Waziri Jerry Slaa: Mimi siyo Mtoto wa Maskini, baba yangu alikuwa Rubani. Nimekataa Rushwa ya Milioni 300

Waziri Jerry Slaa: Mimi siyo Mtoto wa Maskini, baba yangu alikuwa Rubani. Nimekataa Rushwa ya Milioni 300

Mimi kuna kitu sikuelewi

Huyo mwenye petrol station kosa lake nini hasa ? Kwa nini ashupaliwe hivyo?

Kama kujenga kituo labda maeneo ya makqzi uswahilini mbona viko vingi mno tena viko kwenye Mbanano wa wa makazi kote ikiwemo jimboni kwake
Mbona huo mfoko hatujauona akifoka kule wakati vituo kibao viko makazi ya watu?
 
Siyo kama hao wanasiasa wanaona sifa kujitambulisha asili yao kama maskini. Wao wanachosema ndio kweli.

Na ndio ukweli wengi walio uongozini asili yao ni maskini. Nyerere aliwafaidisha sana watoto wa maskini wakapata elimu kisha wengine wakawa matajiri kwa njia sahihi na wengi kwa ulaji rushwa na ufisadi.

Jerry kwa vile baba yako alikua na uwezo unakosea sana kufikiri wanasiasa wenzako kuonesha wametoka kwenye umaskini wanaona fahari.

Wanachotaka tu ni kuwaaminisha raia wengi wao maskini na wanapambana kuinua maisha yao kwamba wanaufahamu umaskin.

Huenda jerry ni mtu wa majivuno na kuna wakati uliwahi kutoa kauli za kumdharau baba wa taifa kwa kujali maskini.

Binafsi nina shaka sana kama ni mtu sahihi kwenye nafasi yako ya uwaziri.
Wanasiasa wa Bongo huwa wanasema wasiyoyaishi !!
 
Awe makini!

Wahuni wasije kumchezea shere!

Wenye misimamo kama hiyo hawapendwi na chama chetu Sasa hivi!

Wasije Wakacheza na afya yake!!

Kataa wahuni!!
Waziri wa Ardhi mh Jerry Slaa amesema kuna Wanasiasa wanaona Sifa kujiita Watoto wa Maskini Lakini yeye siyo Maskini baba yake alikuwa Rubani na hadi leo anakula hela ya Urithi.

Mh Slaa ametuma salamu kwa mafisadi wote kwamba yeye hana Njaa na hapokei Rushwa kwa sababu Biblia imesema mla Rushwa ni kipofu.

Waziri amekataa Rushwa ya tsh 300 milioni kutoka kwa tajiri Mmoja aliyejenga kituo cha Mafuta Kinyume cha utaratibu pale Mikocheni.

I wish you a Merry Christmas 😀
 
Tutakuaminije? Umepataje tender ya kutandaza/ kusambaza maji na kampuni yako ya Mshamindi Construction LTD kule Uhambingeto Wilaya ya Kilolo na umelipwa 90% ya kazi huku hajakamilisha kazi mpaka yule Diwani mwanamke akakushtaki kwa KM wa CCM Chongolo?
 
Waziri wa Ardhi mh Jerry Slaa amesema kuna Wanasiasa wanaona Sifa kujiita Watoto wa Maskini Lakini yeye siyo Maskini baba yake alikuwa Rubani na hadi leo anakula hela ya Urithi.

Mh Slaa ametuma salamu kwa mafisadi wote kwamba yeye hana Njaa na hapokei Rushwa kwa sababu Biblia imesema mla Rushwa ni kipofu.

Waziri amekataa Rushwa ya tsh 300 milioni kutoka kwa tajiri Mmoja aliyejenga kituo cha Mafuta Kinyume cha utaratibu pale Mikocheni.

I wish you a Merry Christmas 😀
Na sisi tutapokea Ili tuondokane na maskini.

Rubani ni sawa tuu na dereva wa ndege so usitutishe
 
Kama anaamini yeye ni tajiri, basi tutafute tafsiri ya neno tajiri, yaani urubani wa baba yake ndio umemfanya kuwa tajiri?
Lakini pia kama ni tajiri asichukuwe mshahara basi wala posho bungeni eti.

Wizara ya Ardhi ukijikana na rushwa ujuwe siku zako hapo zinahesabika kama ilivyokuwa kwa Magufuli, Lukuvi na Mabula.

Ni moja ya sehemu ambazo wateuzi wanatarajia kujipatia ukwasi.

Ukitangazia umma kuwa umekataa kupokea rushwa basi siku ukiletewa za mkubwa kwamba mfikishie mzigo wake pia uutangazie umma kwamba umeletewa mzigo wa mkubwa ukakataa kuupokea kwa kuwa wewe ni msafi.

Sijajuwa Silaa ni wa mrengo gani hapa duniani, kushoto-kati, kushoto (iliyomshinda Zitto) au kulia.
 
Back
Top Bottom