Waziri Innocent Bashungwa awakabidhi Wakuu wa Majeshi Wastaafu Land Cruiser LC300 mpya

Waziri Innocent Bashungwa awakabidhi Wakuu wa Majeshi Wastaafu Land Cruiser LC300 mpya

mbona huyu wa juzi kazi mwamunyange yeye hajakabidhiwa? ama yeye utaratibu wake uko tofauti? ila kwa nchi masikini kama bomgo kuendelea kukumbatia haya mashangingi ambayo ulaya yanamilikiwa na matajiri wakubwa tu ni kuendelea kuwa masikini tena masikini hohehahe.
Njia rahisi kabisa ya kuiba mali ya uma ni kupitia manunuzi !!
Hayo madude ni latest na ghali na ikitokea tukaambiwa bei yake humu wote tutanuna.
 
CDF ( Chief of Defence forces) ni Mkuu wa Majeshi ya ulinzi na usalama ( ikiwemo jeshi la Polisi)


wengi wanadhani akitajwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na usalama maana yake ni Mkuu wa Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) huyu ni Bosi wa Majeshi yote na ndio sababu wakuu wote wa Jeshi la Polisi, Magereza, Uhamiaji ni wasaidizi wake

jeshi la Polisi ni sehemu ya Defence forces

hivyo IGP kupewa gari sawa na Bosi wake si sawa
Sema sijui kwanini wabongo mnakomaa kwamba CDF ni mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama, CDF ni mkuu wa majeshi ya ulinzi tu wakimaanisha zile kamandi za JWTZ (Airforce, Navy, Land, JKT, MMJ) lakini majeshi ya usalama (Polisi, Uhamiaji, Magereza na Zimamoto) yana wakuu wao na hakuna anayewajibika kwa mwingine, ndio maana hivyo vyombo viko chini ya wizara mbili tofauti ila kiitifaki ni kwamba tu ukiwaweka pamoja CDF ndio mkubwa sababu JWTZ ndio jeshi senior
 
Hii ni kawaida sana mbona, nashangaa tu leo limefanywa kisiasa, hili tukio hifanyika miaka yote tena kimya kimya, wanabadilishiwa magari kila baada ya muda fulani, yanajazwa wese na familia zao zinatunzwa safi kabisa, jeshini kustaafu ukiwa na cheo kuanzia bridigia jenerali, meja jenerali, luteni jenerali na jenerali mwenyewe ujue ume ula uzee wako wote, yaani wewe ni reserve
Ni kuanzia Cheo cha Kanali
 

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Innocent Bashungwa @innocentbash amewakabidhi magari mapya Wakuu wa Majeshi Wastaafu kwa maelekezo ya Rais na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Wakuu wa Majeshi Wastaafu waliokabidhiwa magari ni CDF Mstaafu George Waitara na Robert Mboma na makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi za Wizara ya Ulinzi Mtumba Jijini Dodoma

Akikabidhi Magari hayo, Waziri Bashungwa amesema kuwapatia Wastaafu hao magari ni sehemu ya maelekezo ya Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwamba wapatiwe magari mapya ambayo yanatengenezeka na spea zake zinapatikana kwa urahisi.

“Wakuu hawa wa Majeshi Wastaafu walifanya kazi kubwa na iliyotukuka kipindi cha utumishi wao kwa Nchi yetu, Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. Samia Suluhu Hassan imewapatia magari na kuwatakia kheri na maisha marefu Majenerali Wastaafu hawa”

AYO TV
Majenerali wanakula mema ya nchi bwana dah 🤣 hapo service juu ya serikali, mafuta juu ya serikali na ulinzi wa kutosha 😀
 
Hapana gari ni mali yao na ukomo wa kupewa gari huisha pale muhusika anapofariki na ndio maana ina umiliki binafsi, wanufaika wa magari hayo kwa mujibu wa sheria ni jaji mkuu, spika wastaafu, mawaziri wakuu wastaafu, wakurugenzi wa tiss, na kadhalika
Sasa kwa mfano lile alilopewa kabla ya jipya anarudisha baada ya kupewa jipya au linaendelea kuwa lake.
 
Service force, falsafa ya jeshi na polisi ni jeshi ni mbwa anaehakikisha ulinzi nje ya nyumba usiku kucha na adui asiingie ndani na polisi ni paka anaelinda ndani ya nyumba hivo kimsingi mbwa humlinda pia paka hivo jeshi huwalinda pia polisi
Hapa hatupo kijiweni ambapo kila mjumbe anachangia alijualo, mambo mengine yapo kimiongozo hayahitaji akili za kujiongeza CDF ni mkuu wa JWTZ jeshi moja lenye kamandi zake ambazo ni majeshi yanajitegemea. Mkuu wa wote ni CIC...wanakua na chombo chao ambacho mara nyingi sio zote CDF anakuwa mwenyekiti tena mwenyekiti sio kwa mamlaka bali kwa uratibu, msingi wa vikosi na majeshi mengine ni JWZT...chombo chao hiki kipo chini ya kuu taifa ambacho CIC ndo manyota wake
 
Stupid baboon, police ni DEFENSIVE FORCE?
kama hadi kwa umri huo hujajua kuwa defence na security ni components muhimu sana kwny Majeshi na ni inseparable mie nitakusaidia vipi ?

tofauti ndogo na pekee ni kwny law enforcement function kwny jeshi la Polisi kipengele ambacho kinawapa majukumu zaid kisheria kwny kusimamia utii wa sheria
 
Back
Top Bottom