Tetesi: Waziri Maghembe kutumbuliwa

tpaul kwa hakika wewe unaongea kinafiki kwa kuvunga eti unamsifia JPM ili tu ionekane anatumbua mawaziri wengi nakwamba Serikali yake inayumba au kukosa uimara. Wewe ni Li-Chadema, acha unafiki wako. Tumeshakugundua, huwezi kutujaza ujinga ng'o.
 
Kwani mahakama za mafisadi hazijaanza apelekwe huko akajibu tuhuma hizi?
Sijaongelea ufisadi Bali kusema uongo na kudanganya kwa Waziri Mkuu wa kipindi Fulani...akadanganya tena kuwa hawezi Kutoka ndani ya chama kilichomlea...historia inamhukumu
 
Wait....huyu bwana John kafa au kapotea na yeye? Mbona kama mtoa mada kama sijakuelewa vile....Kama umekuja na taarifa yako nyingine vile
 
Wait....huyu bwana John kafa au kapotea na yeye? Mbona kama mtoa mada kama sijakuelewa vile....Kama umekuja na taarifa yako nyingine vile
Rudia tena kusoma uzi mkuu. Faru Johm kauzwa na Maghembe akishirikiana na genge lake la majangili kwa thamani ya Tsh milioni 200. Baada ya kumuuza wamesingizia kwamba faru alikufa wakamzika. PM kawaambia wakamletee mifupa yake ipimwe DNA, wahusika wameingia mitini.
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] kwa hiyo mkuu sasa huyu jamaa john yupo somewhere katulia? Au kauzwa then akafa? Hapa ndo panaponichanganya sasa....
 
Faru aliuzwa kabla hajawa Waziri acha uongo wewe mwongo
 
Faru aliuzwa kabla hajawa Waziri acha uongo wewe mwongo
Nani muongo? Maghembe? Ni kweli Maghembe ni muongo....hata kama hakuwepo wakati anauzwa kwanini amdanganye waziri mkuu kwamba yule faru amekufa ilhali wamemuuza kwa makaburu?
 
Magufuli ni mtu wa visasi...kamwe hawezi kuwateua wapinzani zaidi ya alivyompoza Mrema kwa jitihada zake za kubomoa upinzani.
Hii nchi bhanaa ni shidah! Watu saba kwenye viroba wamekutwa wamekufwa na mawe juu wasionekane, mtaani ibaki stori, polisi kampiga mtoto risasi, ikasemwa polisi alilenga kupiga kwenye lami ikapita, polisi wamevamiwa wakauwawa, wakati mwingine wakaporwa silaha ikapita. sasa faru kupotea imekuwa ishu? Hivi thamani ya watanzania uhai wao si kitu ukilinganisha na wa wanyama pori? Uwiiiiiiiiii
 
wewe nae jiongeze, walipataje zile pembe, kama hawajui mahali alipofia, kwa kuwa alikuwa chini ya uangalizi maalumu, lazima alipo kufa picha za kumbukumbu zilichukuliwa, na mwenendo wa afya yake lazima zilikuwa zinarekodiwa, nahivi ndo PM anavitaka, reasoning beyond dought
 
Sasa nijiongezee nini hapo?!
 
Sasa nijiongezee nini hapo?!
ujiongeze kutoka kwenye maelezo uliosikia, rhino are endemic species, wapo chini ya uangalizi maalumu ndo maana wameitwa hadi majina, si rahisi akafa bila kuwepo na rekodi za msingi
 
ujiongeze kutoka kwenye maelezo uliosikia, rhino are endemic species, wapo chini ya uangalizi maalumu ndo maana wameitwa hadi majina, si rahisi akafa bila kuwepo na rekodi za msingi
Umenisoma kwa vituo ukanielewa?!
 
Mkuu kuna baadhi ya watu humu wanapenda kujitoa akili utadhani wamekatwa vichwa.
 
Sasa sio TETESI tena bali ni DHAHIRI. Waziri Mkuu amekasirika sana baada ya kugundulika kwamba Prof Maghembe alimuonyesha pembe feki za faru na wala hazikuwa za faru John kama ilivyotarajiwa. Baada ya habari hizi kumfikia Rais Makufuri anatarajiwa kumtangaza mrithi wa Maghembe muda wowote juanzia sasa.

Mods tafadhali naomba mbadilishe status ya uzi huu kutoka TETESI kuwa BREAKING NEWS!
 
Umetisha..kama vile ulikua ukimchungulia Faru John all the time
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…