Waziri Mahiga: Serikali ya Uturuki imetuambia wamiliki wa shule za Feza ni magaidi

Kusikia kwa kenge mpaka atoke damu...pale yatakapo tufika ndo tutaanza kumbushana sijui nani alisema

Uchunguzi ufanyike, sio kuishia kusema raisi wa uturuki anataka waminya wapinzani popote walipo.
 
so nawe unaamini kuwa Gullen ni gaidi?,
 
Kwa hii post umejitoa ufahamu kabisa....hivi wanaolalamika kuwa FEZA wanahusika Na jaribio la Mapinduzi huko Uturuki ni serikali ya Uturuki au serikali Tanzania.?
Hifadhi maneno yako mjomba .
 
iyo=hiyo
ata=hata
kua=kuwa
Ukiweza kurekebisha hayo makosa utakuwa umehitimu shule ya FEZA kihalali!
 
iyo=hiyo
ata=hata
kua=kuwa
Ukiweza kurekebisha hayo makosa utakuwa umehitimu shule ya FEZA kihalali!
acha hizo hapa hatuko kwenye kufundishana lugha kama huamini acha iwe ivyo hatuko kubishana hapa. it is non of ur business man
 
acha hizo hapa hatuko kwenye kufundishana lugha kama huamini acha iwe ivyo hatuko kubishana hapa. it is non of ur business man
It is my business sir/madam, as long as you have decided to post your comments in this PUBLIC forum! And yes... we are here to teach and learn, critisize and compromise!
 
ADA elekezi ilishindikana kwa shule za aina hii,kumbe kuna nguvu kubwa namna hii!.Haya mashule ya aina hii ipo siku yataleta mitaala yao yenye utamaduni wao na kuja kuingiza kwetu.
 
Waliosema feza ni magaidi ni serikali ya uturuki na sio dini nyingine, na hata ugaidi wameufanyia uturuki na sio Tanzania, kwa hiyo sioni sababu ya kuwahusisha watu wengine
 
ADA elekezi ilishindikana kwa shule za aina hii,kumbe kuna nguvu kubwa namna hii!.Haya mashule ya aina hii ipo siku yataleta mitaala yao yenye utamaduni wao na kuja kuingiza kwetu.
 
Hapo kunatengenezwa uzushi kuzichafua hizo shule hakuna lingine,tunajua upande flani hauna haki hapa tanzania basi tuachieni hata hivyo vichache jamani.
Yaani wewe ni K kweli kweli. Hizo shutuma dhidi ya Feza schools zimetolewa na serikali ya Uturuki. Uturuki yenyewe ni waislam kwa 85% na serikali yetu ndio ina watetea hao Feza na wala haitaki kuzifungia kwa stupid allegation za Serikali ya Uturuki na Erdogan.
 
Funga shule za magaidi.
Ila beba vitabu vyote watakavyo acha laibrari peleka senti kayumba ili madenti waje wasome senti kayumba

Ng'oa na bati zao peleka kupiga rufu za senti kayumba wasinyeshewe na mvua wala kupigwa jua
 
Magaidi wana alama gani maalumu ya kuwatambua? Gullen kwanza ni nani?
ndo maana umeconclude kabla hayta hujamjua ni nani.
Ngoja nijaribu kueleza bila kufuata reference.
Huyu gullen ni kiongozi wa kidini,yaani imam,huyu ndo walifinince chama cha endorgan kukamata madaraka kupitia kura,chama cha gulen ni cha kiislamu,lakini moderate,hawa kina gullen walipomwingiza endorgan madarakani,alianza kuwageuka,na akaanza kuwa na mwelekeo wa itikadi kali,
hii kitu marekani hakuwa anaikubali na hawakuwa comfortable na utawala wa endorgan,
kwasababu ndoto ya endorgan ni kurudisha ottoman empire,kitu ambacho kwanza kitahatarisha usalama wa israel,
marekani wakaamua endorgan must go,,
wakati huo gullen yuko marekani,lakini ana mtandao mkubwa tu uturuki.
Huu mtandao si wa kigaidi,ni mtandao mfano kama ule wa lowasa,yaani alikuwa na watu katika sector zote.
Sasa hiyo system ndo wamarekani waliitumia kutaka kumpindua endorgan
 
You Nailed it Bro, nimesoma University na wanafunzi waliosoma Feza, napenda niseme kweli jamaa wapo serious na kitabu na nidhamu ya hali ya juu. tusije tukaentertain mambo ya nje yavuruge mazuri yetu ya ndani.
Bahati mbaya mimi nimesoma na wanafunzi masikini kutoka Feza boys. Wanasema wazazi wao hawana uwezo wa kuwasomesha pale. Ila kwakua wako bright na wana ipatia sifa shule ndio maana wakapelekwa pale kusoma.

Nimejiridhisha kua shule ile haipokei weak students.
 
Funga shule za magaidi.
Ila beba vitabu vyote watakavyo acha laibrari peleka senti kayumba ili madenti waje wasome senti kayumba

Ng'oa na bati zao peleka kupiga rufu za senti kayumba wasinyeshewe na mvua wala kupigwa jua
Ni vizuri pia tukang'oe bati za nyumba ya waziri mkuu na makamu wa raisi pale oysterbay tupeleke shule za kayumba pia ni za magaidi.......Udini na siasa ikitawala fikra yako huwezi tofautisha usiku wala mchana.
 
Mmelogwa na nani nyie watu?
Kila kitu mnachomeka udini
Udini unakujaje wakati wanaosema shule ya kigaidi ni waturuki wenyewe?
Waturuki ni wakristo?
Mbona naonaga majina ya kikristo kibao yanafanya vizuri huko huko kwenye shule yenu hiyo?
Kwa akili yako ndogo unafikiri itawaadhiri waislamu tu?
Acheni upumbavu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…