Waziri Katambi aagiza Dudubaya akamatwe kwa kukaidi Wito wa Serikali

Waziri Katambi aagiza Dudubaya akamatwe kwa kukaidi Wito wa Serikali

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251





Video ya Dudu Baya
​
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, ameliagiza Jeshi la Polisi kumtafuta na kumfikisha mbele ya vyombo vya sheria msanii Godfrey Tumaini maarufu Dudubaya, baada ya kushindwa kuitikia wito wa Wizara hiyo.

Akizungumza na wanahabari leo Ijumaa, Katambi amesema Dudubaya alikuwa ametakiwa kufika Wizara ya Mambo ya Ndani baada ya kutajwa katika tuhuma za makosa ya jinai, lakini licha ya kuitwa kwa mara ya pili, bado hakufika.

Soma Pia: Malu, pipytida, Dudu baya, Gigy money, Anko T, Noel na Mwijaku waitwa central station

Waziri amesema Dudubaya ameonekana kwenye mitandao ya kijamii akitoa kauli ambayo Waziri ameielezea kuwa ni kukaidi wito wa Serikali.
 
Police, waziri au kiongozi hawatakiwi kuwa na mamlaka ya kuita raia kiholela.

polisi wanaweza kumuita mtu yoyote yule aidha kwa barua, simu au hata wakafika kwako nyumbani au eneo la kazi na kukutaka ufike kituoni kama wanakuhitaji, nafikiri hiyo ndiyo kazi ya polisi, wote tunapenda mabadiliko lkn tusishabikie utovu wa nidhamu kwa kuwa tu tumekwama, kama kapewa mwaliko rasmi na polisi afike kituoni siku xyz basi alipaswa kutii na kufika na kama hakuweza kufika alipaswa awajulishe halafu wao wangeamua nini cha kufanya kama kumpa tarehe nyingine au vinginevyo lkna kukaidi na kukaa kimya siyo, binafsi siipendi hii regime lkn kosa ni kosa ...
 
Kwa nini msingetumia njia hizo za mtandao kumfikia mfano zoom, MS Teams... na kuhusu hilo la kupimwa, huwezi kumuamrisha mtu apimwe, ni uvunjivu wa haki za mtu anayehusika... acheni kumsumbua...

Nani anayetakiwa kupimwa? Na kupima nini? Waanze kutoa majibu ya muhimbili, mbona wamebaki nayo,
😂😂😂😂 ndio raha ya kuwa na akili, Noel hajawahi feli kabisa, kweli Degree yake ya Sheria anaitendea haki.
 
Back
Top Bottom