Waziri Lukuvi awataka wamiliki wa ardhi kujenga kwa kufuata sheria

Waziri Lukuvi awataka wamiliki wa ardhi kujenga kwa kufuata sheria

Kwa nini anawataka? Chukua hatua kila siku blah blah tu, watu wanaendelea kuvunja sheria, chukua hatua na siyo matamko, ...
 
Bora mtendaji wa mtaa asimamie hiyo kazi lakini kwenda Manispaa ni usumbufu, afisa anakwambia kuja kuona site umpe si chini ya shilingi 100,000/-

Bado usumbufu mara uambiwe kanunue ramani wizara ya ardhi,

Bado hujalipia kibari chenyewe hela chungu nzima[emoji108][emoji108]

Sasa hela hiyo unamatofali mangapi? Mchanga Lori tayari hapo.

Actually pamoja na ukosefu wa pesa lakini swala vibari limerkwambia kiwango cha ujenzi nchini , sasa hayo sijui ni maendeleo au ?

Pelekeni ramani kwa watendaji wa mitaa wao wasimamie na kutoa vibari kwa wiki au monthly
 
Hapa hapa na mimi nichomekee!

Vipi kuhusu vijiji ambavyo vimo ndani ya halmashauri za miji na manispaa vinabanwa na katazo la waziri au sheria?

Kwa sababu, ukiisoma sera ya ardhi ya vijiji ya mwaka 1999 inampa mamlaka mwenyekiti wa kijiji kusimamia ardhi.

Naona kijijini unajenga bila kibali cha halmashauri, labda kwa vijiji vyenye waelewa ndo huwezi kujenga mpaka kamati ya ardhi ya kijiji itakapokuja kukuruhusu ujenge. Wanaweza kukushauri nyumba yako iangalie upande gani. Ukitembelea kijiji ukakiona kimepangwa ujue uongozi wa kijiji upo siriasi.

Sasa, baadhi ya watu sina uhakika kama wanatumia udhaifu wa sheria hii kujenga holela, katika vijiji ambavyo vimo ndani ya halmashauri za miji na manispaa. Nina uthibitisho wa hili, kuna manispaa ukijenga maeneo ya mjini kati, mipango miji wanandika "bomoa" au "leta kibari", ila ukijenga katika vijiji vilivyomo ndani ya manispaa hawaji kuandika, inaonekana wanaijua sheria.

Awamu iliyopita kuna kipindi waziri wa ardhi alisema wapo wanandaa sera mpya ya ardhi ya vijiji ila mpaka leo kimyaa.

Pia, kuna kipindi tena wizara ya ardhi ilisema ipo mbioni kuwapa mamlaka watendaji wa kata, kusimamia mipango miji kama sijakosea ila mpaka leo kimya.

Nilichogundua, wizara ya ardhi haipo siriasi na suala la ujenzi holela.

SULUHISHO
Serikali iipime ardhi yote nchi nzima au ianze kwa ngazi ya katani (wards) ili mtu anapotaka kujenga upande anaoutaka anaenda kununua kiwanja halmashuri kwa bei ndogo. Hela itarudi tu. Pia, faida ni kubwa kwa kizazi kijacho.

Udhaifu wa viwanja vya halmashauri (siyo zote), ni kwamba, baadhi ya halmashauri ni wasanii kwelikweli, badala ya kuuza viwanja maeneo mazuri, ila wenyewe wanaenda kununua maeneo mabaya mfano mbugani, wanayapima na kuwauzia viwanja watu. Usipokuwa makini watakuuzia kiwanja kwa kuangalia kwenye ramani mkiwa ofisini kwao, ila siku ukienda kukiona kiwanja unakuta bonde au mbuga.

Wizara ya ardhi kuweni siriasi na upangaji miji kwa faida y badae. Ni bora muache kujenga reli ilimradi muipange nchi.
Pia inakuwaje mpaka leo kuna vijiji vimo ndani ya halmashauri za manispaa? Hii inachochea ujenzi holela unaofanywa na watu kutoka mjini kati.
 
Halafu siku hizi mtu anatakiwa kulipia land rent kwenye kiwanja kisicho na hati?

