Waziri Kombo amuaga Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Canada baada ya kumaliza ziara ya kikazi nchini

Waziri Kombo amuaga Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Canada baada ya kumaliza ziara ya kikazi nchini

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,773
Reaction score
1,174
Waziri Kombo amuaga Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Canada baada ya kumaliza ziara ya kikazi nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb), ameagana na Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Canada Mhe. Randeep Sarai katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam baada ya kukamilisha ziara yake ya kikazi ya siku tatu nchini.

Ziara hiyo iliyoanza tarehe 20 hadi 23 Julai, 2025 ililenga kuimarisha ushirikiano katika diplomasia ya Uchumi husani katika maeneo ya biashara na uwekezaji, ili kuleta maendeleo endelevu kwa manufaa ya wananchi wa pande zote mbili.

Viongozi hao wamekubaliana kuendelea kuibua maeneo ya ushirikiano katika sekta za kiuchumi zitakazowezesha kukuza ubunifu, kuongeza ajira kwa vijana na wanawake, na kuhamasisha ukuaji wa maendeleo ya jamii, hususani vijijini.

Awali, Mhe. Kombo aliishukuru Serikali ya Canada kwa ushirikiano wa muda mrefu na Tanzania, kwa kuchangia utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya Mwaka 2020-2025, iliyolenga kujenga uchumi imara na shindani, kuboresha maisha ya wananchi wote, kuimarisha utawala bora na kukuza uchumi unaochochea ukuaji wa viwanda na uwekezaji.

Mhe. Randeep Sarai alieleza dhamira ya Serikali ya Canada ya kuendelea kuwa mshirika wa karibu wa Tanzania kwa kusaidia maeneo yenye uhitaji mkubwa kama vile uwezeshaji wa vijana na wanawake, uwekezaji wa kimkakati katika sekta za madini, uvuvi, nishati safi, elimu, mafunzo ya ukuzaji ujuzi, pamoja na kuimarisha misingi ya amani na usalama katika kuleta maendeleo ya watu wa nchi zote mbili.
 

Attachments

  • IMG-20250724-WA0080.jpg
    IMG-20250724-WA0080.jpg
    592.7 KB · Views: 32
  • IMG-20250724-WA0060.jpg
    IMG-20250724-WA0060.jpg
    388.5 KB · Views: 35
  • IMG-20250724-WA0049.jpg
    IMG-20250724-WA0049.jpg
    551 KB · Views: 36
  • IMG-20250724-WA0059.jpg
    IMG-20250724-WA0059.jpg
    374.7 KB · Views: 36
  • IMG-20250724-WA0042.jpg
    IMG-20250724-WA0042.jpg
    375.6 KB · Views: 32
  • IMG-20250724-WA0064.jpg
    IMG-20250724-WA0064.jpg
    366 KB · Views: 34
  • IMG-20250724-WA0071.jpg
    IMG-20250724-WA0071.jpg
    363.2 KB · Views: 33
  • IMG-20250724-WA0063.jpg
    IMG-20250724-WA0063.jpg
    354.2 KB · Views: 36
  • IMG-20250724-WA0079.jpg
    IMG-20250724-WA0079.jpg
    601 KB · Views: 33
  • IMG-20250724-WA0072.jpg
    IMG-20250724-WA0072.jpg
    499.3 KB · Views: 38
  • IMG-20250724-WA0078.jpg
    IMG-20250724-WA0078.jpg
    486 KB · Views: 30
  • IMG-20250724-WA0077.jpg
    IMG-20250724-WA0077.jpg
    514 KB · Views: 34
  • IMG-20250724-WA0067.jpg
    IMG-20250724-WA0067.jpg
    488 KB · Views: 27
  • IMG-20250724-WA0069.jpg
    IMG-20250724-WA0069.jpg
    321 KB · Views: 34
  • IMG-20250724-WA0061.jpg
    IMG-20250724-WA0061.jpg
    414.4 KB · Views: 36
  • IMG-20250724-WA0070.jpg
    IMG-20250724-WA0070.jpg
    316 KB · Views: 32
  • IMG-20250724-WA0073.jpg
    IMG-20250724-WA0073.jpg
    410.7 KB · Views: 34
  • IMG-20250724-WA0075.jpg
    IMG-20250724-WA0075.jpg
    442.4 KB · Views: 35
  • IMG-20250724-WA0065.jpg
    IMG-20250724-WA0065.jpg
    322.8 KB · Views: 31
Back
Top Bottom