Waziri Innocent Bashungwa awakabidhi Wakuu wa Majeshi Wastaafu Land Cruiser LC300 mpya

kwani wastaafu wako wawili tu?
 
Wakuu wa wabrashi viatu wao haiwahusu? au ndo waliamua kujichangachanga wenyewe walau wakatoa ile Prado...
CDF ( Chief of Defence forces) ni Mkuu wa Majeshi ya ulinzi na usalama ( ikiwemo jeshi la Polisi)


wengi wanadhani akitajwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na usalama maana yake ni Mkuu wa Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) huyu ni Bosi wa Majeshi yote na ndio sababu wakuu wote wa Jeshi la Polisi, Magereza, Uhamiaji ni wasaidizi wake

jeshi la Polisi ni sehemu ya Defence forces

hivyo IGP kupewa gari sawa na Bosi wake si sawa
 
Kutaja miaka ni kosa, hapa una refer to kifungu gani? Kindly share hicho kifungu, au kushare hicho kifungu cha sheria nayo ni kosa?
kuweka hadharani circular za Serikali ni kosa kwa mujibu wa sheria

umesahau Mwananchi iliwahi kufungiwa kwa kuweka hadharani stahiki za mawaziri kwa mujibu wa sheria?

sikumbuki vifungu rasmi kwa kuwa si Mwanasheria na sijawahi kuvikariri
 

Hakuna mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama mkuu.

Kuna mkuu wa majeshi ya ulinzi tu.yaani ,ardhi,anga na maji.
Kiitifaki Yeye ni superior kwa wakuu wa vyombo vya mrengo huo yaani anakuwa senior kwa IGP,DGTISS,CGP,CGF,DGPCCB nk.
 
Kwa kweli sisemi neno zaidi ya kusisitiza UZALENDO kwa Taifa maskini la Tanzania.

Wanajeshi tunapaswa kuwajali sana yes. Wana uzalendo wa kweli. Lakini tunapaswa pia kukumbuka kuwa nchi ipo kwenye mkongojo wa kouchumi.


Enewei nisiandike sana, mdomo koma!
 
Nimeona hata Bajeti ya Wizara ya ulinzi nimkubwa sana ,Til.3 za wazi Je ambazo hazitajwi ni kiasi gani?

Hii nayo sio sawa sana Kwa Nchi Maskini kama Tanzania
 
Akikabidhi Magari hayo, Waziri Bashungwa amesema kuwapatia Wastaafu hao magari ni sehemu ya maelekezo ya Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwamba wapatiwe magari mapya ambayo yanatengenezeka na spea zake zinapatikana kwa urahisi.
Bei ya spea za haya magari kwa wastaafu itakuwa rafiki kweli?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…