Waziri Lukuvi awataka wamiliki wa ardhi kujenga kwa kufuata sheria

Waziri Lukuvi awataka wamiliki wa ardhi kujenga kwa kufuata sheria

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amewataka wamiliki wa ardhi wanaotaka kujenga kuhakikisha wanafuata sheria na taratibu zote wakati wa kufanya ujenzi.

Waziri Lukuvi alisema hayo mwishoni mwa wiki hii katika ofisi yake ya ardhi ya mkoani Dar es Salaam na Pwani. Alisema sheria inamtaka mmiliki wa ardhi anayetaka kufanya ujenzi kupata kibali kutoka halmashauri za miji, manispaa na majiji na kuongeza kuwa sheria hiyo inakataza kufanya ujenzi bila kibali kutoka mamlaka husika.

”Naelekeza watendaji wote wawe wa ardhi au mipango miji kuhakikisha sheria zinafuatwa kwa kudhibiti ujenzi holela na sheria inakataza kabisa kujenga bila kupata kibali kutoka katika mamlaka husika” alisema Lukuvi.

Kwa mujibu wa Lukuvi, zoezi la urasimishaji linaloendelea sasa maeneo mbalimbali ni kwa majengo yaliyojengwa tu na kusisitiza kuwa zoezi la urasimishaji isiwe sehemu endelevu ya kuvunja sheria na kubainisha kuwa angetaka kuona maeneo yote ya miji hasa Dodoma yanajengwa kwa kupatiwa kibali.

Aliwataka wataalamu wote hasa waliopo halmashauri katika yale maeneo yaliyotangazwa kimji kwa mujibu wa sheria wananchi wake waelimishwe kujenga katika viwanja vilivyopangwa na kupimwa na wawe wamepatiwa vibali na mamlaka za halmashauri husika.

”hatua zichukuliwe kuzuia jambo hili tunataka miji endelevu ambayo wananchi wanaishi na kujenga kwa mujibu wa sheria” alisema Lukuvi.

1609748113696.png
 
E4653552-55B6-409A-AD56-10C7FFA6FC8B.jpeg
83F5D2CD-2DE2-446D-8E9C-9CDB60033009.jpeg

Baada ya kuongea na kupiga kelele juu ya ujenzi holela ndani ya Tanzania, naona sasa akili zimemuingia lukuvi na ameamua kuja na hili. Napenda kumwambia hongera sio mbaya ila apitie na ule uzi nilioandika humu ili aweze kupata njia zaidi za kupambana na makazi holela.

Nashauri apitie na huu uzi hapa👇
 
Baada ya kuongea na kupiga kelele juu ya ujenzi holela ndani ya Tanzania, Naona sasa akili zimemuingia lukuvi na ameamua kuja na hili. Napenda kumwambia hongera
Hii wala siyo mbinu ya kuzuia majenzi holela. Huu ni mkakati mmojawapo wa kufikisha trillion 2 kwa mwezi.

Hivi vibali tangu vianze kutolewa ni mwaka wa tatu huu lkn bado ujenzi unafanyika holela tu.

Kinachotafutwa hapa ni hela ya vibali tu.
 
Serikali ibomoe makazi holela yote nchini kisha tuanze upya kwa kufuata sheria na kulipia vibali na kodi ya Ardhi kufikia lengo tr. 2 kila mwezi. Itasaidia sana taifa kuingia kwenye uchumi wa kati juu come 2025.
 
Umeniwahi!
 
Muweke sehemu za wazi ili wajukuu wetu wapate pa kucheza, tupate sehemu za kutembea zenye joto wa asili hata tukiwa mijini pia inasaidia mazoezi.
 
Siku serikali ikisema inakopa kwa ajili ya kuipima ardhi ya nchi nzima basi itakuwa vizuri sana.

kuna mwaka huyu huyu Lukuvi alisema watakopa world bank ili kuipima ardhi yote nchi nzima, sijui ule mpango uliishia wapi!

Kuchelewa kuipima ardhi ndiyo husababisha ujenzi holela
 
Hata kama suala la kibajeti/ kifedha ni changamoto wanaweza wakazielekeza serikali za mitaa kusimamia watu wajenge vizuri na kwa mpangilio na bado tukafanikiwa. Hii nchi solution zipo tena nyingi sana. Hatutakagi tu kuzitumia
 
Serikali ibomoe makazi holela yote nchini kisha tuanze upya kwa kufuata sheria na kulipia vibali na kodi ya Ardhi kufikia lengo tr. 2 kila mwezi. Itasaidia sana taifa kuingia kwenye uchumi wa kati juu come 2025.
Hili lazima siku moja tutakuja kulifanya tu. Ujenzi holela umezidi kwa kweli.
 
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amewataka wamiliki wa ardhi wanaotaka kujenga kuhakikisha wanafuata sheria na taratibu zote wakati wa kufanya ujenzi.

Waziri Lukuvi alisema hayo mwishoni mwa wiki hii katika ofisi yake ya ardhi ya mkoani Dar es Salaam na Pwani. Alisema sheria inamtaka mmiliki wa ardhi anayetaka kufanya ujenzi kupata kibali kutoka halmashauri za miji, manispaa na majiji na kuongeza kuwa sheria hiyo inakataza kufanya ujenzi bila kibali kutoka mamlaka husika.

”Naelekeza watendaji wote wawe wa ardhi au mipango miji kuhakikisha sheria zinafuatwa kwa kudhibiti ujenzi holela na sheria inakataza kabisa kujenga bila kupata kibali kutoka katika mamlaka husika” alisema Lukuvi.

