Pre GE2025 Waziri Jenista Mhagama agalagala chini ikiwa ni ishara ya kumshukuru Rais Samia kwa miradi jimbo kwake

Pre GE2025 Waziri Jenista Mhagama agalagala chini ikiwa ni ishara ya kumshukuru Rais Samia kwa miradi jimbo kwake

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kitu Kinachonitia Hofu sana Ni kwamba Huyo Ndiyo Mshauri wa Rais kwa Upande wa Afya..

Ni vigumu sana Kushauri kitu kwa Kutilia Mkazo kama Atatishiwa au Kukataliwa Mawazo yake..

Napata Hofu sana..

Eeh Mungu wangu Chama changu Kinaenda wapi?😭😭

Najua Kuwa Siwezi kuhama Kwenda Upinzani, Chadema au ACT ila Naumia Nikiyaona haya..

Kwa Uchungu kabisa..
CC:- Tlaatlaah
vijana wasio na utambulisho wa kitamaduni kuna tabu, mshangao na sintofahamu nyingi sana aise dah

hili nalo ni la kushangaza au kusikitisha kweli?🤣

umeshawahi kuwaona wale vijanaa wa kisafwa wanaitwa WAMWIDUKA BAND? wanavaaje kwenye matamasha yao ya Kitaifa na kimataifa? umewahi kushangaa au kusikitika kweli? au huwa unaona wanavaa vibweka vya magunia tu? ule ni utambulisho wa utamaduni wao 🤣

wasukuma na wanyakyusa kwa heshima ya kitamaduni, wakitusalimia sisi wazee huwa wanapiga magoti unadhani kwanini? au nayo huwa unashangaa tu na kusikitika?

wamasai kuvaa mashuka kutwa kucha huwa unashangaa au unasikitika pia?

Unadhani kwanini waziri Jenista Muhagama hakugalagala akiwa mkoa wa Pwani au Manyara au mahali pengine nchini, kaenda kugalagala jimboni kwake paramiho?
bila shaka asingeeleweka ndipo huenda ungepaswa kushangaa..

hufahamu kwamba ule ni utamaduni wa Kingoni katika kushukuru na kwamba licha ya kua ni waziri lakini anaheshimu na anathamini na kujali utamaduni wao wa Kingoni, lakini pia ametangaza utamaduni na utalii wa Kingoni nje ya paramiho, Ruvuma na songea kwa ujumla ?🐒

wasio na utambulisho wa utamaduni wao ndio hawa wa kuvaa vigodoro, kuvaa hereni na kutoboa pua tu mijini 🤣

Ule ni utamaduni wa Kingoni katika kushukuru kwa heshima ya kiwango cha juu sana gentleman.
 
Fikiria huyo ni waziri anafanya huo uchawa, je chawa kama ChoiceVariable na Lukas mwashamba unadhani wanaweza kufanyaje? Lakini bahati mbaya kwa taifa chawa hao ndio wanaongoza wizara na idara mbalimbali za serikali.
🤣😅🤣😅🤣 Ujinga ni mzigo kwakweli, alitakiwa aandae wamama UWT na wanawake bwa rank ya chini ndani bya chama!!!!
Sio waziri bwa Afya!!! hatari sana hii!!
 
Kwa hakika kazi aliyoifanya RAIS Samia ndani ya hii Miaka anastahili pongezi na kuungwa mkono.maana ni kama ndoto vile. Kwa sababu huwezi kuamini katika muda na miaka hiyo mitatu ameweza kukamilisha Bwawa la umeme la Mwalimu Nyerere,ujenzi wa reli ya kisasa kabisa ya umeme,utoaji wa Elimu bure hadi kidato cha sita,kuongeza bajeti ya wizara ya kilimo kufikia Trilioni moja na pointi,kutiririsha zaidi ya Trilioni sita secta ya Afya ,ujenzi wa barabara mbalimbali Nchini,ujenzi wa hospitali bora na za kisasa na zenye vifaa bora na vya kisasa.ujenzi wa vyumba vya madarasa zaidi ya elfu 20 na mengine mengi sana.

