Waziri Mahiga: Serikali ya Uturuki imetuambia wamiliki wa shule za Feza ni magaidi

Waziri Mahiga: Serikali ya Uturuki imetuambia wamiliki wa shule za Feza ni magaidi

Zinaweza kuwa zinaenda kwa mfumo wa kawaida kabisa bila hata utakatishaji lakini zimelengwa kufanikisha ugaidi.

Wakisema wanatuma fedh akwenda kwa yule Fetullah aliyeko marekani, kwa jambo sahihi kabisa na la wazi, nani ataquestion? Fetullah anapochannel hizo fedha kutoka amerika, Tz inasimamiaje kwamba haziendi kufanikisha ugaidi?

Serikali ichunguze.
Ok LAKINI bado hatuna uhakika wa nani anamiliki hizo shule hapa Tanzania
 
Tembelea Feza Schools hata kwa Picha tu

4b784bdb-35c4-4e36-a722-6d9c2b18a478_Slayt5%20(Custom).JPG


814009fa-fb82-4b40-8a73-00e966aa022f_Slayt6%20(Custom).JPG


f8defc32-cc16-4377-b75e-1824dddc3923_Slayt7%20(Custom).JPG


2df01bad-edbc-4f8a-a361-471ad532dd79_Slayt11%20(Custom).JPG


d71ce3c5-db5d-4275-ae45-cb617bd3b7bb_Slayt18%20(Custom).JPG


a16d6857-2c41-4c67-9141-560b0fede128_Slayt23%20(Custom).JPG


2462ce2b-5a76-4dc5-af33-c3ad0906848b_Slayt25%20(Custom).JPG


8a8cfbeb-5fae-49cd-91a7-0bd7b604189d_Slayt26%20(Custom).JPG


c5c11b93-99fa-427a-9d9f-15f8f4131074_Slayt31%20(Custom).JPG


90a9d899-8bb5-43fb-acb2-98b8e0492984_Slayt33%20(Custom).JPG


f5dca559-b65d-4c9a-863f-a2f6393b9c66_Slayt39%20(Custom).JPG
 
Hapo kunatengenezwa uzushi kuzichafua hizo shule hakuna lingine,tunajua upande flani hauna haki hapa tanzania basi tuachieni hata hivyo vichache jamani.
Ndugu jitahidi kutumia kichwa kabla ya kuandika, si vizuri kutumia makalio ili hali wasomaji humu jf wanatumia vichwa! Tarifa zimetoka Uturuki wewe unakurupuka eti upande fulani hawana haki, kuna uhusiano gani sasa. Au wewe ni mmoja wa magaidi?
 
Serikali ya Uturuki ni waongo !, wamekubwa na kuchanganyikiwa na jaribio hilo sasa wanataka kumuingiza kila mtu hata asiyehusika !. Wemesingizia eti shule hizo zinafundisha ugaidi !. MFA wasipate taabu kulithibitisha hili, wawasiliane na Baba Mwana Asha , kwa sababu Mwana Asha alisoma hapo.

Pasco
Wanadai jamaa ni mpinzani wa serikali, na fedha zinazokusanywa kama ada hapo zinatumika kufadhili waliotaka kuipindua serikali ya jamaa kule, inaweza kuwa kweli au uwongo..
 
Ishu kama hizi anaziweza Jk na Memba maana wale jamaa kwa diplomasia si mchezo.
 
Swadakta ! Na ukiangalia kisa chake inaweza kuwa waligoma kuchangia kampeni za ccm .
Kwa hii post umejitoa ufahamu kabisa....hivi wanaolalamika kuwa FEZA wanahusika Na jaribio la Mapinduzi huko Uturuki ni serikali ya Uturuki au serikali Tanzania.?
 
