Waziri Lugola: Wizara haihusiki na kupotea kwa Mwandishi wa Kampuni ya Mwananchi Communication Limited, Azory Gwanda

Waziri Lugola: Wizara haihusiki na kupotea kwa Mwandishi wa Kampuni ya Mwananchi Communication Limited, Azory Gwanda

kuna watu ni wapuuzi sana ila wamepewa dhamana kubwa ili hali hawajielewi.

huwez kujibu swali la msingi kipumbavu hivi
 
Waandishi wa habari nao wanamatatizo kwa kweli, sasa unamuuliza swali gani mtu ambaye hana hata zaidi ya wiki ofisini, kwa mambo ambayo yametokea zaidi ya mwaka katika wizara? Hata wakipewa majibu ya aina hii wanastahili kabisa.

Mwandishi alitakiwa kuuliza, kuhusiana na mikakati yake kwa baadhi ya maswala ambayo hayakupatiwa ufumbuzi muda mrefu..
 
Kwanza jifunze kuandika majina ya watu.

Pili, serikali inawajibu ya kuwalinda na kuwahakikishia usalama raia wake wote walio ndani na nje ya mipaka ya nchi. Inawajibu kwa raia wake wote, wanaotangazwa na wasiotangazwa. Kama haitekelezi jukumu hili, wananchi wanakila sababu ya kuishitaki serikali yao.
Sio hoja ya mcng kujua kuandika majina ya watu,ebu niambie ni lini wizara iliwajibika kwa kupotea kwa mtu?Nilikua na ndugu yangu alikua anaondoka tu nyumbani na haieleweki kaenda wapi.Kilichokua kinafanyika ni kutoa tu taarifa kuna ndugu yetu kapotea yuko hivi na hivi,hakuna cha kusema polisi wakamtafute wala nn.na iko hivo.Watu wengi wakipotea tumeona matangazo yakibandikwa kwa ajili ya kuwatafuta.Ingekua ni habari nyingine kama mngesema katekwa,lkn bado hoja itakuja huyo alikua anafanya kitu gani cha kusababisha atekwe? Nini uhusiano wake na hao waliomteka.
 
Majibu kama hayo niyakawaida sana kwa matukio kma hayo kwani uhalisia wa jambo unafahmika

Binafsi huwa sipendi majibu ambayo yanakuwa edited...tuletewe clip humu ili sisi wenyewe tuchambue hoja au majibu yake
 
wanahabari naimani hakuna cha kumgezea kwaiyo gwanda kamtafuteni mgodini
 
Inawezekana ikawa kweli anavyosema Waziri kwamba wizara haihusiki na kupotea kwake,lakini asisahau kuwa wizara yake inahusika na kupatikana kwake kwani wana jukumu la kuhakikisha uslama wa raia na mali zao ilibidi awaeleze waandishi kulingana na taarifa zilizopo wizarani jeshi la polisi mpaka limefanya jitahada gani kuhakikisha huyo mwandishi anapatikana?
 
Duh sasa jeshi la polisi kazi yake nini yaani bora mwigulu aisee
 
Huyu mzee bado yuko ofisini kwa majibu haya? Na jiwe hajachukua hatua? Inasikitisha, usalama wetu upo mashakani.
 
Du ! Hii Kali, Majibu Rahisi Kwa Maswali Magumu. Maisha Gani Magumu Aliyokuwa Nayo Mwandishi Mpaka Atoweke Kimya Kwenda Kutafuta Maisha Kwingine ?
 
Du ! Hii Kali, Majibu Rahisi Kwa Maswali Magumu. Maisha Gani Magumu Aliyokuwa Nayo Mwandishi Mpaka Atoweke Kimya Kwenda Kutafuta Maisha Kwingine ?
 
MITI FUMBENI MACHO NA MASIKIO MSIJE MKAONA YA SIRINI, MCHANGA FUTA NYAYO ZA WATENDAO GIZANI...
 
Back
Top Bottom