Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kuwa msimamizi wa uchaguzi na kada wa CCM kwa wakati mmoja!Kiaje
Chama ndio kigezo kikuu kwa sababu katiba hairuhusu mgombea asiekuwa na chama yaani mgombea binafsi. Hivyo chama kikijitoa ina maanisha wagombea wote wa chama kilichojitoa wamepoteza sifa ama nafasi ya kugombea.Jafo Yuko sahihi.
Mchakato ulishakamilika .
Mtu aliyegombea ndiye anatakiwa atangaze kujitoa sio atolewe na Chama Hadi dakika hi hakuna mgombea yeyote wa upinzani aliyetangaza yeye binafsi kujitoa kwa wasimamizi wa uchaguzi.Swala la kujitoa ni.la mgombea sio Chama.Chama hakikuomba kugombea.Na hakuna mahali kwenye fomu ya kugombea ambapo Chama kiliomba kugombea
akili zile zile za Lumumba! zile zile! Hatuna mgombea binafsi, chama ndiyo kinasimamisha mgombea., kikijitoa basi kila kitu kina collapse!
Ccm huwa hapo wanakwama wanalazimisha mtu aonekane kwenye karatasi kama yupo wajifariji kifungu kipi cha katiba kinazuia mtu kujitoa? Utagundua ni mafisi huwa yanayafuta pa kujifichiaHata Seif Sharif kwenye Uchaguzi wa marudio alitangaza kujitoa lakin hakutolewa kwenye karatasi za kupigia kura
Uchaguzi ni kama ndoa ya kikristo, kuingia rahisi ila kutoka sasa ...
Wewe mwehu hauwezi kujua kama ni mwehuHaijatumika demokrasia kuwakataza watu wasigombee
Mbowe ametumia ubabe
Ubabe umetawala sana acha tu abandike maisha yanaendelea, kila kitu kina mwisho wake na taratibu mwisho unakaribia, tena unakaribia bila watu kusukumana wala kutoana jasho. Ilizoeleka kila unapofanyika uchaguzi kuna kuwa na malalamiko ya wizi wa kura, wapiga kura walipochoka wakaamua kususa kujiandikisha kwa njia ya amani na utulivu. Kwa kuwa kupiga kura ni siri ya mtu wale wachache waliojiandikisha bila kujali vyama vyao dalili zimeonyesha hakutokuwa na uwezekano wa ushindi wa kishindo. Hivyo ikaja mbinu mpya yakuwaengua wengine ili dhana ya ushindi wa kishindo ibaki kama ilivyo pangwa. Kulazimisha kubandika majina ni mtego, itapelekea watu kwenda kupiga kura lakini katika hesabu zitahesabiwa kuwa ni kura zilizo haribika kwa sababu wagombea walio wapigia vyama vyao vilisha jitoa na mshindi atatangazwa kama ilivyopangwa kwa kigezo kwamba watu wamepiga kura.MATOKEO YA RUFAA ZA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KUTOLEWA NOVEMBA 10.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI SELEMANI JAFO akizungumza Jijini Dodoma amesema katika zoezi la kuchukua fomu kuna makosa mbalimbali yalifanyika katika kujaza fomu nyingi ikiwa ni pamoja na kaukosea majina ya eneo pamoja na udhamini. .
.
Akizungumza jijini Dodoma JAFO amesema kuwa kutokana na ziara aliyoifanya katika sehemu mbalimbali amegundua uwepo wa makosa hayo ambapo amesema baadhi ya maeneo wagombea wameigana na kufanya makosa yanayofanana. .
.
Amesema katika zoezi la kuchukua fomu asilimia zaidi ya 98 wagombea wamerudisha fomu na rufaa zaidi ya 13,000 zimewasilishwa ambapo kesho ndio rufaa zitatolewa ili kujua ngapi zimekubaliwa na ngapi zimekataliwa kwa wagombea wote waliowasilisha mapingamizi bila kujali vyama vilivyojitoa kwenye uchaguzi na watakaoteuliwa majina yao watakuwepo siku ya uchaguzi.
Si muendelee tu na uchaguzi wenu kama mlivyopanga??? Kwani lazima jina CHADEMA au ACT liwemo??? Mlipanga kuwakata na wao wamekubali na wamewasaidia ili msitumie nguvu nyingi, tatizo lipo wapiii?????? Yaani mmekuwa wababe hata aibu hamuoni. Utafikiri askari wa zamani wa kimakonde, ukisimama nchale, ukikaa nchale, ukikimbia nchale, ukilala nchale, ukichuchumaa nchale.Huu uchaguzi anatafutwa atakayewafaa wananchi wote sio wanachadema tu!!! Kama hawafai nyie wengine wanamtaka
Sawa lakini si wameenguliwa hao watu?? Sasa sifa za kugombea zimetoka wapi?Hata Seif Sharif kwenye Uchaguzi wa marudio alitangaza kujitoa lakin hakutolewa kwenye karatasi za kupigia kura
Uchaguzi ni kama ndoa ya kikristo, kuingia rahisi ila kutoka sasa ...
Kwa kweli leo nadhani wanaona kunaumuhimu wamgombea binafsi wangepata chaka lakujifika kila siku tunaambiwa mh kafanya kazi kuliko nawapinzani wakaacha nafasi zao kwenda kuunga juhudi za mh pia vyama viunga navyo mkono kulazimishana kunatoka wapi nilitegemea kwakile kilichokuwa kinazungumzwa kuhusu mh nakazi zake nakuvizuia vyama haki yakutandaza sera pia nakubaki chama kimoja kikijisifu kununua ndege nk. ulikuwa ulikuwa wakati watuachie wananchi tuonyeshe kile tunachokijua Sisi tena kwauhuru nahaqWaziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo amesema vyama vya siasa ndivyo vimejitoa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa sio wagombea, na kwamba wagombea wa vyama vilivyojitoa waliokata rufaa, matokeo ya rufaa yakitoka na wakishinda, majina yao yatajumuishwa kwenye karatasi za uchaguzi..
Hoja:
Ivi mtu akienguliwa na chama huwa anabaki kuwa mwanachama? Na mtu akivuliwa uanachama na ni diwani au mbunge huwa anabaki na cheo chake? Hii sheria imetungwa lini?
Kwanini wanalazimisha ushiriki kwanini hawafurahi wapinzani kuwaachia waendelee kushinda bila lupingwa
Basi waandike barua ya kujitoa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa kwa wahusika yaani hao wasimamizi wa uchaguzi au msajili wa vya siasa,wakiainisha mambo ambayo hawakuridhishwa nayo katika mchakato mzima wa uchaguzi,hapo huenda msajili akakaa nao meza moja kujua nini kifanyike,kumbuka baada ya kugomea uchaguzi wanaweza kuchukuliwa hatua kali za kisheria,lakini pia wanaweza kupata mwanga wa chaguzi zijazo zitakavyosimamiwa,wasitangaze tu kwenye vyombo vya habari kisha wakaa kimya.hali itakuwa mbaya sana mwakani,yule dada wanamwita mange kimambi aliwahi kusema kuna uwezekano kusiwe na mbunge hata mmoja wa upinzani bunge la awamu inayofuata.dalili zimeanza kuonekana mapema kwenye huu uchaguzi, tunaelekea kubaya sio siri.