Waziri Jafo asema atabandika majina hata ya wale waliojitoa na kura zitapigwa

Chama ndio kigezo kikuu kwa sababu katiba hairuhusu mgombea asiekuwa na chama yaani mgombea binafsi. Hivyo chama kikijitoa ina maanisha wagombea wote wa chama kilichojitoa wamepoteza sifa ama nafasi ya kugombea.
 
akili zile zile za Lumumba! zile zile! Hatuna mgombea binafsi, chama ndiyo kinasimamisha mgombea., kikijitoa basi kila kitu kina collapse!

Technicalities... taja neno hili mara tatu.
Pamoja na kuwa wagombea wanafanya hivyo chini ya chama fulani. Lkn kugombea au kutogombea ni utashi wa mgombea mwenyewe. Chama kikisema kimejitoa, kikanuni wagombea wa chama hicho bado wana sifa na ni wagombea halali. Lkn mgombea mwenyewe akijitoa rasmi kwa kanuni zilizopo basi hawi mgombea.
 
Hata Seif Sharif kwenye Uchaguzi wa marudio alitangaza kujitoa lakin hakutolewa kwenye karatasi za kupigia kura
Uchaguzi ni kama ndoa ya kikristo, kuingia rahisi ila kutoka sasa ...
Ccm huwa hapo wanakwama wanalazimisha mtu aonekane kwenye karatasi kama yupo wajifariji kifungu kipi cha katiba kinazuia mtu kujitoa? Utagundua ni mafisi huwa yanayafuta pa kujifichia
 
Ubabe umetawala sana acha tu abandike maisha yanaendelea, kila kitu kina mwisho wake na taratibu mwisho unakaribia, tena unakaribia bila watu kusukumana wala kutoana jasho. Ilizoeleka kila unapofanyika uchaguzi kuna kuwa na malalamiko ya wizi wa kura, wapiga kura walipochoka wakaamua kususa kujiandikisha kwa njia ya amani na utulivu. Kwa kuwa kupiga kura ni siri ya mtu wale wachache waliojiandikisha bila kujali vyama vyao dalili zimeonyesha hakutokuwa na uwezekano wa ushindi wa kishindo. Hivyo ikaja mbinu mpya yakuwaengua wengine ili dhana ya ushindi wa kishindo ibaki kama ilivyo pangwa. Kulazimisha kubandika majina ni mtego, itapelekea watu kwenda kupiga kura lakini katika hesabu zitahesabiwa kuwa ni kura zilizo haribika kwa sababu wagombea walio wapigia vyama vyao vilisha jitoa na mshindi atatangazwa kama ilivyopangwa kwa kigezo kwamba watu wamepiga kura.
 
Huu uchaguzi anatafutwa atakayewafaa wananchi wote sio wanachadema tu!!! Kama hawafai nyie wengine wanamtaka
Si muendelee tu na uchaguzi wenu kama mlivyopanga??? Kwani lazima jina CHADEMA au ACT liwemo??? Mlipanga kuwakata na wao wamekubali na wamewasaidia ili msitumie nguvu nyingi, tatizo lipo wapiii?????? Yaani mmekuwa wababe hata aibu hamuoni. Utafikiri askari wa zamani wa kimakonde, ukisimama nchale, ukikaa nchale, ukikimbia nchale, ukilala nchale, ukichuchumaa nchale.

Vyombo vyote vya dora mnavyo nyie wanyonge wameamua kuwapisha njia mpite ili kuepusha shari hamtaki. Sijiu ni nani siku hizi anayewatengenezea strategic plan, yaani mnapangaga vitu bila hata kujiuliza maswali.
 
Tonge La Mwisho Ndiyo La Kukombea Mboga Unaweka Kishimo Kwa Dole Gumba (Kibwinko)
 
Hata Seif Sharif kwenye Uchaguzi wa marudio alitangaza kujitoa lakin hakutolewa kwenye karatasi za kupigia kura


Uchaguzi ni kama ndoa ya kikristo, kuingia rahisi ila kutoka sasa ...
Sawa lakini si wameenguliwa hao watu?? Sasa sifa za kugombea zimetoka wapi?
 
Kwa kweli leo nadhani wanaona kunaumuhimu wamgombea binafsi wangepata chaka lakujifika kila siku tunaambiwa mh kafanya kazi kuliko nawapinzani wakaacha nafasi zao kwenda kuunga juhudi za mh pia vyama viunga navyo mkono kulazimishana kunatoka wapi nilitegemea kwakile kilichokuwa kinazungumzwa kuhusu mh nakazi zake nakuvizuia vyama haki yakutandaza sera pia nakubaki chama kimoja kikijisifu kununua ndege nk. ulikuwa ulikuwa wakati watuachie wananchi tuonyeshe kile tunachokijua Sisi tena kwauhuru nahaq
 
Hivi mkuu mmesha niengua kua nimejaza fomu vibaya kuna haja gani tena ya kuwaomba nijitoe !!!!Si ni maajabu hayo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…