Haya yameanza lini jamani?

Kwanini msipimie watu kwanza wakishapata hati ndiyo walipie?
 
Eti ukienda Manispaa wanakwambia eneo lako liko wapi? Unawajibu sehemu fulani, wanakwambia leo hatushulikii maeneo ya huko, njoo wiki ijayo siku fulani !

Siku utakayoenda utaambiwa kanunue ramani wizara ya ardhi kwanza halafu uje nayo Hapa Manispaa.

Ukishaenda kununua ukija afisa ardhi anakwambia kuja kuona site shilingi 100,000 na kuendelea.

Bado gharama ya kibali chenyewe na nauli ya kufuatilia nenda rudi.

Hapo bado uambiwe eneo lako limeingiliana na eneo la jirani yako kwenye ramani,

Sasa kama limeingiliana na eneo la jirani mimi mwananchi nifanyeje?

Je wizara haijaweka utaratibu wa nini kifanyike iwapo ikitokea hivyo?

Au uambiwe ramani inaonesha eneo ni bonde, unamuuliza ulivyoenda kuona uliona bonde pale? Anakwambia hapana sikuona bonde.

Basi baada ya hapo ni nenda rudi utapigwa danadana hadi ujikatie tamaa mwenyewe na kugairi kujenga!

Watu wengi sana wamegairi kujenga kwa huo usumbufu ulojitokeza!
 
Sheria ilikuwepo kitambo sema swala ilikua kumpata mtu wa kuitekeleza tu.

Tanzania tuna mambo mengi sana mazuri ila yapo kwenye makaratasi hakuna wa kuyafanya yakaonekana.
 
Sheria ilikuwepo kitambo sema swala ilikua kumpata mtu wa kuitekeleza tu.

Tanzania tuna mambo mengi sana mazuri ila yapo kwenye makaratasi hakuna wa kuyafanya yakaonekana.
Kuna mda akili zikiwarudia hadi mnafurahisha
 
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amewataka wamiliki wa ardhi wanaotaka kujenga kuhakikisha wanafuata sheria na taratibu zote wakati wa kufanya ujenzi.

Waziri Lukuvi alisema hayo mwishoni mwa wiki hii katika ofisi yake ya ardhi ya mkoani Dar es Salaam na Pwani. Alisema sheria inamtaka mmiliki wa ardhi anayetaka kufanya ujenzi kupata kibali kutoka halmashauri za miji, manispaa na majiji na kuongeza kuwa sheria hiyo inakataza kufanya ujenzi bila kibali kutoka mamlaka husika.

”Naelekeza watendaji wote wawe wa ardhi au mipango miji kuhakikisha sheria zinafuatwa kwa kudhibiti ujenzi holela na sheria inakataza kabisa kujenga bila kupata kibali kutoka katika mamlaka husika” alisema Lukuvi.

Kwa mujibu wa Lukuvi, zoezi la urasimishaji linaloendelea sasa maeneo mbalimbali ni kwa majengo yaliyojengwa tu na kusisitiza kuwa zoezi la urasimishaji isiwe sehemu endelevu ya kuvunja sheria na kubainisha kuwa angetaka kuona maeneo yote ya miji hasa Dodoma yanajengwa kwa kupatiwa kibali.

Aliwataka wataalamu wote hasa waliopo halmashauri katika yale maeneo yaliyotangazwa kimji kwa mujibu wa sheria wananchi wake waelimishwe kujenga katika viwanja vilivyopangwa na kupimwa na wawe wamepatiwa vibali na mamlaka za halmashauri husika.

”hatua zichukuliwe kuzuia jambo hili tunataka miji endelevu ambayo wananchi wanaishi na kujenga kwa mujibu wa sheria” alisema Lukuvi.



Nadhani lengo la lukuvi ilitakiwa kwa skwata tu ili wakusanye kodi na kupanga vizuri ,sasa maeneo yaliyopimwa si kila mtu anajua mipaka yake na pia matumizi ya eneo lake kama residential,comercial au social services etc hapa kibali ni kwa ajili ya kukusanya kodi tu.
 
Back
Top Bottom