Waziri Jafo: Tanzania Bara kuingia Zanzibar kwa pasipoti ni kujirudisha nyuma

Naunga mkono hoja.
 
PASSPORT ZANZIBAR NI MTEGO
Mkikubaliana na huu MTEGO huu
Ni moja ya mlango wa kuvunja Muungano. Mtu anayekuambia anaupenda Muungano alafu anataka mtu aingie Zanzibar Kwa passport ni mnafiki. Mbinu zinatafutwa za kila namna kuvunja Muungano
 
Zanzibar kwasisi watanganyika tuende tukafanye nini?
 
Serikali tatu zitasababisha chokochoko kama hizi zipate nguvu. Inahitajika serikali moja kwa mustakabali mwema wa Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla.
Tanzania ni moja, Wazanzibari wakifaidi muungano (mmoja mmoja) kuliko Watanganyika.
Hata hivyo, faida za kitaifa ni kubwa zaidi ya zile za mtu binafsi.
 
KUINGIA KWA PASSPORT ZANZIBAR NI MTEGO.
Mkikubali huu MTEGO utadumbukizwa Kwenye mengine wanayoyadai kirahisi
Hakuna Namna mtachomoka
 
Waweke sheria kuingia Zanzibar kwa MTANGANYIKA iwe kwa VISA!
 
Nyerere alizidiwa akili na Karume kwenye muungano, aliifuta Tanganyika ila Zanzibar imebaki, wao wanakula kote kote ila hawataki sisi tule vyao.

Kuna mzanzibari moja katika kila watanzania 30 lakini wao lazima wawe rais ama makamu wa rais, wanapewa vipaumbele kwenye vyeo, katika kila ajira 10 za Tanzania kuna nafasi zao mbili, n.k.

Rais wetu wa sasa mzanzibari akipendekeza kuwe na passport sioni wa kumpinga.
 
Nyerere alizidiwa akili na Karume kwenye muungano, aliifuta Tanganyika ila Zanzibar imebaki, wao wanakula kote kote ila hawataki sisi tule vyao
lengo la Nyerere msiende kuijenga zenji bali wao waje kujenga Bara
 
Zamani tulikuwa tukienda na passport hawa wanataka kuirudisha tena

Ova
 
Mbona ndio fursa Kwa wabara kuomba passport?

Hata Sasa hivi kuingia Zanzibar unatakiwa uonyeshe kitambulisho chako na wabara hamjawahi kulalamika.
 
Waachieni nchi yao. Kwani lazima kuungana.

"Demu kama hataki, usimbake, kulazimisha penzi ni hatari"

Mkuu hapa tunaongelea ndoa, unafikiri mchezo ukautafute mchanga uuchambue wa Tanganyika na Zanzibar uutenganishe?
 
ishu sio Nyerere ishu ni viongozi wenu baada ya mwalimu Nyerere πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ
 
KUINGIA KWA PASSPORT ZANZIBAR NI MTEGO.
Mkikubali huu MTEGO utadumbukizwa Kwenye mengine wanayoyadai kirahisi
Hakuna Namna mtachomoka
Kila jambo na wakati wake.
Yote kheri.
Wafanye kwa kadiri wanavyo ona inafaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…