Waziri Innocent Bashungwa awakabidhi Wakuu wa Majeshi Wastaafu Land Cruiser LC300 mpya

Waziri Innocent Bashungwa awakabidhi Wakuu wa Majeshi Wastaafu Land Cruiser LC300 mpya

CDF ( Chief of Defence forces) ni Mkuu wa Majeshi ya ulinzi na usalama ( ikiwemo jeshi la Polisi)


wengi wanadhani akitajwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na usalama maana yake ni Mkuu wa Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) huyu ni Bosi wa Majeshi yote na ndio sababu wakuu wote wa Jeshi la Polisi, Magereza, Uhamiaji ni wasaidizi wake

jeshi la Polisi ni sehemu ya Defence forces

hivyo IGP kupewa gari sawa na Bosi wake si sawa
Nini maana ya Defence?
Hiki cheo Cha Usalama mnakitoa wapi?
 
Linamtosha
Hakuna asiyependa kuvimba kwenye lile li V6 twin turbo la kisasa.
21110314841DSC_1472.jpg
 
Sema sijui kwanini wabongo mnakomaa kwamba CDF ni mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama, CDF ni mkuu wa majeshi ya ulinzi tu wakimaanisha zile kamandi za JWTZ (Airforce, Navy, Land, JKT, MMJ) lakini majeshi ya usalama (Polisi, Uhamiaji, Magereza na Zimamoto) yana wakuu wao na hakuna anayewajibika kwa mwingine, ndio maana hivyo vyombo viko chini ya wizara mbili tofauti ila kiitifaki ni kwamba tu ukiwaweka pamoja CDF ndio mkubwa sababu JWTZ ndio jeshi senior
Ahsantee kwa ufafanuzii.
 
Hapa hatupo kijiweni ambapo kila mjumbe anachangia alijualo, mambo mengine yapo kimiongozo hayahitaji akili za kujiongeza CDF ni mkuu wa JWTZ jeshi moja lenye kamandi zake ambazo ni majeshi yanajitegemea. Mkuu wa wote ni CIC...wanakua na chombo chao ambacho mara nyingi sio zote CDF anakuwa mwenyekiti tena mwenyekiti sio kwa mamlaka bali kwa uratibu, msingi wa vikosi na majeshi mengine ni JWZT...chombo chao hiki kipo chini ya kuu taifa ambacho CIC ndo manyota wake
CIC ni nani? Hebu tueleweshee na ututajie jina la huyo CIC
 
Vijana tuendelee kusubiri taifa la kesho!
Mara uzee huo..., bila hodi unaibukia taifa la tasaf!
Tuendelee kusoma namba
 
Hata nyumba zao watakabidhiwa au wameshakabidhiwa, Zipo nyedengwa investment area, majirani zao ni akina mama yetu wa Chato, jesika na wengineo. ☺️

Tujitahidi tuwe wakubwa na tuendelee kulipa kodi, sisi ni “wanzalendo”.
 

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Innocent Bashungwa @innocentbash amewakabidhi magari mapya Wakuu wa Majeshi Wastaafu kwa maelekezo ya Rais na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Wakuu wa Majeshi Wastaafu waliokabidhiwa magari ni CDF Mstaafu George Waitara na Robert Mboma na makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi za Wizara ya Ulinzi Mtumba Jijini Dodoma

Akikabidhi Magari hayo, Waziri Bashungwa amesema kuwapatia Wastaafu hao magari ni sehemu ya maelekezo ya Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwamba wapatiwe magari mapya ambayo yanatengenezeka na spea zake zinapatikana kwa urahisi.

“Wakuu hawa wa Majeshi Wastaafu walifanya kazi kubwa na iliyotukuka kipindi cha utumishi wao kwa Nchi yetu, Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. Samia Suluhu Hassan imewapatia magari na kuwatakia kheri na maisha marefu Majenerali Wastaafu hawa”

AYO TV
Huyo wa pili kushoto ni kama alipata wito akiwa bar kisha kwa haraka na bila kwenda home kwanza akawahi Ikulu kupokea chuma.
 
Sirro sio CDF Mstaafu..

Sheria inasema apewe,sasa sijajua wameikarabati pesa ya ununuzi wakachukua kaprado ama vipi maana hiyo kampuni ina matapeli waliokubuhu[emoji28][emoji28][emoji28]
 
Back
Top Bottom