Waziri Kikwete azindua zoezi la kupandisha Mwenge wa uhuru mlima Kilimanjaro kama ilivyoelekezwa na rais Samia

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema Tanzania inapeleka mwenge wa uhuru juu ya mlima Kilimanjaro ili kuitangazia dunia kuwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni imara na pia itaendelea kulinda Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Aidha, Waziri Ridhiwani Kikwete amesema kuwa kwa mwaka huu 2024, Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameamuru mwenge wa uhuru upelekwe juu ya Mlima Kilimanjaro baada ya kuhitimisha mbio zake kwa siku 195.

Mhe. Ridhiwani amesema hayo Oktoba 15, 2024 katika hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro wakati wa hafla ya kupokea kikosi maalumu cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambacho kimepewa jukumu la kupeleka Mwenge wa Uhuru na Bendera ya Taifa la Tanzania kilele cha mlima Kilimanjaro.

Vile vile, Waziri Ridhiwani Kikwete amehamasisha vijana kuendelea kuenzi falsafa za mwenge wa uhuru ulioasisiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mwaka 1961.

Awali akizungumza, Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana amesema kupandishwa mwenge wa uhuru mlima Kilimanjaro mwaka huu 2024 kunaleta hamasa ya uzalendo kwa wananchi hususan wakati huu ambao Tanzania inaadhimisha miaka 60 ya uhuru na mafanikio ya Taifa.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Nurdin Babu amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia mwenge wa uhuru kupandishwa kwa mara nyingine katika kilele cha mlima Kilimanjaro.

Kwa upande wake, Kiongozi wa hicho Maalum, Luteni Kanali Khalid amemhakikishia Mhe. Waziri Ridhiwani Kikwete kuwa kikosi hicho kitafikisha kinaulinda na kuutunza Mwenge wa Uhuru na Bendera ya Taifa la Tanzania hadi katika kilele cha mlima Kilimanjaro.
IMG-20241016-WA0107.jpg
IMG-20241016-WA0105.jpg
IMG-20241016-WA0108.jpg
IMG-20241016-WA0109.jpg
IMG-20241016-WA0102.jpg
IMG-20241016-WA0103.jpg
IMG-20241016-WA0101.jpg
 
View attachment 3126238
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema Tanzania inapeleka mwenge wa uhuru juu ya mlima Kilimanjaro ili kuitangazia dunia kuwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni imara na pia itaendelea kulinda Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Aidha, Waziri Ridhiwani Kikwete amesema kuwa kwa mwaka huu 2024, Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameamuru mwenge wa uhuru upelekwe juu ya Mlima Kilimanjaro baada ya kuhitimisha mbio zake kwa siku 195.

Mhe. Ridhiwani amesema hayo Oktoba 15, 2024 katika hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro wakati wa hafla ya kupokea kikosi maalumu cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambacho kimepewa jukumu la kupeleka Mwenge wa Uhuru na Bendera ya Taifa la Tanzania kilele cha mlima Kilimanjaro.

Vile vile, Waziri Ridhiwani Kikwete amehamasisha vijana kuendelea kuenzi falsafa za mwenge wa uhuru ulioasisiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mwaka 1961.

Awali akizungumza, Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana amesema kupandishwa mwenge wa uhuru mlima Kilimanjaro mwaka huu 2024 kunaleta hamasa ya uzalendo kwa wananchi hususan wakati huu ambao Tanzania inaadhimisha miaka 60 ya uhuru na mafanikio ya Taifa.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Nurdin Babu amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia mwenge wa uhuru kupandishwa kwa mara nyingine katika kilele cha mlima Kilimanjaro.

Kwa upande wake, Kiongozi wa hicho Maalum, Luteni Kanali Khalid amemhakikishia Mhe. Waziri Ridhiwani Kikwete kuwa kikosi hicho kitafikisha kinaulinda na kuutunza Mwenge wa Uhuru na Bendera ya Taifa la Tanzania hadi katika kilele cha mlima Kilimanjaro.
View attachment 3126217View attachment 3126218View attachment 3126219View attachment 3126220View attachment 3126221View attachment 3126222View attachment 3126223
Huyu kijana anakua groomed vizuri na CCM baada ya miaka 10 utaandika Raisi kikwete amepandisha mwenge mlima kilimanjaro.
 
Back
Top Bottom