Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Jafo amesema hayo jana Jumanne Aprili 23, 2024 akitoa majumuisho ya jumla kuhusu hoja za Wabunge zilizotokana na mjadala wa bajeti ya wizara hiyo.
“Kaka yangu pale alipozungumza kwamba, kwa nini watu wasiingie na pasipoti Zanzibar, nikasema aah! kaka wazo zuri lakini unataka kuturudisha nyuma.”
“Katika mchakato huu Serikali ya awamu ya pili chini ya hayati Mzee Mwinyi (Ali Hassan Mwinyi) wakati kule Serikali iliyokuwa chini ya Rais Dk Salmin Amour, kipindi kile walikuwa wanajadili, jambo hili lilitoka kipindi hicho likaonekana linaleta usumbufu,” amesema Dk Jafo.
“Hivi mtu leo mtani wangu Gwajima (mbunge wa Kawe, Josephat Gwajima) atoke Kawe akienda kule Zanzibar atafute pasipoti, tutarudi nyuma sana, na hii si makusudio ya Muungano wetu,” amesema.
Hoja ya kurejesha pasipoti Zanzibar ilitolewa na mbunge wa Konde, Mohamed Said Issa aliyesema Rais wa kwanza hayati Mwalimu Julius Nyerere alikuwa ana akili sana na kwamba haamini kama alizidiwa maarifa na Rais Sheikh Abeid Amani Karume kwa kusema Zanzibar watu waingie kwa utaratibu.
=======================
Minister Dr. Selemani Jafo said that the proposal to reinstate the requirement for mainland Tanzanians to enter Zanzibar with a passport would be a step backward. He mentioned that during the second phase of the government, under the late President Ali Mwinyi, this issue was discussed and it was deemed to be troublesome. Jafo emphasized that this would cause significant setbacks and is not in line with the spirit of our Union.
Pia soma