshimiwa tuko pamoja na wewe na kazi Yako inaonekana endelea na moyo huo huo na Mungu akutangulie katika majukumu Yako.

Uchaguzi ujao Chadema ikichukua nchi tunategemea uje kuwa wazir mkuu inshaallah!!
 
Mie naona wapo sahihi... na wanatakiwa waigwe.

Kuna vizazi vya watu wajinga wajinga sana wanakuja kutusumbua mitaani.
Juzi hapa kuna jamaa wa Arusha alikuwa analewa sana halafu anakuja kumuamsha mama yake usiku kwa matusi ili apewe chakula (mama yake ni mjane)....jamaa akaonywa mara ya 1, ya pili na ya tatu kwa muda wa wiki 3

Baada ya hapo jamii ya Waarusha wakambeba akiwa amelewa na kumpeleka porini... akachapwa viboko 70

Siku 3 nzima amelala ndani...na leo hagusi kabisa kilevi

Sasa hapo viboko havijasaidia?
 
Mama Hongera sana, upo vizuri na endelea na juhudi hizo
 
Waambie hao watandikaji.. waongeze tena 70 zingine ili wamrudishe kwenye Default settings kabisa. Hahah
 
Mimi nalia na wazazi wasio fundisha maadili watoto wao haya mambo hatutayaona kabisa. Lakini kuanza kukandamiza uhuru wa mtu binafsi ni ujinga tu.
 
Yale ni miongoni mwa maamuzi ya kipumbavu kabisa kuwahi kuyaona
 
WAZIRI NIKUTAKE RADHI WASWAHILI WANASEMA ASHUKUM SIO MATUSI ILA TANZANIA HAKUNA MAADILI KUANZIA KWA VIONGOZI MPAKA WATU BINAFSI NADHANI UMESHAELEWA NACHOMAANISHA.
MTU MZIMA AKIVULIWA NGUO UCHUTAMA UNAFIKI NI KITU KIBAYA SANA.UKWELI NI KWAMBA TANZANIA HAKUNA MAADILI KUANZIA KWA VIONGOZI WETU NA BABA ZETU NA MAMA ZETU NA VIONGOZI WETU WA KIIMANI
NA KAMA YUPO MTANZANIA AU KIONGOZI WA KITANZANIA MWENYE MAADILI YA KITANZANIA NITAJIE HATA MMOJA.
LABDA TUANZE NA WEWE DADANGU UNAYO MAADILI YA KUJIVUNIA MBELE YA JAMII YAKO NA WATANZANIA KWA UJUMLA?????
 
Hakuna cha msingi ulichomjibu mtoa mada, ameongelea uhalisia na namna ya kukabiliana na hizo changamoto. Kilichofanywa na hao viongozi wa kijiji husika hakipaswi kuungwa mkono kamwe, na ni uvunjifu mkubwa wa haki za raia. Wajaribu kutatua chanzo na wewe hukupaswa kuliunga hilo mkono.
Hicho kijiji si kisiwa ni kama ambavyo nchi yetu si kisiwa, nikitoka mjini ambako hakuna hiyo sheria na kwenda huko kuwa salimia wazee na nimevaa suruali ya jinzi iliyotobolewa magotini nitachukuliwa kama muhalifu na kutozwa faini. Nchi ya ajabu sana hii.
Kuweni serious na masuala ya msingi kwa maendeleo ya nchi hii na si bla bla kila siku
 
Ukitaka kulipima jambo lolote kama ni baya au zuri lipime Kwa watu unao wapenda mfano unajisikiaje baba Yako au mama Yako wakinyoa viduku? Vipi mama yako au dada Yako akitembea uchi?
Lina koneksheni gani na uhalifu au mmomonyoko wa maadili. Hadi Karne iliyopita tulikuwa tukicheza ngoma za asili huku wadada chuchu zikiwa nje.
 
Ukiwa kiongozi unatakiwa ku regulate mambo ya jamii yaende mahala sahihi, siyo kuzimisha hatua za jamii kwamba wewe na mimo ndiyo tunajua zaidi. Sasa mm msimamo wangu ni ku regulate, kuwezesha jambo lenye Nia njema liende kwenye mstari sahihi. Sawa, kama kwenye maneno yangu hapa kwenye video. Naanza na wewe kukuelimisha kwanza maana na ww ni sehemu ya jamii vilevile.
Your browser is not able to display this video.


Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Hongera Sana ww mtakatifu mwenye Nuru [emoji847][emoji847][emoji847]inuka sasa uangaze Nuru yako ikawe dawa kwenye janga hili la mmomonyoko wa maadili.... sisi tunasubiri Nuru yako ituangazie....

Uzuri hata Sauli kabla hajawa Mtume Paulo alitoka kwenye dhambi nyingi, akaja akageuka kuwasafisha wengine. Inuka tu uangaze sisi tuna shida na Nuru.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
TATIZO MH UNALETA SIASA KWENYE MAISHA HALISI YA VIJANA WA KITANZANIA AMBAO TUNA UPEO WA KUELEWA MAMBO KIUELEDI.
VIONGOZI WETU HAWANA MAADILI NA NDIO VIOO VYA JAMII WANAOIGWA NA VIJANA .NA VIJANA WANAIGA YANAYOFANYWA NA VIONGOZI WETU AMBAO WANAOONGOZA KWA MMOMONYOKO WA MAADILI TENA WAZIWAZI BILA VIFICHO.
WA KULAUMIWA NI VIONGOZI WETU TULIOWAPA DHAMANA YA KUTUONGOZA WAMEKOSA MAADILI NA UKIWAKOSOA BASI WEWE NI JEURI NA HUNA NIDHAMU NA MHAINI UNASITAHILI KIFUNGO NA ADHABU KALI.
WATANZANIA WANAOGOPA KUSEMA NDIO MAANA WAPO KIMYA.
 
Hata mm sijakudharau kabisa, tena wala sijakubeza. Ila nimekuongoza tu kwenye mstari wa hekima kuwa, ukipewa neema ya kuwa mwana wa Nuru, usianze kuhoji kwa nn huyu ni mwana wa Giza ila amestahili hili. Wewe inuka uangaze ufanye jambo la kuleta nafuu kwenye jamii, utaonekana na utainuliwa na Mungu utatumika kwa ajili ya jamii. Sasa na wewe tatizo lako ukielezwa lugha za hekima unaona umepuuzwa unaletewa siasa. Njoo Sasa huku tuna mitandao mingi ya Mashujaa wa kijamii uje tushirikiane, na karama yako ionekane. Vinginevyo kukaa humu na kushutumu na uko mbali uwanja wa vita mm naona na ww huna msaada na hatutoki tulipokwama.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…