Waziri Juma Aweso, sifa zake zinatoka wapi? Mbona matatizo ya maji ni mengi mno

Wizara ya Maji ni moja ya wizara ngumu sana kuongoza.
Wizi kuanzia wizarani ni mwingi mno.
Fedha inapotengwa bungeni huwa inaliwa wazi wazi na watendaji kuanzia wizarani hadi Halmashauri.

Aweso aliingia wizarani na gia kubwa akifikiri wizi unatokana na watu wa nje kama makandarasi na watoa huduma.
Baada ya muda baada ya kutonywa aliambiwa wizi unatokana na watendaji ndani ya wizara yake.

Mfano: Bunge linatenga fedha kwa ajili ya mradi katika kata A , mkoani B.
Fedha inapelekwa Wizarani na hapo inapangiwa matumizi ya warsha , makongamano na hata mikutano na safari za vigogo nje na ndani ya nchi.
Katika ripoti itaandikwa mradi katika kata A mkoa B unaendelea vizuri lakini fedha hazikutosha.

Sasa Waziri au Katibu Mkuu CCM. mbio za Mwenge au hata viongozi wa juu wakitembelea eneo la mradi, anatafutwa mkandarasi kidampa na anapewa mkataba fasta na fedha kidogo juu juu na kuambiwa awe pale site Waziri akiwepo, na asijibu kitu.
Kweli mkandarasi amepewa fedha LAKINI pale site hakuna kitu,
Waziri atafoka huku watendaji wakikonyezana.
Ndiyo imetoka hiyo.
Sana sana waziri atesema mkandarasi awekwe ndani, kwa siku tatu maana hata yeye waziri hana charge ya makosa.

Watendaji wizarani wanazidi kunenepa huku wakimcheka waziri.

Hayo yamekuwa yakifanywa tokea zamani sana enzi za kina Pius Ng'wandu, Magembe na wengine mawaziri wa Maji.

Serikali bila kuifuatilia wizara hii itaendelea kuwa kichaka cha ufujaji wa fedha za umma.
Waziri Aweso hana exposure wala uelewa wa intricacies za wizara hii ambayo ni very very technical.
 
Sijui nani hata anamsifia, mm namwonaga ni makelele tu mbele ya camera, miradi imejaa upigaji tupu.
 
Kiukweli sijajua wanaomsifia huyu mtu wanatumia vigezo gani;
Nauliza, huyu Aweso huwa anasifiwa kwa jambo gani la maana?
Ndie waziri mweny kelele jukwaani kuliko wote --jamaa ana sauti kama Mtangazaji wa soka goli linapofungwa, tena zile za "Nani Kama Mama!"
 
Watu wakiamua kusifiana ujinga huwa wanafanya hivyo.
 
Yawezekana mtu anae 'mtaalanu' wake konki wa kusafisha nyota; mambo ya ndumba na ngai
 
Kama magari gani? Forester au?
Mkuu wacha waishi kifahari tu na sie tutaendelea kutoa kodi na tozo ili wao waendelee kuishi kifahari na wakati huo huo wakifisadi, ila tu wakati unapokuwa unajaribu kueleza matumizi ya hizi kodi na tozo usisahau kutaja na hayo magari sio unaishia kutaja vituo vya afya tu.
 
Magari ni machache yapo kwa viongozi wa juu tuu..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…