PostGE2025 Waziri Kombo: Tanzania hatutakufa kwa kukosa fedha za EU

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Sema wazee wale watanganyika wenzetu waliopo ngazi za juu kwenye vyombo vya usalama ni sana.

Sijui wote wametoka kwenye backgrounds za kimaskini ndio maana wamepumbazwa kirahisi na hizo rushwa za mabilioni?

Hii serikali ya wazanzibari haikutakiwa kutuongoza mpaka dk hii kwa maslahi mapana ya taifa la sasa na lijalo.
 
Sema wazee wale watanganyika wenzetu waliopo ngazi za juu kwenye vyombo vya usalama ni

Yaani umeongea ukweli ingawa umetumia Lugha nzinto
 
Sema wazee wale watanganyika wenzetu waliopo ngazi za juu kwenye vyombo vya usalama ni

Sijui wote wametoka kwenye backgrounds za kimaskini ndio maana wamepumbazwa kirahisi na hizo rushwa za mabilioni?

Hii serikali ya wazanzibari haikutakiwa kutuongoza mpaka dk hii kwa maslahi mapana ya taifa la sasa na lijalo.
Wale siku zao zinahesabika. Ni suala la muda. Hivyo vipande vya fedha walivyokubali na kuacha damu za Watanganyika zimwagike vitawatokea puani.
 
Hawajui hawa wakianza kukubana wanaenda hatua kwa hatua, na kila hatua ina athari pana za kiuchumi na kijamii.

Leo wamefuta misaada ya kwenye bajeti, ukiendelea kuleta kiburi, wanazuia kufanya biashara na wewe. Hakuna utalii wala kupeleka bidhaa zako kwao.

Baadae ukiendelea na kiburi, wanakuja kuwawekea vikwazo viongozi binafsi na familia zao pamoja na kufungia account na kukamata mali zao.

Baadae haukopesheki au utakopa kwa riba kubwa sana kwa sababu risk ya kukukopesha imekuwa kubwa.

Hatua kwa hatua.

Wanadhani watakimbilia China na Uarabuni ila wanajidanganya. Hata hao hawatoi pesa iende kupotea bure.
 
Bunge la Umoja wa Ulaya (EU) limepitisha azimio linalopendekeza kusitishwa kwa ufadhili wa fedha za maendeleo kwa Tanzania, likieleza wasiwasi juu ya mazingira ya kisiasa na ukiukaji wa haki za binadamu ulioripotiwa baada ya uchaguzi wa Oktoba 2025.

Uhusiano wa Tanzania na Umoja wa Ulaya umedumu kwa miongo kadhaa, ukijengwa juu ya misaada, mikopo nafuu, ushirikiano wa kibiashara na miradi ya mageuzi ya kiuchumi na kijamii. EU ilikuwa imepanga kutoa zaidi ya Euro milioni 150, sawa na zaidi ya Sh400 bilioni, kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya Tanzania mwaka 2026.

Serikali kupitia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo, imesema inafuatilia kwa karibu suala hilo kupitia kwa Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji lilipo bunge hilo, Jestas Nyamanga. Waziri Kombo amesema serikali itatoa kauli rasmi baada ya kupokea taarifa kamili ya matokeo ya mjadala huo kutoka kwa Balozi Nyamanga.

“Tunafuatilia majadiliano hayo na Balozi Jestas Nyamanga yuko huko kama mwalikwa. EU wana haki ya kujadili chochote kwa sababu ni fedha zao, ni haki yao. Balozi wetu atatuleta ripoti kisha Serikali tutatoa taarifa,” amesema Balozi Kombo katika taarifa iliyochapishwa na gazeti Mwananchi.

Akizungumzia athari za kusitishwa kwa fedha hizo, Waziri Kombo amesema Tanzania haitakabiliwa na njaa wala kusimama kwa shughuli za maendeleo, kwani ina bajeti na vyanzo vyake vingine vya mapato. Amesema ni muhimu wananchi kufuatilia kiasi halisi kinachotarajiwa kukosekana na kukilinganisha na bajeti ya Taifa kwa mwaka 2025/26 ambayo ni Sh56.49 trilioni.

“Fuatilia huko mitandaoni ujue ni kiasi gani cha fedha tutakikosa…Sisi Watanzania hatutakufa kwa kukosa fedha hizo. Angalia wanatoa kiasi gani, kaangalie na bajeti yetu kwa mwaka, kisha fanya hesabu ni asilimia ngapi ya bajeti yetu,” amesema Balozi Kombo.

Azimio la EU limeeleza kusikitishwa na matukio ya vifo vilivyotokea kabla, siku ya uchaguzi na baada yake, pamoja na taarifa za ukiukwaji wa haki za binadamu, ikiwemo utekaji, mauaji ya wakosoaji wa serikali na udhibiti dhidi ya vyombo vya habari.