Kwa mujibu wa Lukuvi, zoezi la urasimishaji linaloendelea sasa maeneo mbalimbali ni kwa majengo yaliyojengwa tu na kusisitiza kuwa zoezi la urasimishaji isiwe sehemu endelevu ya kuvunja sheria na kubainisha kuwa angetaka kuona maeneo yote ya miji hasa Dodoma yanajengwa kwa kupatiwa kibali.

Aliwataka wataalamu wote hasa waliopo halmashauri katika yale maeneo yaliyotangazwa kimji kwa mujibu wa sheria wananchi wake waelimishwe kujenga katika viwanja vilivyopangwa na kupimwa na wawe wamepatiwa vibali na mamlaka za halmashauri husika.

”hatua zichukuliwe kuzuia jambo hili tunataka miji endelevu ambayo wananchi wanaishi na kujenga kwa mujibu wa sheria” alisema Lukuvi.

Shida vibali rushwa mingi na pesa haikai.?
 
Too late! Dar es Salaam nyingi imejengwa kiholela, nilitegemea Dodoma angalau ijengwe kimpangilio, ila na yenyewe imejengwa kiholela hivyo hivyo! Hii nchi kama tumerogwa tu!
 
Hata kama suala la kibajeti/ kifedha ni changamoto wanaweza wakazielekeza serikali za mitaa kusimamia watu wajenge vizuri na kwa mpangilio na bado tukafanikiwa. Hii nchi solution zipo tena nyingi sana. Hatutakagi tu kuzitumia

Bora mtendaji wa mtaa asimamie hiyo kazi lakini kwenda Manispaa ni usumbufu, afisa anakwambia kuja kuona site umpe si chini ya shilingi 100,000/-

Sasa hela hiyo unamatofali mangapi? Mchanga Lori tayari hapo.

Actually pamoja na ukosefu wa pesa lakini swala vibari limerkwambia kiwango cha ujenzi nchini , sasa hayo sijui ni maendeleo au ?

Pelekeni ramani kwa watendaji wa mitaa wao wasimamie na kutoa vibari kwa wiki au monthly
 
Ukienda manispaa kupigwa danadana, unaambiwa leo hatushulikii maeneo ya huko njoo wiki ijayo!
 
Hapa hapa na mimi nichomekee!

Vipi kuhusu vijiji ambavyo vimo ndani ya halmashauri za miji na manispaa vinabanwa na katazo la waziri au sheria?

Kwa sababu, ukiisoma sera ya ardhi ya vijiji ya mwaka 1999 inampa mamlaka mwenyekiti wa kijiji kusimamia ardhi.

Naona kijijini unajenga bila kibali cha halmashauri, labda kwa vijiji vyenye waelewa ndo huwezi kujenga mpaka kamati ya ardhi ya kijiji itakapokuja kukuruhusu ujenge. Wanaweza kukushauri nyumba yako iangalie upande gani. Ukitembelea kijiji ukakiona kimepangwa ujue uongozi wa kijiji upo siriasi.

Sasa, baadhi ya watu sina uhakika kama wanatumia udhaifu wa sheria hii kujenga holela, katika vijiji ambavyo vimo ndani ya halmashauri za miji na manispaa. Nina uthibitisho wa hili, kuna manispaa ukijenga maeneo ya mjini kati, mipango miji wanandika "bomoa" au "leta kibari", ila ukijenga katika vijiji vilivyomo ndani ya manispaa hawaji kuandika, inaonekana wanaijua sheria.

Awamu iliyopita kuna kipindi waziri wa ardhi alisema wapo wanandaa sera mpya ya ardhi ya vijiji ila mpaka leo kimyaa.

Pia, kuna kipindi tena wizara ya ardhi ilisema ipo mbioni kuwapa mamlaka watendaji wa kata, kusimamia mipango miji kama sijakosea ila mpaka leo kimya.

Nilichogundua, wizara ya ardhi haipo siriasi na suala la ujenzi holela.

SULUHISHO
Serikali iipime ardhi yote nchi nzima au ianze kwa ngazi ya katani (wards) ili mtu anapotaka kujenga upande anaoutaka anaenda kununua kiwanja halmashuri kwa bei ndogo. Hela itarudi tu. Pia, faida ni kubwa kwa kizazi kijacho.

Udhaifu wa viwanja vya halmashauri (siyo zote), ni kwamba, baadhi ya halmashauri ni wasanii kwelikweli, badala ya kuuza viwanja maeneo mazuri, ila wenyewe wanaenda kununua maeneo mabaya mfano mbugani, wanayapima na kuwauzia viwanja watu. Usipokuwa makini watakuuzia kiwanja kwa kuangalia kwenye ramani mkiwa ofisini kwao, ila siku ukienda kukiona kiwanja unakuta bonde au mbuga.

Wizara ya ardhi kuweni siriasi na upangaji miji kwa faida y badae. Ni bora muache kujenga reli ilimradi muipange nchi.
 
Kuwepo na ratiba ya afisa ardhi anishirikiana na mtendaji wa mtaa kuhusu hivyo vibari,

Walau kwa wiki au kwa mwezi wafanyie kazi mwananchi yeye akachukue apeleke maombi yake na kwenda kuchukua kibali kwa mtendaji kwa wiki au ndani ya wiki mbili.

Au awawepo afisa ardhi kwenye kila serikali ya mtaa.

Lakini utaratibu uliopo sasa unakatisha tama kabisa!
 
Back
Top Bottom