Utawala wa kishetani bhana.. kutia watu hofu tu kila kukicha, kama kuna uhusiano na sheikh Fethullah kwanini wasimtie nguvuni huko marekani
 
GAIDI HALAFU ANAISHI USA ? HAWA JAMAA WASITUINGIZE KATIKA MAGOMVI YAO YA NDANI. HUYU RAIS WA UTURUKI NI DICTETA WA KUTUPA KILA ANAEMPINGA NI GAIDI HAJIAMINI.
TUSIJIINGIZE KATIKA MATATIZO YAO...ALITAKA KUPINDULIWA AKA SALIMIKA HAYO YAKE MWENYEWE
ADUI WAKE SIO ADUI WETU, NA RAFIKI WAKE SIO RAFIKI YETU.
ASITUCHAGULIE RAFIKI HUO NDO MTAZAMO WA SERIKALI YETU IFUATE
 
Mimi nadhani barozi yuko sahihi kutaka ushahidi. Lakini pia usalama wafanye utafiti wa jambo hilo ili kujua mbivu na mbichi.
 
Upuuzi mpya wa waturuki. Watatue matatizo yao ya ndani waachane na siasa za kipuuzi
 
Waturuki Kwahili Ni Wazushi, Wao Walitaka Kupinduana...
Sasa Mas-ala Yao Ya Kisiasa Wameamua Kumfatilia Kila Mpinzani Anayeishi Hata Kama Nje Ya Nchi Katika Sehemu Yeyote Hile Duniani ikiwemo Tanzania Kumzima Kwa Njia Yoyote hile.
Kwahiyo Wanataka Kuitumia Tanzania Kisiasa Kutaka Kuwazima Wamiliki wa Feza Kwakuwa Chama Kinachotawala Uturuki Kinaamini Kuwa Ni Wapinzani.
Na Kwa Mujibu Wa Uturuki Katika Jitihada Zao Za Kutaka Kuzima Upinzani Basi Wamehukumu Kuwa Kila Mpinzani Basi Kwa Njia Moja au Nyengine Itakuwa Alihusika Katika Mapinduzi.
Usibishe bishe hovyo kwa jambo usilolijua.
Toa ushahidi unaokinzana na wa serikali ya uturuki vinginevyo unapiga mboyoyo zisizo na maana
 
Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Augustino Mahiga amesema serikali ya Uturuki kupitia balozi wake hapa nchini imedai wamiliki wa shule za Feza Tanzania walifadhili jaribio la mapinduzi Uturuki

Serikali hiyo inadai mapinduzi hayo hayakuanzia jeshini tu bali yameanzia kwenye vyuo na shule mbalimbali Uturuki na nje ya uturuki
Ubalozi wa Uturuki umesema wamiliki wa shule hizo hapa nchini wanahusika na kufadhili mapinduzi hayo huko Uturuki na ada inayokusanywa kutoka kwenye shule hizo ilitumika kufadhili mapinduzi hayo na ni magaidi
Balozi Mahiga amesema wametaka ushahidi zaidi kutoka serikali ya Uturuki kuhusu madai hayo



Walimu wa shule ya Feza wamedai wao hawahusiki kabisa na mapinduzi hayo na shule zao hazijihusishi na mambo ya siasa na zinamilikiwa na watanzania

Ni ajabu walimu wa shule kukanusha taarifa zinazopaswa kukanushwa na wamiliki wa shule . hao wamiliki wa shule hawapo mpaka walimu waje wakanushe taarifa ambazo ziko nje ya mamlaka yao ?
 
mimi ni mmoja wa wanafunzi nimesoma apo FEZA o-level na high-level. shule za FEZA hazina mtaala wowote unaofundisha ugaidi.

shule ina walimu mchanganyiko waturuki na watanzania. wanafunzi wengine niliosoma nao sasa hivi ni walimu apo FEZA. kwa mfano mkuu wa shule ya FEZA boys alisoma apo O-level baadae akafanya bachelor Uturuki na masters kafanya UDSM.

miaka yote iyo tumesoma mpaka sasa kila mtu anafanya maisha yake sijawahi kusikia ata siku moja mwanafunzi yeyote wa FEZA ambaye amefanya tukio la kigaidi. wengi wetu tumekua watu wema kutokana na mafunzo mazuri tuliyopata pale shuleni.

