Waziri Innocent Bashungwa awakabidhi Wakuu wa Majeshi Wastaafu Land Cruiser LC300 mpya

Waziri Innocent Bashungwa awakabidhi Wakuu wa Majeshi Wastaafu Land Cruiser LC300 mpya

CDF ( Chief of Defence forces) ni Mkuu wa Majeshi ya ulinzi na usalama ( ikiwemo jeshi la Polisi) wengi wanadhani akitajwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na usalama maana yake ni Mkuu wa Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) huyu ni Bosi wa Majeshi yote na ndio sababu wakuu wote wa Jeshi la Polisi, Magereza, Uhamiaji ni wasaidizi wake jeshi la Polisi ni sehemu ya Defence forces hivyo IGP kupewa gari sawa na Bosi wake si sawa
 
Kweli mwenye nacho huongezewa...kama ni kununua Ambulances zingepatikana ngapi?..na zingeokoa maisha ya wangapi?...najua mtasingizia sheria..haya bwana ILA yana mwisho haya
 

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Innocent Bashungwa @innocentbash amewakabidhi magari mapya Wakuu wa Majeshi Wastaafu kwa maelekezo ya Rais na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Wakuu wa Majeshi Wastaafu waliokabidhiwa magari ni CDF Mstaafu George Waitara na Robert Mboma na makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi za Wizara ya Ulinzi Mtumba Jijini Dodoma

Akikabidhi Magari hayo, Waziri Bashungwa amesema kuwapatia Wastaafu hao magari ni sehemu ya maelekezo ya Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwamba wapatiwe magari mapya ambayo yanatengenezeka na spea zake zinapatikana kwa urahisi.

“Wakuu hawa wa Majeshi Wastaafu walifanya kazi kubwa na iliyotukuka kipindi cha utumishi wao kwa Nchi yetu, Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. Samia Suluhu Hassan imewapatia magari na kuwatakia kheri na maisha marefu Majenerali Wastaafu hawa”

AYO TV
David msuguri yeye hajapewa gari kama wenzake?au yeye lake hawajalipia
 
CDF ( Chief of Defence forces) ni Mkuu wa Majeshi ya ulinzi na usalama ( ikiwemo jeshi la Polisi)


wengi wanadhani akitajwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na usalama maana yake ni Mkuu wa Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) huyu ni Bosi wa Majeshi yote na ndio sababu wakuu wote wa Jeshi la Polisi, Magereza, Uhamiaji ni wasaidizi wake

jeshi la Polisi ni sehemu ya Defence forces

hivyo IGP kupewa gari sawa na Bosi wake si sawa
Acha uongo.
 
Back
Top Bottom