Tetesi: Waziri Maghembe kutumbuliwa

Kwa PM kudai kaburi la uncle Faru John ni kutokana na maelezo ya wataalamu wa hifadhi kuwa alikufa kwa ugonjwa,na akifa kwa ugonjwa na ikathibitika hivyo,huzikwa ili kutoleta maambukizi kwa wanyama wengine wala mizoga kama fisi na mbwa mwitu,hivyo watuonyeshe kaburi lake,la hasha kama kama hakufa kwa ugonjwa ni kipi kilichomuua?
 
Alinifukuza chuo huyu akafanya nihamie bara lingine kabisa . Naamini zamu yake nae imefika kuishi kama shetani.

[HASHTAG]#BringBackBenAlive[/HASHTAG].
Duh!kama ni kweli na kama alikuonea acha zamu yake ifike haraka haraka,binafsi siwapendi watu wanaokatisha ndoto za wenzao kwa uonevu.
 
Mkuu umeongea jambo la msingi sana. Hiki ulichoongea hasa ndio mzizi wa skandali hii. Sioni jinsi ambavyo hili jangili (Maghembe) litanusurika katika sakata hili hasa ukizingatia naye alikuwa mstari wa mbele kumdanganya PM. Sasa anapoombwa atuoneshe lilipo kaburi hilo anabaki anang'aang'aa na kupepesa macho kama tutusa. Ajitokeze kutoka huko mafichoni aliko atuoneshe kaburi. Hicho tu ndicho tunachokitaka...na asidhani akionyesha kaburi itaishia hapo...maana asije akaenda mbio mbio kuua tembo na kumzika akaja kutuambia ni John...vinasaba vitapimwa babu wee! Hapa ndipo patamu. Yaani hana pa kuchomokea...maji yako shingoni.

[HASHTAG]#bringbackourrhinoalive[/HASHTAG]
 
Mi namkumbuka Waziri Mkuu mmoja tu aliyediriki kuweka uongo na kudanganya...sasa hivi Yuki chadema
Kwani mahakama za mafisadi hazijaanza apelekwe huko akajibu tuhuma hizi?
 
Mkuu nchi hii inaongozwa na ukoo wa panya...usiumize kichwa. Wapiga deal wanaanzia Magogoni hadi kule kijijini Mtakuja. Inauma sana.
 

Hahahaaaa! Na kaomba Pembe kaletewa Pembe za Fudu Pori ahangaike nalo lile la Faru John washatengenezea Mkuyati wa Kichina watu wametumia na sasa wapo juu ya Viuno wanapiga show
 
Hahahaaaa! Na kaomba Pembe kaletewa Pembe za Fudu Pori ahangaike nalo lile la Faru John washatengenezea Mkuyati wa Kichina watu wametumia na sasa wapo juu ya Viuno wanapiga show
Hahahahahahaaaaaaaaaa! Mkuu una maneno wewe.
 
maghembe na makaburu wa Sasakwa wanajuwa kila kitu warudish Faru wetu.Hawa CCM hawana jipya tulisha sema Faru wao Tembo wao.Halafu Mwakyembe anakuja na mbwembwe eti mahakama ya mafisadi haina kesi badala ya kusema haijui ianze na nani maana wote ni majizi watupu.Aibu yako Mwakyembe unaaibisha taaluma yako nenda kafundishe.
 
Hawezi kutumbuliwa kwa 100%

Akitumbuliwa hamna tena waziri kutoka kaskazini
 
Hawezi kutumbuliwa kwa 100%

Akitumbuliwa hamna tena waziri kutoka kaskazini
Kwani yupo pale kwa sababu ya UKASKAZINI wake? Kama ndivyo, basi ataendelea kuua vifaru wetu hadi atosheke mwenyewe!
 
Atumbuliwe kwann alidanganye taifa kuwa faru john amekufa wakat kauzwaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…