Waziri Jafo aagiza Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Tarime kusimamishwa kazi kwa kusafirisha mwili wa mtumishi juu ya carrier ya gari

Mbona nasikia miaka yote maiti husafirishwa kwa namna hiyo, hasa watumishi wakisafirishwa na serikali. Nafikiri ni kuweka nafasi ndani ya watu kukaa. Mi sioni ubaya wowote.
 
Huu utaratibu upo siku nyingi na hauna tatizo lolote. Hata kwenye ndege maiti hukaa sehemu ya mizigo.
Sawa...lkn syo kuweka maiti juu ya gari
Bora wangemtia kwenye kirikuu

Ova
 
Nafikiri umeshapita sehemu ukahisi harufu ya mzoga wa mnyama fulani aliyekufa hapo na hakuna aliyeshughulika na mzoga ule. Kama wanadamu baada ya kifo tungefanyiwa vile, basi mitaani ingekuwa ni harufu ya mizoga yetu.

Kama binadamu na si wanyama, tuna akili timamu, na heshima kati yetu, tukiwa hai na mfu, si tu katika kuhifadhi maiti na si mzoga kama unavyoita, bali hata jinsi ya kusafirisha.
 
Duuu! Sijawahi kuona kitu kama hii! Hata kama ni visa, lakini imagine it were you!
Hapo msiba unasubiriwa kwenu, halafu mwili unaingia namna hiyo, na hiki ni kipindi cha mvua.

Ni dharau ya hali ya juu sana.
Si utu kwa kweli!
 
Ukishakufa hauna thamani tena ndiyo maana hata kwenye ndege unatupiwa sehemu ya mizigo huenda mkurugenzi aliapply namna hiyo akaamua awekwe kwenye carrier maana ni mzigo huo
Wa Tz tumejua ndege imekuwa nongwa! Ni maiti za WaTz wangapi zinasafirishwa na ndege? Basi huyu marehemu angepelekewa bombardia!
 
Mimi ningemuweka ndani Kisha kumfungulia kesi ya kukiuka kanuni ya Q7 na uhujumu uchumi kwa kutumia gari vibaya
Kama wewe ni mtumishi wa umma basi kunakitu umesahau.
Hapa hata aliyemkaimisha ana shida, alimkaimisha mtu asiyejua taratibu.Foremost, alipashwa ashirikishe LGA ya mahali palipotokea ajali, secondly, atakuwa aliunda kamati au alifanya kikao cha menejiment na kupanga sequency of events. Kama hawakumshauri vizuri, basi kuna shida kwenye halmashauri hiyo. Hii ndo tabu ya kukaimisha wasiojua taratibu
 
Nimebofya "Like"; Kaimu Mkurugenzi ni mtu mdogo mno kwa waziri, kama ni miongozo, aliyetakiwa kusimamia zoezi ni RAS Singida akishirikiana na RAS mara----- hawa ndo size ya waziri, hawa ndio naopaswa kuwatolea maagizo
 
Duuuu! Kaimu mkurugenzi katisha, nataka kujua hakuna watu waliomshauri kuwa kufanya hivyo sio uungwana
Huenda alikuwa ofisini akiendelea na kazi, kama kuandaa malipo ya mazishi ya marehemu. Yaani hapo ni ujuha kumsimamisha kazi huyo kaimu mkurugenzi kwa tendo alilofanya mtumishi mwingine (labda dereva), na unakuta gari hilo lilikuwa na abiria zaidi ya 8..
Kama dereva hakutumia busara, waziri amefuata mkumbo huohuo
 
kiutumishi ofisi inatakiwa imgaramie marehemu kila kitu yani ofisi ya mkurugenzi imekosa milioni 3 ya kukodi costa
 
Jafo sio mnafiki...ni kijana aliyenyooka. Hata katika matamshi yake huwezi kumsikia anamtajataja Magufuli wa Chato
 
Duuh hii.kwel.hapana ,kama raia tu mtaan huwaga wanajichanga na kukodi coaster ya kusafairisha maiti ,sembuse na serikal?huu sio uungwana .ilaaa tuishi vizur jmn maiaha yetu si marefu hapa dunian
Hapa ndio uone tofauti ya watu wa kitaa (mchanganyiko wa wasomi na wasio wasomi) na hao wasomi wa Halmashauri. Aliyefariki alikuwa mkuu wa Idara, Halmashauri ina wakuu wa Idara zaidi ya 13, walishindwa kujiongeza kuchanga hata elfu 50 kila mmoja ili rafiki yao (mkuu wa idara mwenzao) akodiwe hata Noah kama utetezi ni kuwa Halmashauri haina magari wala fedha. Watu wa mtaani wanawaza kibusara kuliko hao jamaa wa Tarime.

Ila pia ni somo kwa wengine kutambua jinsi marafiki wa kazini watavyowachukulia siku watakapolala mauti.
 
Aliyemkaimisha ukurugenzi nafikiri ni Mkurugenzi mwenyewe aliyepata ajali (internal), alimkaimisha kabla hajaondoka hapo Tarime.

Anayekaimishwa ofisi ya mkurugenzi ni lazima atoke katika Wakuu wa Idara za Halmashauri au nje ya Halmashauri kwa watumishi wenye sifa sawa na mkuu wa idara. Huyu ni lazima anajua taratibu za kitumishi sababu ili uwe mkuu wa idara pamoja na suala la elimu, ni lazima uwe na uzoefu usiopungua miaka 7 kazini, ameshuhudia mengi huyu kaimu.

LGA alipofariki huyo bwana wangewasaidia tu bila kuombwa watu wa Tarime (kama shida ni fedha) hata kwa hela za mfukoni mwao, maana taarifa walikuwa nazo, maiti ipo hospitali yao na majeruhi nao huenda wapo hospitali zao.
 
Hapo inawezekana kaimu mkurungezi alishauliwa harafu akakata ushauri wa kwamba viti vifunguliwe ili mwili ukae ndan,kosa lake ni kufunga juu ya gari wakati ndani ungewezekana kuingia ndani ya gari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…