maroon7
JF-Expert Member
- Nov 3, 2010
- 11,345
- 15,851
Leo nimeona Waziri wetu mpendwa Mhe. Jaffo katoa wito kwa vyuo kuangalia utaratibu wa kufadhili wanafunzi wanaofanya vizuri masomo ya sekondari ili kuendelea na masomo ya elimu ya juu.
Ni wazo zuri sana na ikiwezekana iwe lazima kila chuo kila mwaka kitoe ufadhili. Ila pamoja na hayo bado serikali haijaviwezesha vyuo kuwa hata na uwezo wa kujiendesha vyenyewe hata kulipa gharama za msingi.
Mfano mzuri ni chuo cha DIT ambacho ni chuo cha Serikali huwezi kuamini hiki chuo hakina uwezo hata wa kulipa walimu wake wa part time.
Chuo kinauhaba mkubwa wa walimu hivyo kulazimika kwa kiasi kikubwa kuchukua walimu wa part time ambao ndio wanafanya kazi kubwa lakini ajabu yake wanahenyeshwa vibaya mno kwenye malipo.
Kwanza wanalipwa kiduchu kuliko vyuo vyote, na pili hawalipwi kwa utaratibu unaoeleweka maana hata mwaka mzima huwa unakatika wanahenyeshwa tu.
Hata leo ninapoandika walimu hao wanadai malipo yao ya semester iliyopita ambapo hawajalipwa hata mia kila siku ni kalenda tu. Hii inapelekea kuathiri sana elimu ya chuo ambayo ndio ufunguo halisi wa maisha.
Sasa katika hali kama hii Mheshimiwa Jaffo utasema vyuo vifadhili wanafunzi kama hata salary ya mwezi mmoja DIT wanashindwa kulipa?
Nadhani muangalie namna nzuri ya kuviwezesha vyuo kwanza kujitegemea ili viwe bora kirasilimali mkianzia na DIT ambacho kipo katikati ya jiji ila kinawatia doa, na hapo hata haya ya kufadhili wanafunzi yatawezekana.