Waziri Mahiga: Serikali ya Uturuki imetuambia wamiliki wa shule za Feza ni magaidi

Waziri Mahiga: Serikali ya Uturuki imetuambia wamiliki wa shule za Feza ni magaidi

Hapo kunatengenezwa uzushi kuzichafua hizo shule hakuna lingine,tunajua upande flani hauna haki hapa tanzania basi tuachieni hata hivyo vichache jamani.
Watu wengine kila sehemu mnatamani kujamba tu, hivi wewe mwislamu mvaa kandambili una jeuri ya kumsomesha mtoto wako FEZA School? Au unadhani ile ni Al almain?

Feza malipo ni kwa dola hakuna hata sheikh ubwabwa mmoja mwenye jeuri ya kupeleka mtoto wake pale.
 
Ndio madhara ya kuruhusu wawekezaji wageni bila kuwa na ubia na raia wa Tz. Serikali ya Tz haina namna kubisha wapewe ushahidi zaidi ya tukio,la sivyo diplomasia yetu na uturuki haitakuwa salama. Hivi leo kuwe na watanzania uturuki wamefanya uharifu Tz,tutahitaji tuwapelekee ushahidi waturuki,wakati hao ni raia wetu,na serikali halali ndiyo inatoa amri hiyo.
 
The bottom line of the entire story ni udini. Shule za FEZA ndio zilionekana kutoa upinzani mkalikwa shule za makanisa na hili lilikuwa halifurahiwi. Kama zilikuwa zinatumia mbinu za kigaidi kufundishia wanafunzi(sijui ndio maana wanafanya vizuri mitihani yao) Serikali ilikuwa wapi wakati wote huo " isiwashughulikie"? Wacheni unafiki wa kidini tena kweupe
Mbona hapo Fedha wakristu ndo wanafaulu sana
 
Watu wengine kila sehemu mnatamani kujamba tu, hivi wewe mwislamu mvaa kandambili una jeuri ya kumsomesha mtoto wako FEZA School? Au unadhani ile ni Al almain?

Feza malipo ni kwa dola hakuna hata sheikh ubwabwa mmoja mwenye jeuri ya kupeleka mtoto wake pale.
Wacha dharau wewe. Kwa uelewa wangu hata kule Zanzibar FEZA school ipo pia licha ya kua idadi kubwa ya watu ni waislamu. Fuatilia uje tena hapa utuambie kua hakuna waislamu wanaosoma hapo.
 
Marekani akikubali hii hoja na wengine watafuata. Huku kwetu bado tunalinda maslahi yetu kwanza.
 
mimi ni mmoja wa wanafunzi nimesoma apo FEZA o-level na high-level. shule za FEZA hazina mtaala wowote unaofundisha ugaidi.

shule ina walimu mchanganyiko waturuki na watanzania. wanafunzi wengine niliosoma nao sasa hivi ni walimu apo FEZA. kwa mfano mkuu wa shule ya FEZA boys alisoma apo O-level baadae akafanya bachelor Uturuki na masters kafanya UDSM.

miaka yote iyo tumesoma mpaka sasa kila mtu anafanya maisha yake sijawahi kusikia ata siku moja mwanafunzi yeyote wa FEZA ambaye amefanya tukio la kigaidi. wengi wetu tumekua watu wema kutokana na mafunzo mazuri tuliyopata pale shuleni.

nimewahi kua moja wa kiongozi wa wanafunzi ila hakuna ata siku moja ambayo tumeelekezwa tufanye tukio la ovyo. shule ziko serious na elimu pekee. shule za FEZA zinajiendesha kutoakana na ada wanazolipa wazazi wa wanafunzi matajiri pia wanafunzi maskini wanasomeshwa kutokana na michango ya wazazi matajiri na baadhi ya wanafunzi waliosoma apo ambao asilimia kubwa wamefanikiwa kimaisha.

ivyo basi kwa mimi binafsi naweza kusema kuwa shule za FEZA hazina uhusiano wowote ule na ugaidi. Uturuki raisi Erdogan amevurugwa tu kutokana na sera zake za ovyo za kuminya demokrasia na ndio maana mpaka leo umoja wa ulaya (EU) wameshindwa kuiruhusu uturuki kujiunga na umoja huo kutokana na uvunjifu mkubwa wa demokrasia.