Pia Soma: Rasmi, Bunge la Ulaya lapiga kura zote 539 za NDIYO kuzuia misaada Tanzania, wahusika wa kadhia ya Oktoba 29 kuwekewa vikwazo

CHAI
 
Wenzetu wanzanzibari wameshashiba ninamwelewa. Lakini wewe boda boda maisha yatakuwa magumu
 
Bora wanyimwe tu hzo pesa mwananchi mim hazinisaidii chochote, balabala ni mbovu miundo mbinu hairidhishi na pesa wanakopa wanajirimbikizia wao.

Wanyimwe tu na deni la taifa lisimame, wananch tupumue.
Japokuwa vitu baadh tutahangaika au vikawa adim
 
Hiyo bajeti ya Tanzania ya dola bilioni 22 kwa mwaka huu inajumuisha msaada w EU, misaada na mikopo kutoka mataifa wanachama wa EU. Sasa ukinyimwa msaada wa EU, nchi wanachama wa EU, ukanyimwa na mikopo, bado utasema hakuna athari. Zamia ndani ya miaka 2 amekopazaidiya trilioni 50. Hii ni wastani wa kiasi cha trilioni 25 kwa mwaka. Halafu bajeti yako ni trilioni 57. Ina maana nusu ya bajeti ni mikopo. Sasa ukinyimwa hiyo nusu ya bajeti, mambo yatabakia kawaida?
Hapo na wananchi wanaamua kutoklipa kodi na hakuna wa kumfanya kitu.

Naogopa sana hali ya hii nchi. Mungu atuepusha tusikifikie hali ngumu hivyo.
 
Bunge la Umoja wa Ulaya (EU) limepitisha azimio linalopendekeza kusitishwa kwa ufadhili wa fedha za maendeleo kwa Tanzania, likieleza wasiwasi juu ya mazingira ya kisiasa na ukiukaji wa haki za binadamu ulioripotiwa baada ya uchaguzi wa Oktoba 2025.

Uhusiano wa Tanzania na Umoja wa Ulaya umedumu kwa miongo kadhaa, ukijengwa juu ya misaada, mikopo nafuu, ushirikiano wa kibiashara na miradi ya mageuzi ya kiuchumi na kijamii. EU ilikuwa imepanga kutoa zaidi ya Euro milioni 150, sawa na zaidi ya Sh400 bilioni, kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya Tanzania mwaka 2026.

Serikali kupitia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo, imesema inafuatilia kwa karibu suala hilo kupitia kwa Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji lilipo bunge hilo, Jestas Nyamanga. Waziri Kombo amesema serikali itatoa kauli rasmi baada ya kupokea taarifa kamili ya matokeo ya mjadala huo kutoka kwa Balozi Nyamanga.

“Tunafuatilia majadiliano hayo na Balozi Jestas Nyamanga yuko huko kama mwalikwa. EU wana haki ya kujadili chochote kwa sababu ni fedha zao, ni haki yao. Balozi wetu atatuleta ripoti kisha Serikali tutatoa taarifa,” amesema Balozi Kombo katika taarifa iliyochapishwa na gazeti Mwananchi.

Akizungumzia athari za kusitishwa kwa fedha hizo, Waziri Kombo amesema Tanzania haitakabiliwa na njaa wala kusimama kwa shughuli za maendeleo, kwani ina bajeti na vyanzo vyake vingine vya mapato. Amesema ni muhimu wananchi kufuatilia kiasi halisi kinachotarajiwa kukosekana na kukilinganisha na bajeti ya Taifa kwa mwaka 2025/26 ambayo ni Sh56.49 trilioni.

“Fuatilia huko mitandaoni ujue ni kiasi gani cha fedha tutakikosa…Sisi Watanzania hatutakufa kwa kukosa fedha hizo. Angalia wanatoa kiasi gani, kaangalie na bajeti yetu kwa mwaka, kisha fanya hesabu ni asilimia ngapi ya bajeti yetu,” amesema Balozi Kombo.

Azimio la EU limeeleza kusikitishwa na matukio ya vifo vilivyotokea kabla, siku ya uchaguzi na baada yake, pamoja na taarifa za ukiukwaji wa haki za binadamu, ikiwemo utekaji, mauaji ya wakosoaji wa serikali na udhibiti dhidi ya vyombo vya habari.

Pia Soma: Rasmi, Bunge la Ulaya lapiga kura zote 539 za NDIYO kuzuia misaada Tanzania, wahusika wa kadhia ya Oktoba 29 kuwekewa vikwazo

Huyu jamaa ukimuangalia kama alishawahi kupata Shida ya afya ya akili utotoni ,anamuaibisha Mzee Thabit Kombo(Mpigania uhuru wa Zanzibar/Tanganyika) baba yake au babu yake.
 
Serikali yetu inapaswa kuwa sikivu sana na kujitahidi kuchukua hadhari mapema badala ya kusubiria matokeo na kutumia njia za kushindana. Haipo haja ya kushindana na maazimio yaliyotolewa ila ipo haja ya kujipima kwa hoja zetu binafsi na kujirekebisha.
 
Back
Top Bottom