nimewahi kua moja wa kiongozi wa wanafunzi ila hakuna ata siku moja ambayo tumeelekezwa tufanye tukio la ovyo. shule ziko serious na elimu pekee. shule za FEZA zinajiendesha kutoakana na ada wanazolipa wazazi wa wanafunzi matajiri pia wanafunzi maskini wanasomeshwa kutokana na michango ya wazazi matajiri na baadhi ya wanafunzi waliosoma apo ambao asilimia kubwa wamefanikiwa kimaisha.

ivyo basi kwa mimi binafsi naweza kusema kuwa shule za FEZA hazina uhusiano wowote ule na ugaidi. Uturuki raisi Erdogan amevurugwa tu kutokana na sera zake za ovyo za kuminya demokrasia na ndio maana mpaka leo umoja wa ulaya (EU) wameshindwa kuiruhusu uturuki kujiunga na umoja huo kutokana na uvunjifu mkubwa wa demokrasia.

Waturuki ni watu wanapenda sana biashara na wamesambaa kila kona ya dunia na wamechangia kukua kwa uchumi kwa nchi mbalimbali duniani kwa kutoa ajira kwa wazawa wa mataifa ambayo wanawekeza. kwa mfano ukienda Poland, Germany na mataifa mengi tu ya ulaya jamaa wametoa ajira kwa mamilioni ya watu.

kwa mfano rafiki zangu wengi tu hapa bongo na ata nje ya nchi wanafanya kazi na waturuki na wako vizuri tu. Fethullah Gullen yeye sio mmiliki wa shule za FEZA ila yeye alitoa idea kwa waturuki kuanzisha mashule nje ya uturuki ili kutoa elimu bora kwa mataifa mbalimbali duniani.

Hachangii na wala hapewi ata senti kutoka kwenye shule. uwekezaji hapa bongo wote umefanywa kutokana na ada na michango ya watanzania wachache ambao wameshawishika kuchangia shule.

rafiki yangu mmoja baba yake mzazi ametoa tiles za shule nzima for free. mimi pamoja na wanafunzi wengine tumeshapiga rangi sana shule za FEZA kwa kujitolea. ivyo basi naweza sema shule za FEZA hazina uhusiano wowote ule ayo mambo yao ya ndani ya uturuki wajaribu kumalizana nayo wenyewe.

huo ubalozi kama unajua kuhusu iyo michango ya kigaidi basi wafungie hizo account ambazo zinapewa iyo misaada. Nigeria wamemgomea Erdogan na serikali yake kuhusu kufunga shule za aina ya FEZA ambazo zipo Uturuki ivyo serikali yetu isiyumbishwe kutokana na uyo Erdogan.

shule hizi zinazalisha wataalamu wakutosha ambao wana mchango mkubwa tu kwa taifa ili. rafiki zangu wengi tu sasa hivi ni madiktar katika hospitali za hapahapa nchini, wengine mainjia wazuri tu na wanasaidia mambo mbalimbali.
You Nailed it Bro, nimesoma University na wanafunzi waliosoma Feza, napenda niseme kweli jamaa wapo serious na kitabu na nidhamu ya hali ya juu. tusije tukaentertain mambo ya nje yavuruge mazuri yetu ya ndani.
 
Wagaratia wanaozungumziwa kwenye biblia ndio Waturuki haswa.. Nadhani waislam wote waeleweni hii jamii ndio tabia yao wakigombana wao kwa wao na wewe una urafiki nao wote wanakuambia uchague upande mmoja. Zama hizo waliitwa watu wapumbavu na Malofa.

Erdogan anatumia mwanya Wa mapinduzi kuteketeza adui zake wote... Hadi walimu wauza pipi n.k yaani mpango wake sio kuwazuia au kuwafunga Bali kuwanyonga wote... Watatoa msimamo wao soon na hizo shule watazichukua serikali ya Ankara

hapo juu nilipo Bold + italics Ongezea Neno Malofa
 
Back
Top Bottom