Watanzania wengi hawujui chochote kuhusu umeme na mikataba zaidi ya kwamba ni wahanga wa uwongo wa Magufuli. Na kwa ujinga wao ndiyo walikuwa mtaji wa Magufuli kwa miaka 5.
JNHPP was wastage of money. Hilo dude litabakia white elephant. Litajengwa ila halitakuja kuzalisha hizo megawati 2,100 za umeme.
Kwa maamuzi ya Dikteta mmoja mkemia asiyeamini sayansi, tumeharibu baioanuai ya selous na kukata miti yenye saizi ya ukubwa wa Mkoa wa Dar es Salaam. Hili litatugharimu milele.
Ni wakati wa kufanya maamuzi magumu kwa kusitisha kuendelea kujenga na kuendelea na umeme wa gesi. Kwa sasa Kinyerezi 1 & 2 zinachangia 60% ya umeme tunaotumia Tanzania. Na zinatumia hardly 10% ya gesi ya Mtwara
Miradi yote ya maji yaani Kidatu, Mtera, Kihansi, Nyumba ya Mungu, Hale, Pangani nk inachangia 40%. Numbers don't lie. Umeme wa kutegemea mvua siyo reliable na vile vile una athari kwa mazingira.
Kama Magufuli asingetokea mwaka 2015 tungepiga hatua kubwa sana kiuchumi kwa kuwa;
1. Kinyerezi 3 & 4 zingekamilika na kuwa chanzo kikuu cha nishati.
2. Tusingevuruga baioanuai ya Selous kwa kukata miti ili tujenge bwawa la umeme kwa ajili ya kupata Megawati 2,100 tu ambazo zinapatikana kwa kutumia 25% tu ya gesi ya Mtwara.