ryan riz
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 423
- 683
Kiukweli sijajua wanaomsifia huyu mtu wanatumia vigezo gani;
1. Baada ya kulipa bili ya kuonganishiwa maji itachukua hata nusu mwaka kuungishiwa bomba mpaka mitaro inajifukia(mabomba wanasema hamna na hapa rushwa na watu wa stoo ndio kwao kama TANESCO).
2. Wananchi kujichangisha mamilioni ili kuisaidia wizara na nyie pia kununua mipira ili mpate maji. Mwisho wa siku mabomba mtaunganishiwa ila hayatoi maji(kama TANESCO, mtajichanga kununua nguzo ishirini ila mtapigwa danadana za mita na waya zimeisha, halafu baada ya miez kadhaa wanakuja usiku kuziiba hizo nguzo mpaka zinaisha).
3. Sehemu ambazo ziko karibu na bomba kubwa la maji, mitaa hiyo mkiomba muunganishiwe huduma ya maji, mtaambiwa subirini masaveya wetu waje wafanye tathmini(hapo itakata miaka). Na ikitokea wamekuja (hapo kwa kulazimisha baada ya kutoa rushwa) utasikia "tumeliona eneo lenu na mnastahili kuunganishiwa huduma, ngoja tukalifanyie kazi". Hapo mtasubiri miaka tena.
4. Madiwani wetu wakienda kule ofisini kwao sijui huwa wanapewa nini? Maana kwenye vikao vya kata wanakuwa wako moto, wao pamoja na wabunge wetu na kuahidi tena kwa munkari kwamba, haipiti mwezi ila wakirudi vikao vijavyo hili suala la maji hulikwepa kabisa kuliongelea!
Nauliza, huyu Aweso huwa anasifiwa kwa jambo gani la maana?