Waziri Kalemani: Bwawa la Nyerere kujazwa Maji Novemba 15, 2021. Umeme wa maji ni nafuu kuliko wa vyanzo vingine

Waziri Kalemani: Bwawa la Nyerere kujazwa Maji Novemba 15, 2021. Umeme wa maji ni nafuu kuliko wa vyanzo vingine

Nuclear ni cheaper zaidi..
Maji kuna gharama za mazingira kubwa Sana
Kufyeka heka zote zile utasema hakuna gharama?

Amepima loss yake? Kufyeka heka zaidi ya milioni?
Hilo bwawa lililojengwa litafaidisha wilaya tano ambazo zinazunguka hilo Bwawa kwa shughuli za uvuvi.Litatengeneza ajira nyingi sana.Likikamilika misamaki hiyo inamwagwa
 
From my experince in Europe. For example, during a windy day, electricity prizes goes to negative. Upepo unapokuwa mwingi bei ya umeme inakuwa negative japo hali hii haitokei kila siku au kwa muda mrefu.
Nashukuru kwa hizo taarifa.


Little direct benefit​

Consumers whose power agreements are directly tied to the power exchange will benefit the most from the negative price dip. However, savings are likely to be minimal as electricity distribution prices still apply.

Negative electricity prices are more common in Denmark and Germany, which have more wind power capacity than Finland.
 
Waziri nishati Dkt. Kalemani asema Bwawa la Nyerere kujazwa Maji Novemba 15 mwaka huu wa 2021 aeleza gharama za kuzalisha umeme kwa kila chanzo bunge lamshangilia sana...
Muongo amekubali bwawa lianze kujazwa maji?
 
Waziri nishati Dkt. Kalemani asema Bwawa la Nyerere kujazwa Maji Novemba 15 mwaka huu wa 2021 aeleza gharama za kuzalisha umeme kwa kila chanzo bunge lamshangilia sana...
Aweke akiba ya maneno sie ikikaribia tutamkumbusha kwani tumeweka alarm kbs

Sent from my Nokia 3.2 using JamiiForums mobile app
 
Tulipofikia, unaweza kuwapa mtihani mmoja wahitimu wa darasa la saba na maprofesa na madokta na wahitimu wa la darasa la saba wakafaulu mtihani huo kuliko hao wengine.
Eeenheee, Heee,

Naliwaza hili kwa makini sana.

Hapana.

Labda kama umeandaa kitita cha mabilioni hapo pembeni na ahadi ya hao watakaofeli wanakibeba kitita hicho!

Huo ndio msukumo huu unaowaondoa akili wote toka "Jalalani" hadi sijui wapi!
 
Waziri nishati Dkt. Kalemani asema Bwawa la Nyerere kujazwa Maji Novemba 15 mwaka huu wa 2021 aeleza gharama za kuzalisha umeme kwa kila chanzo bunge lamshangilia sana...
Hamna lolote! Sasa kama umeme wa maji ni rahisi unit ni shilling 36, kwani umeme tunaotumia sisi wa Kidatu na Kihansi si wamaji, mbona tunalipa shilling 320 kwa Unit? Ndio zao hao tusije tukajikuta umeme huhuo wa bwawa la Nyerere tuuziwe unit kwa 500sht
 
Hayo maji nasikia kujaa kwenye hiko bwawa ni miaka 5 eti ni kweli
 
Nuclear ni cheaper kuliko gasi, tatizo ni usalama; infrastarture ya Nuclear power plant inahitaji investmenet kubwa sana ili kuthibitisha usalama kuliko power sources nyingine.
Nyuklia si nafuu! Gharama za bima za ajali (ambazo kila kituo cha umeme kinahitaji!) ni juu mno kiasi cha hadi sasa nchi nyingi zilifuta masharti haya kwa vituo vya nyuklia. Maana gharama zimefichwa. Pale unapohitaji kuweka bima, hakuna anayejenga. Au unajua mfano??? Lete!

Halafu gharama za kushughulika takataka nyuklia ni kubwa zimezidi kupanda. Maana si fueli iliyotumika tu, baada ya matumizi (mwisho) wa kituo kila punje ya saruji ya jengo, kila skrubu inayobaki ni hatari inahitaji kutunzwa kwa miaka mingi hadi mnururisho umekwisha.
 
Nashukuru kwa hizo taarifa..
Hizi "bei has" hazifikii kwenye ngazi ya mteja; Hadi sasa umeme wa upepo una changamoto kuna njia chache mno ya kuihifadhi; bei kati ya watengenezaji na makampuni makubwa huwa hasi wakati upatikanaji wa umeme unazidi mahitaji.

Makampuni ya kuuzia umeme yanalazimishwa kuwa na vituo vya nyongeza kwa vipindi ambako upepo hautoshi. Vituo hivi vya akiba ni sababu ya bei kubwa za umeme kwa wateja wa kawaida katika nchi za Ulaya.