Kama vile kuwapandisha madaraja na kuwalipa malimbikizo ya madeni yao watumishi wa umma,kutoa ajira kwa vijana na mengine mengi
Kazi walizofanya WATANZANIA tax payers!!

Then serikali ikatumia kodi zetu kwa maendeleo!!
 
Kwa hakika kazi aliyoifanya RAIS Samia ndani ya hii Miaka anastahili pongezi na kuungwa mkono.maana ni kama ndoto vile. Kwa sababu huwezi kuamini katika muda na miaka hiyo mitatu ameweza kukamilisha Bwawa la umeme la Mwalimu Nyerere,ujenzi wa reli ya kisasa kabisa ya umeme,utoaji wa Elimu bure hadi kidato cha sita,kuongeza bajeti ya wizara ya kilimo kufikia Trilioni moja na pointi,kutiririsha zaidi ya Trilioni sita secta ya Afya ,ujenzi wa barabara mbalimbali Nchini,ujenzi wa hospitali bora na za kisasa na zenye vifaa bora na vya kisasa.ujenzi wa vyumba vya madarasa zaidi ya elfu 20 na mengine mengi sana.

Kama vile kuwapandisha madaraja na kuwalipa malimbikizo ya madeni yao watumishi wa umma,kutoa ajira kwa vijana na mengine mengi
Sahivi sio tu kububujikwa, ni kugalagala kwa furaha.
 
Huu utamaduni ni wa kujikomba na kutupumbaza sisi wapiga Kura.

Kama waziri anacheza sinema hii ili atie simenti Kali ili kulinda kitumbua chake.

Ningekuwa rais huyu Mhagama Leo hii ningetengua uteuzi wake kabisa.

Watanzania wa Leo tumesharunguka macho hivyo hii ngonjera tushazistukia.

Waziri Mhagama naomba ujitafakali Kwa kitendo chako hiki.

markup_1000012699.png
 
Waziri wa Afya ambaye pia ni Mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama akigalagala ikiwa ni ishara ya kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika jimbo lake, wakati Rais Samia Suluhu Hassan alipotembelea na kuzungumza ya wananchi wa jimbo hilo, leo Jumanne Septemba 24, 2024.

My jicho ......

Tuseme kwamba huu ni uchawa au ni udhaifu kwa kiongozi kuonyesha kitu kama hichi kwani alishindwa kushukuru kawaida hadi kufanya alichokifanya binafsi natafsiri ni ushamba wa maarifa. Ifike mahali hawa viongozi wafanye mambo yao kwa uwelidi na sio kuongozwa na mihemuko fulani.

Soma Pia: Kilombero: Mbunge apiga Magoti Kumshukuru Rais Samia kwa Barabara

🔨🔨🔨

View: https://www.instagram.com/p/DATgSAftqCf/?igsh=MXQxeG9hY2ZnZGM4bg==
 
Ni Mila yao kwa kabila lake. Nakumbuka eng. Stella Manyanya aliwahi kufanya hivo pia kama kumbukumbu zangu zipo sawa
 
Huyu mwalimu mwa..nga sio bure, ndiye aliyependekeza makadilio madogo kabisa ya kikokotoo kwa watumishi wa umma.
 
Waziri wa Afya ambaye pia ni Mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama akigalagala ikiwa ni ishara ya kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika jimbo lake, wakati Rais Samia Suluhu Hassan alipotembelea na kuzungumza ya wananchi wa jimbo hilo, leo Jumanne Septemba 24, 2024.

My jicho ......

Tuseme kwamba huu ni uchawa au ni udhaifu kwa kiongozi kuonyesha kitu kama hichi kwani alishindwa kushukuru kawaida hadi kufanya alichokifanya binafsi natafsiri ni ushamba wa maarifa. Ifike mahali hawa viongozi wafanye mambo yao kwa uwelidi na sio kuongozwa na mihemuko fulani.

Soma Pia: Kilombero: Mbunge apiga Magoti Kumshukuru Rais Samia kwa Barabara

Hiyo ni ishara ya kushukuru kwa makabila ya kusini mwa Tanzania,hasa wanawake,kwahiyo usimshangae sana...
 
Back
Top Bottom