Waziri Kikwete: Fursa za ajira kwa vijana nje ya nchi kipaumbele cha Serikali ya Rais Samia

Waziri Kikwete: Fursa za ajira kwa vijana nje ya nchi kipaumbele cha Serikali ya Rais Samia

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2019
Posts
377
Reaction score
435
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeendelea kufungua fursa zaidi za ajira kwa watanzania nje ya nchi.

Aidha, Mhe. Ridhiwani amesema serikali inatekeleza mpango wa kuwaandaa vijana kuwa na ujuzi stahiki unao wawezesha kumudu ushindani kwenye soko la ajira la kimataifa sambamba na kufanya kazi zenye tija.

Mhe. Ridhiwani amebainisha hayo leo Novemba 28, 2024 Jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya kuwaaga Vijana wa Kitanzania wanaoenda kufanya kazi nchini Saudi Arabia.

Waziri Ridhiwani Kikwete, amebainisha kuwa Serikali imesaini makubaliano ya ushirikiano katika masuala ya ajira na nchi ya Falme za Kiarabu (UAE), Saudi Arabia, Iran na Qatar kwa lengo la kuongeza fursa zaajira kwa watanzania kwenye nchi hizo.

"Serikali imeweka malengo mahususi ya kuongeza fursa za ajira kwa Watanzania kutoka 556,065 kwa mwaka 2022 hadi 1,000,000 ifikapo mwaka 2028," amesema

Vile vile, amesema serikali itaendelea kulinda haki na wajibu wa wafanyakazi wa kitanzania nje ya nchi kwa kuhakikisha wanafanya kazi za staha ili kuongeza idadi ya watanzania wanaofanya kazi za kitaaluma.

Sambamba na hayo, ametoa rai kwa Wauguzi wanao kwenda kufanya kazi nchini Saudi Arabia, kufanya kazi kwa uadilifu na uaminifu ili kuaminika na kuiletea heshima nchi yao Tanzania.
 

Attachments

  • FB_IMG_1732821000985.jpg
    FB_IMG_1732821000985.jpg
    37.8 KB · Views: 5
  • FB_IMG_1732821020408.jpg
    FB_IMG_1732821020408.jpg
    76.1 KB · Views: 9
  • FB_IMG_1732821027292.jpg
    FB_IMG_1732821027292.jpg
    69.9 KB · Views: 4
  • FB_IMG_1732821187093.jpg
    FB_IMG_1732821187093.jpg
    109.5 KB · Views: 5
Kuna mtu anaweza amini kabisa wizara ya afya huko Saudi Arabia (nchi ya dunia ya kwanza) inaweza ajiri nurses from third world, katika dunia ya leo.

Labda kama habari ina gap, vinginevyo kwa jinsi hao watu wanavyo train nurses leo sidhani kama wanaweza waokota from third world bila ya kuwapa training kwanza.

Unless liwe taifa la hovyo na alijali quality ya huduma ya afya vinginevyo strategically utataka watu wenye matching competent skills.

Labda aseme wanaenda kuwa care workers huko Saudi Arabia na kuna mipango sahihi ya ulinzi wao (I doubt).

Ukitafuta documentaries za mambo wanayopitia hawa madada kwa baadhi ya hao wenyeji wanaowapokea (sio wote) huwezi mshauri mtu ampeleke mtoto wake miaka 800.

Yaani kama ni deals huko serikalini bora ukazipige sehemu zingine, lakini kushadidia kupeleka watoto wa maskini hizo nchi ni hatari wakifikia kwa wenyeji ambao hawana utu.
 
Back
Top Bottom