Waziri Katambi aagiza Dudubaya akamatwe kwa kukaidi Wito wa Serikali

Waziri Katambi aagiza Dudubaya akamatwe kwa kukaidi Wito wa Serikali

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, ameliagiza Jeshi la Polisi kumtafuta na kumfikisha mbele ya vyombo vya sheria msanii Godfrey Tumaini maarufu Dudubaya, baada ya kushindwa kuitikia wito wa Wizara hiyo.

Akizungumza na wanahabari leo Ijumaa, Katambi amesema Dudubaya alikuwa ametakiwa kufika Wizara ya Mambo ya Ndani baada ya kutajwa katika tuhuma za makosa ya jinai, lakini licha ya kuitwa kwa mara ya pili, bado hakufika.

Soma Pia: Malu, pipytida, Dudu baya, Gigy money, Anko T, Noel na Mwijaku waitwa central station

Waziri amesema Dudubaya ameonekana kwenye mitandao ya kijamii akitoa kauli ambayo Waziri ameielezea kuwa ni kukaidi wito wa Serikali.
Sasa Katambi anaingiza utoto kwenye kazi yake.
Kaamua kucheza na machizi, na yeye anaonekana chizi.
 
hawalazimiki kukwambia wanachokuitia, lazima uelewe kazi ya polisi ni kulinda usalama wa raia, hivyo kama wewe ni raia mwema kwa hali ya kawaida hauna cha kuhofia kwani ndiyo sehemu inayaopaswa kuwa salama klk zote kwa raia in theory at least na unapaswa kutii, usipotii kuna sheria inayowalinda kwa kukukamata na kukufungulia mashitaka ya kukaidi wito.
again sijui undani wa hiyo kesi, ila naongelea kiujumla polisi anaweza kumuita mtu yoyote yule kutaka ufike kituoni hiyo ni kawaida kabisa na ni dunia nzima na hawalazimiki kukwambia sababu ya kukuitia kabla ya kuripoti kuna wengine wanaweza kukwambia upige simu mkayamaliza kwenye simu au wengine wakataka ufike kituoni au hata wakatia timu kwako au ofisini lkn kuitikia wito siyo hiari ...
Nakubaliana ni lazima uende ukiitwa. Lakini lazima wakwambie sababu. Mfano Kuna mashitaka kuhusu jambo fulani. Kama wanadhani kwa kukwambia utatoroka basi wakamkamate. Na hata unapokamatwa lazima uambiwe tunakukamata kwa..... Ila bongo wakikudaka utasikia ujua mbele kwa mbele? Why ? Na hiyo sio hisia ni sheria. Sasa kama sheria ya kukwambia mtuhumiwa kosa lake ni mbaya, waibadilishe, kuliko kuwa na sheria ambayo police hawaifuati
 
Ndio maana watanzania tunataka katiba mpya. Sasa kama mtu ana jinai anataka akamwone waziri kwa sababu gani? Si angetakiwa aambiwe aende kituoni au akakamatwe? Au ndio ile watuhumiwa wengi ni makosa ya kisiasa
 
Jamaa wanaweza mtoa ktk ramani

Naona hizo sifa zitamponza muda sio mrefu
Sifa gani? Hivi kama mtu ana makosa ya kijinai kwanini umsamehe? Yaani mimi ningekuwa Dudubaya muda wote ningekuwa natembea na Mwanasheria ,wakija hao VICHWA MAJI atapambana na mwanasheria waseme wananikamata kwa kosa gani...inatakiwa wafuate PGOs zote.

Kuna Ulazima wa kumiliki "MIKWAJU" maana hao ViCHWA MAJI wakishapewa order huwa nao wanakurupuka tu na kukukamata bila kufuata procedures ,sasa wakijichanganya unawafanyia kama alivyowafanyia PETER ZAKARIA wale WAHUNI waliotaka kumteka.
 
Hii serikali inachosha sana akili ukijidai kuifuatilia kwa makini.

Katambi ulishaambiwa Duduz ana allergy na mashoga, kumkalisha meza moja na Anko T ni dharau kwake.
 
Waziri angebaki na mambo ya kisera. Kama Kuna uchunguzi police ndo waite watu. Na kama case ipo hatua za awali sana sio lazima kuujulisha umma umeita watu
Yaani wanafanya ujinga ujinga tu wakati tuna mambo mengi sana kama nchi ya kufanya ,maji hakuna ,barabara zinajengwa zaidi ya miaka minne haziishi ,utekaji kila kona ,badala ya kupambana kumaliza utekaji wao wanadeal na petty issues.
 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, ameliagiza Jeshi la Polisi kumtafuta na kumfikisha mbele ya vyombo vya sheria msanii Godfrey Tumaini maarufu Dudubaya, baada ya kushindwa kuitikia wito wa Wizara hiyo.

Akizungumza na wanahabari leo Ijumaa, Katambi amesema Dudubaya alikuwa ametakiwa kufika Wizara ya Mambo ya Ndani baada ya kutajwa katika tuhuma za makosa ya jinai, lakini licha ya kuitwa kwa mara ya pili, bado hakufika.

Soma Pia: Malu, pipytida, Dudu baya, Gigy money, Anko T, Noel na Mwijaku waitwa central station

Waziri amesema Dudubaya ameonekana kwenye mitandao ya kijamii akitoa kauli ambayo Waziri ameielezea kuwa ni kukaidi wito wa Serikali.
Hapo safi inaonekana hajui mdudu anaitwa serikali anajua dudubaya ndiyo kila kitu
 
Back
Top Bottom