Waziri Kombo apokea hati za utambulisho kutoka kwa Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini

Habari za Zanzibar

New Member
Joined
Dec 18, 2024
Posts
4
Reaction score
2
WAZIRI KOMBO APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO KUTOKA KWA MWAKILISHI MKAZI WA UMOJA WA MATAIFA NCHINI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thatib Kombo amepokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa Bi. Susan Namondo katika Ofisi Ndogo za Wizara, jijini Dar es Salaam Desemba 23, 2024.

Akipokea nakala hizo Waziri Kombo amempongeza Bi Nomondo kwa uteuzi aliuopata na amemuahidi kumpa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yake kwa kipindi atakachokuwa nchini kuuwakilisha Umoja wa Mataifa.

Aidha, Mhe. Kombo ameushukuru Umoja wa Mataifa kwa mchango wake katika kuiwezesha Tanzania kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu na Ajenda ya Afrika ya mwaka 2063 kupitia Mfumo wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNSDCF) wa mwaka 2022-2027.

Kwa upande wake Mwakilishi huyo Mkazi wa Umoja wa Mataifa ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa mapokezzi mazuri na amehaidi kuendeleza ushirikiano na Tanzania ili kuwezesha utekelezaji wenye matokeo mazuri wa malengo ya maendeleo endelevu nchini Tanzania.

IMG-20241224-WA0138.jpg
IMG-20241224-WA0134.jpg
 
IMG-20241224-WA0136.jpg

IMG-20241224-WA0140.jpg
IMG-20241224-WA0124.jpg
IMG-20241224-WA0122.jpg
IMG-20241224-WA0132.jpg
 
Attachments

  • IMG-20241224-WA0130.jpg
    IMG-20241224-WA0130.jpg
    424.9 KB · Views: 3
  • IMG-20241224-WA0128.jpg
    IMG-20241224-WA0128.jpg
    474.5 KB · Views: 4
  • IMG-20241224-WA0126.jpg
    IMG-20241224-WA0126.jpg
    496.1 KB · Views: 4
  • IMG-20241224-WA0120.jpg
    IMG-20241224-WA0120.jpg
    516.7 KB · Views: 4
Back
Top Bottom