Waturuki ni watu wanapenda sana biashara na wamesambaa kila kona ya dunia na wamechangia kukua kwa uchumi kwa nchi mbalimbali duniani kwa kutoa ajira kwa wazawa wa mataifa ambayo wanawekeza. kwa mfano ukienda Poland, Germany na mataifa mengi tu ya ulaya jamaa wametoa ajira kwa mamilioni ya watu.

kwa mfano rafiki zangu wengi tu hapa bongo na ata nje ya nchi wanafanya kazi na waturuki na wako vizuri tu. Fethullah Gullen yeye sio mmiliki wa shule za FEZA ila yeye alitoa idea kwa waturuki kuanzisha mashule nje ya uturuki ili kutoa elimu bora kwa mataifa mbalimbali duniani.

Hachangii na wala hapewi ata senti kutoka kwenye shule. uwekezaji hapa bongo wote umefanywa kutokana na ada na michango ya watanzania wachache ambao wameshawishika kuchangia shule.

rafiki yangu mmoja baba yake mzazi ametoa tiles za shule nzima for free. mimi pamoja na wanafunzi wengine tumeshapiga rangi sana shule za FEZA kwa kujitolea. ivyo basi naweza sema shule za FEZA hazina uhusiano wowote ule ayo mambo yao ya ndani ya uturuki wajaribu kumalizana nayo wenyewe.

huo ubalozi kama unajua kuhusu iyo michango ya kigaidi basi wafungie hizo account ambazo zinapewa iyo misaada. Nigeria wamemgomea Erdogan na serikali yake kuhusu kufunga shule za aina ya FEZA ambazo zipo Uturuki ivyo serikali yetu isiyumbishwe kutokana na uyo Erdogan.

shule hizi zinazalisha wataalamu wakutosha ambao wana mchango mkubwa tu kwa taifa ili. rafiki zangu wengi tu sasa hivi ni madiktar katika hospitali za hapahapa nchini, wengine mainjia wazuri tu na wanasaidia mambo mbalimbali.
Umeongea ki Gaidi sana Mkuu
 
Hii topic nilitaka kuianzishia thread siku nyingi nikaamua kuichunia, nilikuwa najua itaibuka tu. Hivi nani hasa amekuwa anafadhili timu zetu za taifa na vilabu kwenda Uturuki, mmewahi kujiuliza kulikoni?
 
Hiyo kauli ya serikali ya Uturuki ni ya kipuuzi kabisa. Shule za FEZA zipo kwenye mataifa mbalimbali zaidi ya 50. Watoto wangu 3 wamesoma FEZA, Mmojawapo akiwa amejiunga mwaka huu. Wawili wa mwanzo waliwahi kutembelea Uturuki mara 2 wakiwa masomoni kwaajili ya mashindano mbalimbali. Wakiwa huko walitembelea majimbo na vyuo vikuu mbalimbali wakikaribishwa na viongozi wa majimbo wa serikali ya Uturuki. Ina maana sahizi ndiyo wamegundua kuwa shule hizo ni za kigaidi? Kwa nini haikusemwa miaka ya huko nyuma?

Huyu Waziri Mkuu alikwishawahi kufungwa alipokuwa mwanachama wa Islamic Party na anatajwa kuwa ni mdini, na wengi wanaomuunga mkono ni wale wenye siasa za mlengo wa kidini, sasa anawageuzia wapinzani wake. Huyu naona ameamua kuiga siasa za baadhi ya viongozi wa Kiafrika, usipokubaliana nao wanataka usifanikiwe katika shughuli zako nyingine ambazo una haki za kikatiba.
Mkuu ni kwamba hutaki kuamini kuwa una Support u Gaidi indirectly kwa ada unayolipa ama hutaki kusikia kuwa wanao wanafundishwa Mbinu za ki Gaidi ?
 
