Mkuu huyu Mwarabu akiondolewa kweli nitafurahi. Amenyanyasa sana wazawa, ole wako upotee njia upitie karibu na kambi yao, adhabu utakayopata utajuta kuzaliwa Tz. Huyu yuko karibu kabisa na Geti la serengeti ..Cleins gate kutokea Loliondo. Kwa kifupi yuko serengeti national park kwa mpaka wa Loliondo/Wasso.Huyo mwarabu ndo tunaambiwa huku JF kuwa hilo eneo lake ana mtandao binafsi wa simu?
Na hii ishu ndo iliondoa uhai wa Stan Katabaro?
pasco
CCM wanajikosha tu kwa wananchi,hiyo mikataba waliingia wenyewe na hao wawekezaji..Stan Katabaro my best Tanzanian investigative journalist...!!
Nilikuwa sikosi gazeti la Mfanyakazi kufuatilia Loliondo gate...!!
Siku moja na nafikiri inakaribia ambapo mchango wake wa kufichua mikataba ya kifisadi utakumbukwa na kuenziwa.
Mkuu hii kampuni imefaidi wanyama wa Tz kushinda hata serikali. Kwa kifupi wanyama wa serengeti pembezoni ni wa waoSijaelewa kuhus ugawaji wa vitalu, wanataka vigawiwe kwa wazawa tu au ?
au ndio anawabeep ili wamletee bahasha yake ?
Alimzima Dr. Mwaka[emoji12]Hivi Kigwangala ashafanikisha nini katika matamko yake yote akiwa Naibu Waziri?
Miganchi ya matamko,je hao wawekezaji wapo kihalali au kimagumashi?naogopa tusijekunyolewa bila maji!
Waziri wa Maliasili asili na utalii Mh. Kigwangala akiwa katika ziara yake wilayani Ngorongoro pamoja na kuagiza kuvifuta vibali vyote vya uwindaji nchi nzima ikiwamo vya kampuni ya ORTELLO BUSINESS CORPORATION (OBC) ya Loliondo, ameagiza kampuni hiyo ya MWARABU kujiandaa kurudi walikotokea, kwasababu hata kama wakibaki mchakato mpya wa ugawaji vitalu vya uwindaji utakapoanza hautawahusu.
Ikumbukwe kampuni ilipewa eneo hilo miaka ya 1990 kwa mkataba wa miaka 99.View attachment 618635
Sasa nimeelewa aisee,huyo Twiga lazima ahamie kwa mamdogo[emoji3]hakuna namna.Nimecheka sana Mkuu..
Twiga alipandia KIA Mkuu.
Hakika, Akiweza ntampongeza sanaKwahili namuunga mkono mh kigwangala
Captain unahasira!hadi unatetemeka! Kunywa maji bana.Acha tu turudi!! Kwanza hawa OBC waliteketeza kijiji kizima kwa madai kuwa eti hilo eneo la kijiji ambacho kimekuwepo hapo kwa makumi ya miaka kipo ndani ya eneo lao! Tena Kigwa angetupa ruhusa tukawaondoe wenyewe,wametuulia ndugu zetu wengi sana hawa hayawani! Mwarabu ni shetani kabisa!!!!
Mnapenda kupiga makofi na kupongeza bila ya kuangalia "impact" yake.....Kwa tamko hili lazima apongezwe sasa tuone kama utekelezaji wake utakamilika haraka iwezekanavyo.
Mnapenda kupiga makofi na kupongeza bila ya kuangalia "impact" yake.....
Rip stanley Katabaro wananchi wa kweli Bado wanakukumbu moja kati ya maandiko yako ulisema kuna kizazi kitakuja kufukua kaburi lako kuangalia ulikuwa na kichwa cha namna gani na pia watafukua kaburi la rais wa wakati huo ili kujua kichwa chake kilikuwa kinafananaje.Huyo mwarabu ndo tunaambiwa huku JF kuwa hilo eneo lake ana mtandao binafsi wa simu?
Na hii ishu ndo iliondoa uhai wa Stan Katabaro?
pasco