Waziri Mahiga: Serikali ya Uturuki imetuambia wamiliki wa shule za Feza ni magaidi

Ok LAKINI bado hatuna uhakika wa nani anamiliki hizo shule hapa Tanzania
 
Hapo kunatengenezwa uzushi kuzichafua hizo shule hakuna lingine,tunajua upande flani hauna haki hapa tanzania basi tuachieni hata hivyo vichache jamani.
Ndugu jitahidi kutumia kichwa kabla ya kuandika, si vizuri kutumia makalio ili hali wasomaji humu jf wanatumia vichwa! Tarifa zimetoka Uturuki wewe unakurupuka eti upande fulani hawana haki, kuna uhusiano gani sasa. Au wewe ni mmoja wa magaidi?
 
Wanadai jamaa ni mpinzani wa serikali, na fedha zinazokusanywa kama ada hapo zinatumika kufadhili waliotaka kuipindua serikali ya jamaa kule, inaweza kuwa kweli au uwongo..
 
Ishu kama hizi anaziweza Jk na Memba maana wale jamaa kwa diplomasia si mchezo.
 
Swadakta ! Na ukiangalia kisa chake inaweza kuwa waligoma kuchangia kampeni za ccm .
Kwa hii post umejitoa ufahamu kabisa....hivi wanaolalamika kuwa FEZA wanahusika Na jaribio la Mapinduzi huko Uturuki ni serikali ya Uturuki au serikali Tanzania.?
 
Utawala wa kishetani bhana.. kutia watu hofu tu kila kukicha, kama kuna uhusiano na sheikh Fethullah kwanini wasimtie nguvuni huko marekani
 
GAIDI HALAFU ANAISHI USA ? HAWA JAMAA WASITUINGIZE KATIKA MAGOMVI YAO YA NDANI. HUYU RAIS WA UTURUKI NI DICTETA WA KUTUPA KILA ANAEMPINGA NI GAIDI HAJIAMINI.
TUSIJIINGIZE KATIKA MATATIZO YAO...ALITAKA KUPINDULIWA AKA SALIMIKA HAYO YAKE MWENYEWE
ADUI WAKE SIO ADUI WETU, NA RAFIKI WAKE SIO RAFIKI YETU.
ASITUCHAGULIE RAFIKI HUO NDO MTAZAMO WA SERIKALI YETU IFUATE
 
Mimi nadhani barozi yuko sahihi kutaka ushahidi. Lakini pia usalama wafanye utafiti wa jambo hilo ili kujua mbivu na mbichi.
 
Upuuzi mpya wa waturuki. Watatue matatizo yao ya ndani waachane na siasa za kipuuzi
 
Usibishe bishe hovyo kwa jambo usilolijua.
Toa ushahidi unaokinzana na wa serikali ya uturuki vinginevyo unapiga mboyoyo zisizo na maana
 
Ni ajabu walimu wa shule kukanusha taarifa zinazopaswa kukanushwa na wamiliki wa shule . hao wamiliki wa shule hawapo mpaka walimu waje wakanushe taarifa ambazo ziko nje ya mamlaka yao ?
 
You Nailed it Bro, nimesoma University na wanafunzi waliosoma Feza, napenda niseme kweli jamaa wapo serious na kitabu na nidhamu ya hali ya juu. tusije tukaentertain mambo ya nje yavuruge mazuri yetu ya ndani.
 

hapo juu nilipo Bold + italics Ongezea Neno Malofa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…