Hayo madai sio kweli. Walimu wapale wanakuja pale kufundisha and they are nice and helpful.
 
Wacha dharau wewe. Kwa uelewa wangu hata kule Zanzibar FEZA school ipo pia licha ya kua idadi kubwa ya watu ni waislamu. Fuatilia uje tena hapa utuambie kua hakuna waislamu wanaosoma hapo.

Kwani waislamu hawawezi kusoma? Mbona hamna point hapa?
 
Watoto Wa wakubwa na matajiri na watu wenye uwezo wao ndio wanasoma shule hizo hawawezi kuzifungia zaidi watawambia wapinzani Wa erdogan popote duniani wake kuwwkeza Tanzania watawalinda... Hizo shule zikifungwa zitakatisha ndoto za watoto Wa vigogo... Hilo haliwezekani ndio maana Ada elekezi ilishindikana
hapohata mtoto wa waziriwa mambo ya ndani anasoma mbona patamu #mwiguluson
 
Awali ilikuwa ni ugomvi wa utofauti wao katika kugombea madaraka kati ya Erdogan na Gullen.

Lakini sasa hivi hao wawili walokuwa marafiki ni maadui wakubwa na tena uadui umechukua sura mpya na sasa imekuwa ni proxy war kati ya Urusi na USA.

Tanzania inatakiwa iwe makini sana katika kushughulikia madai hayo ya wamiliki wa FEZA schools kujihusisha na uhaini kule Uturuki.

Busara na hekima itumike bila hivyo diplomacy itakuwa matatani.
 
Shule zilianzishwa na zinamilikiwa na Ishik Foundation ambayo inafadhiliwa na Waturuki(Mostly Matajiri), hawa wafadhili ni wafuasi wa Gulan (wale wanaofuata falsafa zake). Currently kuna transformation inafanyika katika uongozi wa juu wa Ishik TZ( mfano Mwenyekiti mpya ni Mtanzania), But nakubaliana na wewe kwamba Feza haifundishi Ugaidi ila kwene umiliki ndio tunapotofautiana
Kwani ugaidi unawekwa kwenye mtaala??
 
Awali ilikuwa ni ugomvi wa utofauti wao katika kugombea madaraka kati ya Erdogan na Gullen.

Lakini sasa hivi hao wawili walokuwa marafiki ni maadui wakubwa na tena uadui umechukua sura mpya na sasa imekuwa ni proxy war kati ya Urusi na USA.

Tanzania inatakiwa iwe makini sana katika kushughulikia madai hayo ya wamiliki wa FEZA schools kujihusisha na uhaini kule Uturuki.

Busara na hekima itumike bila hivyo diplomacy itakuwa matatani.
Ingawaje pale Magogoni pana shida kubwa kwenye eneo la diplomatic lakini Mungu mkubwa tunaye waziri sahihi kwa wizara ya mambo ya nje, ni mtu aliyebobea kwenye diplomasia.

Tena chondechonde Ngosha hasichangie comment yoyote kwenye hili maana anaweza kufyatuka akijuwa anahutubia wasukuma kumbe kuna watu serious wanaokusikiliza nukta kwa nukta.

Hili sekeseke aachiwe balozi Mahiga hilo ndilo eneo lake la kujidai, si la wafyatukaji, yeye aendelee na episode nyingine.
 
Hii topic nilitaka kuianzishia thread siku nyingi nikaamua kuichunia, nilikuwa najua itaibuka tu. Hivi nani hasa amekuwa anafadhili timu zetu za taifa na vilabu kwenda Uturuki, mmewahi kujiuliza kulikoni?
Hizi ndio akili za watu waliofirisika ubongo na kuweza kumuuzia timu muhindi mmoja kwa siku moja wakati babu zenu kwa miaka 80 waliijenga timu hiyo.
 
Back
Top Bottom