Waziri Jaffo kama DIT wanashindwa kulipa walimu wataweza ufadhili wa wanafunzi?


Unajaribu kupotosha kwa maksudi sijui kwa maslahi ya nani, hata sasa wapo wanafunzi wanasoma kwa udhamini wa bure... mfano ni madaktari na non refundable grants!

Acha hao, hata shule zenye ushindani kielimu mfano FEZA Schools husomesha β€˜bure’ watoto wenye kukidhi sifa fulani... sifa hizo ni pamoja na ufaulu mzuri.

Njoo kwenye zile "scholarships", baadhi hulipiwa kila kitu... acha wivu mkuu.
 
Ukipewa kazi si unapewa mshahara wa kununua mahitaji yako, iweje upewe mshara upewe tena vitu bure, huo mshahara wakazi gani.
Ni bora hao watoto wapewe bure waziri anamshahara lakini anapewa bure sasa mtoto mmoja asipewe bure si uonevu kwa watoto.Hats wazungu hutoa scholarship kwa watu wachache, huu ni mfumo tulioukuta mkuu.
 
Sio lazima uwe na pointi, ungebwabwaja tu kama hivi... kwahiyo kutumia mfano wa chuo kimoja kwenye jambo la kitaifa ndo umeaona pointi?
Wewe ndio huna uelewa mi nimeanzisha mada kwa muktadha wangu, nawewe unaruhusiwa kuanzisha mada kwa muktadha wako ukaongelea vyuo vyote kama unavyotaka
 
Halafu miaka yote hii bunge limeshindwaje kutoa scholarship? Nao wangekua wanakatwa hata bukubuku kwenye posho zao za kila siku wasaidie kama kweli nia wanayo sio kuwapa mizigo wengine ambao hata posho za walimu wanashindwa kulipa afu uwaambie wachukue mzigo mwingine kutoa udhamini kwa wanafunzi
 
Katika zama hizi haiwezekani kumpata Kiongozi yoyote wa kutoa ufafanuzi
 
Katika zama hizi haiwezekani kumpata Kiongozi yoyote wa kutoa ufafanuzi
Tena kipindi cha uchaguzi ndio wanajua serikali ipo likizo wanafanya watakavyo
 
Unajua mwanasiasa anaposimama kwenye hadhira, ni lazima atoe neno. Liwe na uhalisia au la yeye hajali, na ninamaanisha, hajali!
Wanasiasa sio wa kuwaamini
 
βœ“Sio raisi, MTU kutoka DIT akaja akazungumza vitu, kama ivyo mbele ya utawala huu, maana anavumilia iyo anayopata asije akapoteza kabisa ukizingatia njee ya ajira hawezi kabisa kutusua Ndio maana hata sectors nyingi zilizipigwa pini zinashindwa kuongea
 
Exactly mkuu hizi ndio zama za kunyanyasika mtu unafanyiwa lolote na bado unakosa la kufanya. Na mbaya zaidi ni taasisi zinaongozwa na wasomi wanajiita maprofesa sasa sipati picha kwenye kampuni ya mtu binafsi tena asie na shule mambo ikoje
 
DIT nimiongoni mwa vyuo vyote kama jafo ametaka implementation ifanyike kwa vyuo vyote na DIT inachangomoto hizo huoni dhana ya vyuo vyote itapotea
 
Sasa tutajuaje kama hizo lawama zina ukweli wowote ndani yake kama tukikaa kusikiliza upande mmoja pekee?
 
Na chakushangaza mda ukifika hawahawa DIT watapeleka gawio la mabilioni ya pesaπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ .....hii ndo tz.
 
Na chakushangaza mda ukifika hawahawa DIT watapeleka gawio la mabilioni ya pesaπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ .....hii ndo tz.
Hahahahaaa kabisa mkuu hapo ndio utashangaa hii dunia ilivyo na mambo ya ajabu
 
Sasa tutajuaje kama hizo lawama zina ukweli wowote ndani yake kama tukikaa kusikiliza upande mmoja pekee?
βœ“[emoji769]Tuanzie na wewe, mbona umehificha na ID fake utaki kuweka jina lako wazi, kuogopa kufatiliwa. Na wao wenyewe ni ivyo ivyo Mkuuu. Wewe unafikiri MTU mwenye watoto 5 na kimada juuu ana watoto 3 anaweza akathubutu kusema mapungufu afukuzwe kazi. Unataka family yake ya watoto 5 na kimada wake mwenye watoto 3 utamsiadia kulisha family. Kwa wasiokuwa na majukumu ndio anaweza akathubutu kusema mapungufu lakini kwa mwenye majukumu hawezi kuthubutu hata kama kazini anapigwa makofi. Wangapi wanafanya kazi kwa wachina na wahindi wanapigwa mpaka vibao wanakausha hawasemi. Ongea yako inaonyesha bado ni mvulana ujajua majukumu yalivyo. Watu wamebadilishiwa gia angani ndio maana hawana cha kufanya, sema ni changamoto sana kwa kizazi kinachokuja kinatakiwa kiishi kwa akili na kisiishi kwa utegemezi mwingi wa ajira. Uwe na nje ya ajira uweze kufanya Mambo mengi. Wenzetu wahindi wanaishi maisha mazuri maana hawaishi Kwa utegemezi mwingi wa serikali na ajira zake
 
Sasa tutajuaje kama hizo lawama zina ukweli wowote ndani yake kama tukikaa kusikiliza upande mmoja pekee?
Hawana ubavu wa kusema chochote wanafaham ni wazinguaji na ndio maana nna wasiwasi ikitokea wametoa ufadhili kama alivyoshauri waziri Jaffo basi ujue wanaenda kuua watoto wa watu na njaa
 
Na we ni mmoja wao? Maana umeandika ukiwa unayajua kwa undani sana
 
Na chakushangaza mda ukifika hawahawa DIT watapeleka gawio la mabilioni ya pesaπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ .....hii ndo tz.
Hahahaha! Ndugu hilo gawio ( 10% ya walichokusanya kwa mwaka) ipo kwa mujibu sa Sheria hivyo itabidi wapeleke tu.
 
Hahahaha! Ndugu hilo gawio ( 10% ya walichokusanya kwa mwaka) ipo kwa mujibu sa Sheria hivyo itabidi wapeleke tu.
Hapo ndo ushangae kwenye gawiwo hela itapatikana ila kwenye mambo ya msingi kama mishahara hamna hela na wanategemea watoto wapate elimu bora
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…