Powder
JF-Expert Member
- Jan 6, 2016
- 4,977
- 6,635
Gaidi Mtarajiwa!Sasa na mtoto wa mkuu anasoma FEZA itakuwaje?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Gaidi Mtarajiwa!Sasa na mtoto wa mkuu anasoma FEZA itakuwaje?
Sasa n'jomba kwani hili sakata limeanzishwa na makanisa hapa bongo au limetoka Uturuki??!!The bottom line of the entire story ni udini. Shule za FEZA ndio zilionekana kutoa upinzani mkalikwa shule za makanisa na hili lilikuwa halifurahiwi. Kama zilikuwa zinatumia mbinu za kigaidi kufundishia wanafunzi(sijui ndio maana wanafanya vizuri mitihani yao) Serikali ilikuwa wapi wakati wote huo " isiwashughulikie"? Wacheni unafiki wa kidini tena kweupe
Unamaanisha shule za FEZA ni za upande flani na siyo za yule mturuki?Hapo kunatengenezwa uzushi kuzichafua hizo shule hakuna lingine,tunajua upande flani hauna haki hapa tanzania basi tuachieni hata hivyo vichache jamani.
Umenena VEMAKwani balozi wa uturuki aliyesema hizo shule zilikuwa zinatumia mbinu za kigaidi ni mkristo? Hayo ya ugaidi hayajasemwa na kanisa wala serikali ya Tanzania yamesemwa na balozi wa uturuki.
Taarifa zimepelekwa kwa hao jamaa kua huku tanzania kuna shule ya upande fulani imeanza kufaulisha sana tufanyeje ili tuiue tubaki na shule zetu?kwa vile nchi yetu ni ya upande fulani basi wakatoa ushirikiano haraka sana.Unamaanisha shule za FEZA ni za upande flani na siyo za yule mturuki?
ADA, UGAIDI natafakariWanalipa ada inayotumika kufadhili ugaidi.jiongeze wewe usiwe na akili fupi kama mkia wa mbuzi.
Mkuu taratibuKwa hiyo ao walimu wanaotumia mbinu za kigaidi kufundishia wameshakamatwa?
Kanisa katoliki lilishiriki kwa kiasi kikubwa mauaji ya kimbari Rwanda,Tanzania tuwe makini na kanisa hilo na shule zake..wachangiaji wanakosea kulichukulia suala hili kirahisi-rahisi.
..wamiliki wa shule za Feza wanatuhumiwa kuhusika na UHAINI nchini kwao. Hizi ni tuhuma nzito.
..kama nchi tunatakiwa tuwe makini sana na watu hao.
..tuangalie maslahi mapana ya nchi yetu KIUCHUMI na KIUSALAMA.
Serikali ya Tanzania yasema haina ushahidi wa kutosha kuzitia hatiani shule za Feza zinazodaiwa kumilikiwa na raia wa Uturuki anayetuhumiwa kujihusisha na jaribio la kupindua Serikali ya Uturuki.
Serikali ya Uturuki inadai wamiliki wa shule hizo na baadhi ya wafanyabiashara wanafadhili ugaidi kwa kushirikiana na Imamu Fethullah Gulen anayeishi nchini Marekani ambaye ndio inadaiwa yuko nyuma ya jaribio la Mapinduzi.
= > Serikali ya Uturuki yatakiwa kuwasilisha taarifa zenye ushahidi wa kutosha juu ya hili.
= > Aidha, Ubalozi wa Uturuki Tanzania umedai kuwa baadhi ya walimu wa shule za FEZA ambao ni raia wa Uturuki wamekuwa wakitumia mbinu za kigaidi kufundisha wanafunzi.
