Waziri Lukuvi apiga marufuku madalali kulipwa posho ya mwezi mmoja na wapangaji. Asema ni ujambazi

Waziri Lukuvi apiga marufuku madalali kulipwa posho ya mwezi mmoja na wapangaji. Asema ni ujambazi

Hajasema wasilipwe, ila ni marufuku mpangaji kutoa hiyo kodi ya mwezi mmoja isipokuwa aliyempa kazi ya kutafuta mpangaji ndio amlipe dalali so wenye nyumba ndio wanatakiwa wawalipe madalili wao and obvious kodi itapanda kwa hiyo ni mule mule tu
 
Wanaopanga hawana shida kulipa maana si kazi rahisi kupata nyumba.

Sasa kama ni hivo dalali si anaweza kuongea na mwenye nyumba bei iwe juu ,kitu kile kile
Kuna umuhimu wa kurudisha Rent Restriction Act ili isimamie viwango vya Kodi za upangaji wa nyumba. Madalali wanatabia ya kupandisha Bei ya nyumba ili wavune wasipopanda.
 
Waziri wa Ardhi, William Lukuvi amepiga marufuku Madalali kuwadai Wapangaji Fedha ya Mwezi Mmoja, akiita kitendo hicho kuwa ni ujambazi.

Amesema, "Kuna baadhi ya Madalali wanapangisha nyumba halafu wanachukua kwa Wapangaji Kodi ya mwezi. Hawa wanaochukua pesa za wapangaji waache mchezo huo kwasababu ni wizi wa mchana kabisa. Wewe umeajiriwa na mwenye nyumba, yeye lazima akulipe wewe"

View attachment 2011900
Serkali inakaba hata penati? Haifahamu kuwa udalali ni ajira na anayehitaji huduma ndiye mlipaji?
 
Sikujua Kumbe bado nchi iko gizani halafu bado wanasema Jiwe alikusanya kodi hivi kodi kiasi gani imepotea kwa hawa watu wanaofanya udalali??

Kuna haja ya kuwa na website za rental houses mtu akitaka anaingia na kulipa akiridhika hij ni rahisi na salama na kila kitu kiko traced!

Happ kodi itaonekana na kukatwa kodi na hizo commision za udalali zitakatwa kodi pia
... kwa utaratibu huo badala ya dalali kuchukua kodi ya mwezi maana yake itakuwa formalized na TRA watachukua 18%! Hii nchi haijawahi kuwa na huruma kwa mnyonge! Hadi Waziri ameongea hivyo kuna something "fishy" below the carpet; hajaongea kwa bahati mbaya au eti anawahurumia sana wapangaji! Most likely kuna ka-mswada kanaandaliwa chanzo kingine cha mapato! CCM?
 
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi, amewapiga marufuku madalali wa nyumba wanaochukua kodi ya mwezi mmoja kwa wapangaji na badala yake pesa hizo walipwe na wenye nyumba.

Kauli hiyo ameitoa Novemba 15, 2021, mkoani Iringa na kusema kwamba kitendo cha kuchukua pesa kwa mtu anayepanga ni wizi wa waziwazi.

"Tunawashangaa hawa majambazi wanaochukua kodi ya mwezi kwa mpangaji, hawa madalali wanaochukua pesa kwa mpangakji waache mchezo huo kwa sababu ni wizi wa mchana kabisa, mwenye nyumba lazima akulipe wewe," ameeleza Waziri Lukuvi
 
Good for us 'wapangaji..

Hasara kwa maza & faza's house.

Madalali na msikie 😁👌

Ije na kwa wale wenye nyumba wanaotulipisha pesa za rangi, wengine sisi somo la usafi tulifaulu kiasi kuta zenu wenye nyumba hatuchafui lakini mnakaza bongo kuwa tuwalipe.
 
Kwahiyo wakilipwa na mwenye nyumba unakuwa ni wizi wa usiku au anamaanisha nini!
Baadhi ya wenye nyumba uwaambia madalali wawatafutie wapangaji and sometimes dalali mwenyewe anatafuta nyumba ambazo zinahitaji mpangaji...

Mwenye nyumba yake awe responsible na kumlipa dalali kwa kumletea mteja.
 
Nadhani anayetoa kazi ndio alipie.

Kama mpangaji kamuomba dalali amtafutie nyumba, mpangaji ndio alipie huduma ya kutafutiwa nyumba.

Kama mwenye nyumba kamuomba dalali amtafutie mpangaji, mwenye nyumba alipie hiyo huduma ya kutafutiwa mpanganji.

Simple.

Muhimu kiwekwe kiwango cha kiasi gani au asilimia ngapi itakuwa fee ya kufanya hiyo kazi. Hii ya mwezi mmoja ni kubwa sana.
 
Back
Top Bottom