Kuna mipango kutumia umeme wa ziada kwenye vipindi ambako hauhitajiki kuzalisha hidrojeni (kwa kupasua maji kuwa hidrojeni na oksijeni, vinavyopatikana ukiingiza umeme kwenye maji) na kutumia hidrojeni kama fueli ya magari na vituo vya umeme. Ila hadi sasa mahitaji ya uwekezaji yalikuwa kubwa mno..
 
Si nasikia alirudia rudia shule za misingi mara kibao!!!!
 
Kuna jamaa yangu alinidokezea kuwa walishachukua usa toka enzi za mkwere!
Sio kweli kule wapo Mantra chini ya Uranium One ya Urusi. Ingawa na Muhongo ndio aliwasainisha mkataba huku anawarushia makaratasi... Baada ya Mkwere na Nyarandu kuvuta chao halafu fupa wakamwachia prof.
 
Ninawasalimu wote,

Waziri wa Nishati Dkt. Kalemani amesema Bwawa la Nyerere litajazwa Maji Novemba 15 mwaka huu wa 2021 na ameeleza gharama za kuzalisha umeme kwa kila chanzo kuwa,

• Maji ni shilingi 36 kwa unit moja.

• Nyuklia ni shilingi 65 kwa unit moja.

• Solar na upepo shilingi 103 kwa unit moja.

• Makaa ya mawe shilingi 118 kwa unit moja.

• Joto Ardhi shilingi 119 hadi 120 kwa unit moja.

• Gas shilingi 147 kwa unit moja.

• Mafuta mazito shilingi 546 kwa unit moja.

Pia alisema umeme wa maji ndio wa nafuu kuliko vyanzo vingine vyote. (Alipokuwa akitoa Taarifa hii kulikuwa na shangwe za kutosha).

Binafsi nampongeza sana kwa ufafanuzi alioutoa.

Lakini nahitaji Mheshimiwa Waziri wa Nishati atuambie na Kututhibitishia kwa UWAZI kabisa GHARAMA AMBAYO MTUMIAJI WA UMEME ATATOZWA KWA KILA UNIT MOJA (1) baada ya BWAWA LA MWALIMU NYERERE Kuanza kuzalisha Umeme.

Hii habari ya kutuambia na kutuaminisha kuwa Umeme wa Maji ni umeme wa Gharama nafuu bila kutuambia na kutuhakikishia Gharama halisi kwa Unit Kwa Mtumiaji wa Mwisho ni kutuona Sisi Watanzania kuwa ni Wajinga.
 
Tanzania wamejaa akina profesa Muhogo ambao enzi zao walikuwa wanaingia mikataba mingi ya kitapeli kwa manufaa yao na wakati mwendazake alipokuwa hai hawakuwa na jeuri ya kubweka kama wanavyobekwa hivi sasa, kweli mwendazake alikuwa chiboko mijizi na mitapeli yote ilikuwa kimya
 
Unaonyesha umbumbu wako, hiyo hapo ni bei ya kuzalisha, ukiuza unit 1 sh 37 inamaanisha Maintainance cost na kurudisha pesa ya investment hamna, bei itashuka kidogo sana Ila shirika la Tanesco litaanza kutengeneza faida ambayo inaweza kutumika kuanzisha miradi mingine badala ya kuchota serikali kuu.

FYI; Kipindi cha JK Tanesco walikuwa wanauziwa unit moja zaidi ya Tsh 400 sababu ya mikataba ya kijinga ya Dowans, IPTL na ifananayo...
 
Unaonyesha umbumbu wako, hiyo hapo ni bei ya kuzalisha, ukiuza unit 1 sh 37 inamaanisha Maintainance cost na kurudisha pesa ya investment hamna, bei itashuka kidogo sana Ila shirika la Tanesco litaanza kutengeneza faida ambayo inaweza kutumika kuanzisha miradi mingine badala ya kuchota serikali kuu.

FYI; Kipindi cha JK Tanesco walikuwa wanauziwa unit moja zaidi ya Tsh 400 sababu ya mikataba ya kijinga ya Dowans, IPTL na ifananayo...

..una uhakika kwamba mkopo tuliochukua kwa ajili ya stieglers ni wa masharti nafuu?

..waziri anatakiwa atueleze baada ya stieglers kukamilika gharama ya unit ya umeme itashuka kiasi gani kulinganisha na sasa hivi.
 
Hizi stori za unafuu wa bei za upatikanaji wa nishati huwa zinapigwa Sana wakati wa ujenzi wa mradi.

Gesi ya Mtwara tuliambiwa Mtwara itageuka kuwa Paradiso na Tanzania itajaa neema. Lln mpk Sasa hatuoni

Sio story ni vitu halisia, TANESCO ilikuwa katika hali ngumu sana kibiashara kipindi cha JK, umeme wa Dowans na IPTL ulikuwa unatumia mafuta mazito ambao ndio umeme wa gharama zaidi, kama isingekuwa maamuzi ya kibabe na kishujaa ya Magu mpaka saivi tungekuwa tunaongelea hasara tu za TANESCO.
 
Back
Top Bottom