Feza wakanusha kuhusika
Umeona ee. Yaani Watanzania wanawajua zaidi waturuki kuliko waturuki wenzao!Waturuki wenyewe wanasema FEZA ni magaidi alafu nyie wabongo mnaleta ubishi..... Povu jingi..... Subirini muone
Waturuki wenyewe wanasema FEZA ni magaidi alafu nyie wabongo mnaleta ubishi..... Povu jingi..... Subirini muone
mimi ni mmoja wa wanafunzi nimesoma apo FEZA o-level na high-level. shule za FEZA hazina mtaala wowote unaofundisha ugaidi. shule ina walimu mchanganyiko waturuki na watanzania. wanafunzi wengine niliosoma nao sasa hivi ni walimu apo FEZA. kwa mfano mkuu wa shule ya FEZA boys alisoma apo O-level baadae akafanya bachelor Uturuki na masters kafanya UDSM. miaka yote iyo tumesoma mpaka sasa kila mtu anafanya maisha yake sijawahi kusikia ata siku moja mwanafunzi yeyote wa FEZA ambaye amefanya tukio la kigaidi. wengi wetu tumekua watu wema kutokana na mafunzo mazuri tuliyopata pale shuleni. nimewahi kua moja wa kiongozi wa wanafunzi ila hakuna ata siku moja ambayo tumeelekezwa tufanye tukio la ovyo. shule ziko serious na elimu pekee. shule za FEZA zinajiendesha kutoakana na ada wanazolipa wazazi wa wanafunzi matajiri pia wanafunzi maskini wanasomeshwa kutokana na michango ya wazazi matajiri na baadhi ya wanafunzi waliosoma apo ambao asilimia kubwa wamefanikiwa kimaisha. ivyo basi kwa mimi binafsi naweza kusema kuwa shule za FEZA hazina uhusiano wowote ule na ugaidi. Uturuki raisi Erdogan amevurugwa tu kutokana na sera zake za ovyo za kuminya demokrasia na ndio maana mpaka leo umoja wa ulaya (EU) wameshindwa kuiruhusu uturuki kujiunga na umoja huo kutokana na uvunjifu mkubwa wa demokrasia. Waturuki ni watu wanapenda sana biashara na wamesambaa kila kona ya dunia na wamechangia kukua kwa uchumi kwa nchi mbalimbali duniani kwa kutoa ajira kwa wazawa wa mataifa ambayo wanawekeza. kwa mfano ukienda Poland, Germany na mataifa mengi tu ya ulaya jamaa wametoa ajira kwa mamilioni ya watu. kwa mfano rafiki zangu wengi tu hapa bongo na ata nje ya nchi wanafanya kazi na waturuki na wako vizuri tu. Fethullah Gullen yeye sio mmiliki wa shule za FEZA ila yeye alitoa idea kwa waturuki kuanzisha mashule nje ya uturuki ili kutoa elimu bora kwa mataifa mbalimbali duniani. Hachangii na wala hapewi ata senti kutoka kwenye shule. uwekezaji hapa bongo wote umefanywa kutokana na ada na michango ya watanzania wachache ambao wameshawishika kuchangia shule. rafiki yangu mmoja baba yake mzazi ametoa tiles za shule nzima for free. mimi pamoja na wanafunzi wengine tumeshapiga rangi sana shule za FEZA kwa kujitolea. ivyo basi naweza sema shule za FEZA hazina uhusiano wowote ule ayo mambo yao ya ndani ya uturuki wajaribu kumalizana nayo wenyewe. huo ubalozi kama unajua kuhusu iyo michango ya kigaidi basi wafungie hizo account ambazo zinapewa iyo misaada. Nigeria wamemgomea Erdogan na serikali yake kuhusu kufunga shule za aina ya FEZA ambazo zipo Uturuki ivyo serikali yetu isiyumbishwe kutokana na uyo Erdogan. shule hizi zinazalisha wataalamu wakutosha ambao wana mchango mkubwa tu kwa taifa ili. rafiki zangu wengi tu sasa hivi ni madiktar katika hospitali za hapahapa nchini, wengine mainjia wazuri tu na wanasaidia mambo mbalimbali.
kwani Feza iko Uturuki?Waturuki wenyewe wanasema FEZA ni magaidi alafu nyie wabongo mnaleta ubishi..... Povu jingi..... Subirini muone
wanamiliki kwa pamoja wote watanzania na waturuki.Shule zinamilikiwa na nani? Watanzania au Waturuki under Ishik Foundation
Kanisa katoliki lilishiriki kwa kiasi kikubwa mauaji ya kimbari Rwanda,Tanzania tuwe makini na kanisa hilo na shule zake