Waziri Jafo amuondoa kwenye nafasi yake Meneja wa TARURA jijini Arusha kwa kushindwa kuita Wananchi kushuhudia ufunguzi wa barabara

Anamuonea bure Arusha wanajitambua hakuna watu wa kusombwa kwenye malori kwa elfu tanotano.
 
Me nadhani waziri anamuharibia raisi kwa kujua au kutokujua haiwezekani sababu hizo kumuhamisha mtu ambae hajaiba nakasimamia mradi nakukamilika vyema halafu meneja ni Mtendaji hiyo kazi yakukusanya watu niyakisiasa zaidi ndio mana kuna wakuu wamikoa, wilaya na wakurugenzi hata kanuni zautumishi zinakataza kutweza utu wa mtu namna hiyo kwa maslahi yakisiasa.
 
Kulewa madaraka ndo hivi.
Hivi wahandisi na mameneja wao wana jukumu la kuita na kuwakirimu mawaziri katika miradi ya serikali?
Na fungu hilo lipo?
Jafo kwa kweli ni mpuuzi san.
Hatujasahau sakata la SKOL kule Dodoma aliporap mpaka mtu akazimia!
 
Sasa Jafo alitaka huyo Engineer akatafute wananchi waje wamsikilize? Wananchi waache kutafuta ugali wao waje wamsikilize yeye aliyeshiba? Labda wawe wanaccm. Jafo amelewa sifa tangu adhulumu uchaguzi wa serikali za mitaa amekuwa kipenzi cha JPM
 
Vyeo vya kuteuliwaa kwa tz ni upuuzi tuu...!! Sasa hapo meneja kosa lake lipii...yani kazi ya mkurugenzi kukodi gari la matangazo ilii kuwajulisha wananchi lawama anapewa Meneja wa tarulaaaa...
 
Huyu naye kwanza kuwa na tabia za ajabusana. Kwani lazima watu waje.??? Unaweza kuwaalika lakini bado wakaacha tu kuja kwani hio Ni hiari.
Pili ni ishara ya ccm kutokubalika na Mambo yake ya uonevu
 
Nilichojifunza hapa ni kuwa Mh Jafo anajua kabisa Jpm hakuna alichofanya cha kuwashawishi watanzania. Na anataka kuhamisha lawama zinazomfika Jpm kuwa ni kwa sababu ya watendaji hawaoneshi mafanikio ya jpm, tena anaongeza kuwa wanamhujum.😅😅😅😅😅😅
 
Hahaaa mkurugenz8 alikosa pesa za kukodi malori ya kubeba wanalumumba😁😁
 
Huyu naye kwanza kuwa na tabia za ajabusana. Kwani lazima watu waje.??? Unaweza kuwaalika lakini bado wakaacha tu kuja kwani hio Ni hiari.
Pili ni ishara ya ccm kutokubalika na Mambo yake ya uonevu
Au hizo barabara ziko whatsapp kwamba lazima uite watu ndio wazione?? Eti wanasababisha wananchi waone serikali haijafanya kitu. Kwani hiyo barabara ya Arusha ndio itafanya tuon3 kafanya kitu. Hii awamy ni ya hovyo sana.
 
Unaenda kuweka kukagua barabara eneo la Njiro tena VETA/ ATOMIC kule unategemea wananchi wajitokeze.. Uonevu kwa Engineer.. Lawama zilitakiwa kuwa kwa UVCCM na washirika wao wa uhamasishaji..
 
Sasa jafo Alitaka huyo meneja paige tarumbeta keita wananchi? Huyo kazi ya mkuuwa Wiley bana na mkurugenzi was Jiji
 
Au uyo meneja aliificha hiyo barabara chumbani wananchi tusiione? Jafo aache ujjnga
 
serikali hii inatia aibu sn.....wakoloni walifanya haya yote lkn awakuwahi kujisifia lkn hawa wamelewa madara basi kila kitu wanamsingizia rais......

Mm ningekua rais nisingekubali kuchuma hii dhambi take huyu isingeisha siku nishamtumbua
 
Huu ni mpango na maagizo ya mkuu angalia sababu ya kumtumbua linganisha na Kanda anayotokea utajua sababu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…