DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Bunge la Umoja wa Ulaya (EU) limepitisha azimio linalopendekeza kusitishwa kwa ufadhili wa fedha za maendeleo kwa Tanzania, likieleza wasiwasi juu ya mazingira ya kisiasa na ukiukaji wa haki za binadamu ulioripotiwa baada ya uchaguzi wa Oktoba 2025.
Uhusiano wa Tanzania na Umoja wa Ulaya umedumu kwa miongo kadhaa, ukijengwa juu ya misaada, mikopo nafuu, ushirikiano wa kibiashara na miradi ya mageuzi ya kiuchumi na kijamii. EU ilikuwa imepanga kutoa zaidi ya Euro milioni 150, sawa na zaidi ya Sh400 bilioni, kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya Tanzania mwaka 2026.
Serikali kupitia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo, imesema inafuatilia kwa karibu suala hilo kupitia kwa Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji lilipo bunge hilo, Jestas Nyamanga. Waziri Kombo amesema serikali itatoa kauli rasmi baada ya kupokea taarifa kamili ya matokeo ya mjadala huo kutoka kwa Balozi Nyamanga.
“Tunafuatilia majadiliano hayo na Balozi Jestas Nyamanga yuko huko kama mwalikwa. EU wana haki ya kujadili chochote kwa sababu ni fedha zao, ni haki yao. Balozi wetu atatuleta ripoti kisha Serikali tutatoa taarifa,” amesema Balozi Kombo katika taarifa iliyochapishwa na gazeti Mwananchi.
Akizungumzia athari za kusitishwa kwa fedha hizo, Waziri Kombo amesema Tanzania haitakabiliwa na njaa wala kusimama kwa shughuli za maendeleo, kwani ina bajeti na vyanzo vyake vingine vya mapato. Amesema ni muhimu wananchi kufuatilia kiasi halisi kinachotarajiwa kukosekana na kukilinganisha na bajeti ya Taifa kwa mwaka 2025/26 ambayo ni Sh56.49 trilioni.
“Fuatilia huko mitandaoni ujue ni kiasi gani cha fedha tutakikosa…Sisi Watanzania hatutakufa kwa kukosa fedha hizo. Angalia wanatoa kiasi gani, kaangalie na bajeti yetu kwa mwaka, kisha fanya hesabu ni asilimia ngapi ya bajeti yetu,” amesema Balozi Kombo.
Azimio la EU limeeleza kusikitishwa na matukio ya vifo vilivyotokea kabla, siku ya uchaguzi na baada yake, pamoja na taarifa za ukiukwaji wa haki za binadamu, ikiwemo utekaji, mauaji ya wakosoaji wa serikali na udhibiti dhidi ya vyombo vya habari.
Pia Soma: Rasmi, Bunge la Ulaya lapiga kura zote 539 za NDIYO kuzuia misaada Tanzania, wahusika wa kadhia ya Oktoba 29 kuwekewa vikwazo